Lissu hashauriki; Walishindwa Jaji Warioba na Raila Odinga kuhusu NRNE

Huihui2

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
9,727
Reaction score
14,479
Screenshot_20260823_084903_Instagram Lite.jpg

Tarehe 10 Februari 2025
Screenshot_20260823_084151_WhatsApp.jpg

Screenshot_20260823_083923_Chrome.jpg

Raila Odinga na Jaji Mstaafu Joseph Warioba walitoa ushauri mzito kwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, lakini aliuacha hewani kwa msimamo wake mkali. Tarehehe 22 Machi, 2025 Odinga alimkumbusha Lissu umuhimu wa maridhiano na mazungumzo ya kisiasa na serikali, akitolea mfano wa siasa za Kenya. Hata hivyo, Lissu alipuuza somo hilo na kung'ang'ania kauli mbiu yake ya "Hakuna mageuzi, hakuna uchaguzi."
Msimamo huu wa kususia uchaguzi mkuu unaleta wasiwasi mkubwa kuhusu ufanisi wake, kwani historia inaonyesha kuwa kususia uchaguzi hakujawahi kuleta mabadiliko ya kidemokrasia yenye maana duniani. Badala yake, hatua hiyo inawanyima wananchi haki ya kupiga kura na kukiacha chama chake pembezoni mwa ulingo wa maamuzi.
Kwa upande mwingine, Jaji Warioba mnamo tarehe 10 Februari, 2025 alimshauri Lissu kuwa malalamiko yake kuhusu mfumo wa uchaguzi ni ya kweli, lakini ombi lake la kuahirisha uchaguzi kwa miaka mitatu halitekelezeki. Warioba alisisitiza kuwa mabadiliko ya kanuni za uchaguzi yanaweza kufanyika mara moja ili kurekebisha changamoto za kiutaratibu bila kususia uchaguzi mzima. Kwa kukataa ushauri wa viongozi hawa wazoefu, Lissu anaonekana kuendesha siasa za kibinafsi na za msimamo usio na tija kwa mustakabali wa nchi.

Lissu hafai kuwa kiongozi wa kitu chochote
 
View attachment 3655454
Tarehe 10 Februari 2025
View attachment 3655455
View attachment 3655456

Ebu Ansbert Ngurumo (najua yupo humu) arudir kuusoma Uzi wake kama aliyoandika ndiyo yaliyotokea!
Kifupi ushauri waliompa Tundu Antipas Lissu si jambo jipya... Ni siasa za Mbowe tangu 1992.
Maridhiano, majadiliano, handshakes zenye utata na maslahi binafsi!

TAL na WaTanganyika hawataki ubabaishaji, hadaa na viongozi hewa!
 
NRNE si ililetwa na Mbowe baada ya uchaguzi kuvurugwa na CCM ile 2024? Lissu kusimamia hoja hiyo alikosea wapi?

Nakwambia NRNE ndio imeipa heshima chadema na lazima katiba mpya itapatikana kabla ya 2030. Maana Ccm wanajua wakizingua tena basi uchaguzi wa 2030 hautafanyika na pengine pakageuka uwanja wa vita.
 
Sema No reforms no election,Lissu alicheza kama Pele, Heche amesema bila reforms hawaingii kwenye uchaguzi wa 2030, acha kiwake😁
Ifikie wakati ccm waheshimu maamuzi ya wananchi kuchagua viongozi wanao wapenda. Hizi mbinu zao za kitoto za kuiba kura na kuwashinikiza makarani kupiga kura za wagombea wao kwa kutumia majina ya wapiga kura waliosusia hilo zoezi, watambue fika zimepitwa na wakati.
 
Ebu Ansbert Ngurumo (najua yupo humu) arudir kuusoma Uzi wake kama aliyoandika ndiyo yaliyotokea!
Kifupi ushauri waliompa Tundu Antipas Lissu si jambo jipya... Ni siasa za Mbowe tangu 1992.
Maridhiano, majadiliano, handshakes zenye utata na maslahi binafsi!

TAL na WaTanganyika hawataki ubabaishaji, hadaa na viongozi hewa!
Na lilikuwa jambo jema sana. Kauli za Lissu ndiyo zimepelekea watu kuuawa 29/10
 
NRNE si ililetwa na Mbowe baada ya uchaguzi kuvurugwa na CCM ile 2024? Lissu kusimamia hoja hiyo alikosea wapi?

Nakwambia NRNE ndio imeipa heshima chadema na lazima katiba mpya itapatikana kabla ya 2030. Maana Ccm wanajua wakizingua tena basi uchaguzi wa 2030 hautafanyika na pengine pakageuka uwanja wa vita.
NRE ili kauli mbiu tu (unique selling proposition), haikumaanisha kususia uchaguzi. Lissu ali misinterpret ndiyo imemdhuru yuko jela
 
View attachment 3655454
Tarehe 10 Februari 2025
View attachment 3655455
View attachment 3655456
Raila Odinga na Jaji Mstaafu Joseph Warioba walitoa ushauri mzito kwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, lakini aliuacha hewani kwa msimamo wake mkali. Tarehehe 22 Machi, 2025 Odinga alimkumbusha Lissu umuhimu wa maridhiano na mazungumzo ya kisiasa na serikali, akitolea mfano wa siasa za Kenya. Hata hivyo, Lissu alipuuza somo hilo na kung'ang'ania kauli mbiu yake ya "Hakuna mageuzi, hakuna uchaguzi."
Msimamo huu wa kususia uchaguzi mkuu unaleta wasiwasi mkubwa kuhusu ufanisi wake, kwani historia inaonyesha kuwa kususia uchaguzi hakujawahi kuleta mabadiliko ya kidemokrasia yenye maana duniani. Badala yake, hatua hiyo inawanyima wananchi haki ya kupiga kura na kukiacha chama chake pembezoni mwa ulingo wa maamuzi.
Kwa upande mwingine, Jaji Warioba mnamo tarehe 10 Februari, 2025 alimshauri Lissu kuwa malalamiko yake kuhusu mfumo wa uchaguzi ni ya kweli, lakini ombi lake la kuahirisha uchaguzi kwa miaka mitatu halitekelezeki. Warioba alisisitiza kuwa mabadiliko ya kanuni za uchaguzi yanaweza kufanyika mara moja ili kurekebisha changamoto za kiutaratibu bila kususia uchaguzi mzima. Kwa kukataa ushauri wa viongozi hawa wazoefu, Lissu anaonekana kuendesha siasa za kibinafsi na za msimamo usio na tija kwa mustakabali wa nchi.

Lissu hafai kuwa kiongozi wa kitu chochote

Kwa nini mnataka Lissu akubali na siyo Samia. Sasa tumejulishwa kuwa Samia alikataa kukutana na Maaskofu mwaka jana kupokea ushauri.

Wasira tayari keshasema hawatafanya maridhiano na chama. Sasa hapo Lissu anaingiaje? Wamshauri Wasira kwanza.
 
Kupokea ni sawa na ni sahihi kabisa. Kukubali na kuufanyia kazi ni utashi binafsi kutokana na sababu mbalimbali
Unapokataa ushauri wa watu wazima kama Jaji Warioba na Raila Odinga ambao hawana masilahi na siasanza Tanzania, na umewafuata na kuwaomba ushauri, nao ni ukichaa.

Kama una msimamo wako basi usipoteze muda wa wazee wa busara
 
Kwa nini mnataka Lissu akubali na siyo Samia. Sasa tumejulishwa kuwa Samia alikataa kukutana na Maaskofu mwaka jana kupokea ushauri.

Wasira tayari keshasema hawatafanya maridhiano na chama. Sasa hapo Lissu anaingiaje? Wamshauri Wasira kwanza.
Maaskofu wangu wa TEC (Nami ni muumini wa RC) tayari walikuwa wamechagua upande wa kushabikia wakiongozwa na Charles Kitima (anayejiita padre).

Maaskofu wangu walifunga na NOVENA ya zaidi ya mwezi ili lolote litokee dhidi ya Samia kabla ya uchaguzi. Je Samia angeanzaje kwenda kuongea na watu wa namna hiyo?? Wanaomtakia mabaya!!
 
Back
Top Bottom