joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,613
Kenya ni nchi yenye matatizo mengi ya kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa sasa, ukabila, rushwa, ukosefu wa usalama, upungufu wa chakula, migogoro kati ya jamii za wafugaji, miradi ya serikali isitozingatia mahitaji ya wananchi, Covid -19, dhuluma ya umiliki wa athi, vurugu za kisiasa wakati na baada ya uchaguzi ni baadhi tu ya matatizo ya msingi yanayoikabila nchi ya Kenya.
Ukiangalia kwa makini ni kwamba, kwa kiwango kikubwa, Tanzania imefanikiwa sana katika kupunguza kama sio kumaliza kabisa haya matatizo. Kwa akili ya kawaida kabisa, ilipaswa Kenya kujifunza yale mazuri ambayo Tanzania imefanikiwa na ni rahisi kuyamaliza kwa mda mfupi kama kupambana na rushwa, kupambana na ujambazi, kuzalisha chakula, kupambana na Civil -19 na kuzuia ghasia katika vipindi vya uchaguzi, haya ni mambo yanayoweza kudhibitiwa ndani ya muda mfupi bila hata kusubiri BBI na katiba mpya.
Viongozi wa Kenya lazima wakubali kwamba kuna mambo mengi mazuri wanapaswa kuiga toka Tanzania, hakuna faida yoyote ya kujisikia aibu kwa kuiga mazuri yanayofanywa na jirani yako, hata kama ni adui yako, kwa kufanya hivyo Kenya itaendelea kubaki na matatizo bila kujinasua.
"If you can't beat them, join them"