Kama ilivyo kwa watu wengi, nimekuwa nikisikia hadithi na imani mbalimbali za mitaani kuhusu matumizi ya limau. Hivi karibuni, niliamua kunywa maji ya limau kwa wingi. Lengo langu halikuwa kufanya majaribio ya kitabibu, bali ilikuwa ni sehemu ya utaratibu wangu tu wa kawaida.
Huwa nimewahi kusikia kuwa ukitaka kusogeza siku zako ziende mbele unatakiwa kunywa juisi ya malimao. Nikajaribu baada ya kunywa hedhi ikakakta ghafla kwa siku kadhaa ikarudi tena na inasemekana pia kuwa ukinywa limau nyingi kabla ya hedhi kuanza, utapata siku chache sana (kwa mfano siku mbili badala ya tano).
Je, huu ni ukweli wa kisayansi au ni sadfa (coincidence) tu?
Huwa nimewahi kusikia kuwa ukitaka kusogeza siku zako ziende mbele unatakiwa kunywa juisi ya malimao. Nikajaribu baada ya kunywa hedhi ikakakta ghafla kwa siku kadhaa ikarudi tena na inasemekana pia kuwa ukinywa limau nyingi kabla ya hedhi kuanza, utapata siku chache sana (kwa mfano siku mbili badala ya tano).
Je, huu ni ukweli wa kisayansi au ni sadfa (coincidence) tu?
- Tunachokijua
- Kuzuia hedhi (Menstrual suppression) ni njia ya kupunguza au kusimamisha kabisa hedhi kwa kutumia dawa za homoni, hasa kwa ajili ya kusaidia kupunguza dalili kama maumivu makali au kutokwa damu nyingi.
Njia hii hutumia dawa za homoni ambazo hufanya kazi kwenye vipokezi (receptors) vilivyopo kwenye seli za ukuta wa mfuko wa uzazi (uterasi), na kusaidia kuufanya ukuta huo ubaki mwembamba. Ukuta wa mfuko wa uzazi usipojijenga (kutoongezeka unene), huwa ni salama kwa mtu kutopata hedhi.
Madai
Kumekuwapo na taarifa zinazoeleza kuwa wanawake wanaweza kusogeza siku zao za hedhi mbele kwa kutumia limao.
Je, ni salama kusogeza siku za hedhi mbele?
Machapisho yahususyo afya yanabainisa kuwa ni salama kabisa mtu kuamua kusogeza siku zake za hedhi mbele kwa kipindi fulani kama itafanywa kwa usahihi, ni ni kwa mujibu wa daktari wa masuala ya uzazi, Stacie Jhaveri kama alivyonukulia na tovuti ya Clever clinic.
Tovuti ya clever clinic inaeleza kuwa unaweza kuzuia hedhi yako kwa wiki, mwezi ama kwa kipindi kirefu tu. Wanaeleza kuwa watu hufanya maamuzi ya kusogeza siku zao za hedhi mbele kwa sababu kama vile;
- Kutokwa na damu nyingi
- Maumivu makali
- Maumivu ya kichwa
- Matatizo ya kuganda damu
- Upungufu wa damu
Kwa mujibu wa tovuti ya hospitali ya watoto Colorado inaeleza kuwa baada ya kutumia dawa za kusogeza mbele hedhi kwa muda unaotaka na ukaitisha kufanya hivyo pia kwa muda wowote.
Lakini kusogeza mbele siku za hedhi hakuathiri uwezo wa mwanamke kuwa na mtoto hapo baadaye kwa sababu atakapomaliza matibabu yake hayo hedhi itarudi kama kawaida.
Ikumbukwa kuwa machapisho na wataalamu wanaeleza kuwa hakuna njia ya kuzuia hedhi ama kuiondoa moja kwa moja.
Je, unaweza kutumia mbinu gani ili kusogeza mbele hedhi yako?
Kama ilivyoelezwa hapo awali ili kufanikisha jambo hili unapaswa kulifanya kwa usalama kwa kuzingatia ushauri wa kitabibu kutoka kwa madaktari wa masuala ya uzazi.
Kusimamisha hedhi kunategemea njia za uzazi wa mpango zinazotumia homoni. Njia hizi ni pamoja na:
- Vidonge vya uzazi wa mpango (birth control pills)
- Sindano za uzazi wa mpango
- Vipandikizi (implant) vinavyowekwa chini ya ngozi
- Kitanzi cha homoni (IUD ya homoni)
- Pete ya uke (vaginal ring) na Kiraka cha homoni (patch) kinachobandikwa kwenye ngozi
Je, vipi kuhusu limao na kuzuia ama kusogeza mbele siku za hedhi?
Hakuna uthibitisho wa kisayansi kuwa matumizi ya limao ama juisi yake inaweza kusimamisha hedhi yako kwa sababu limao haiwezi kutoa udhibiiti wa kutosha wa homoni kusimamisha hedhi.
Njia nyingine zisizo na uthibitisho wa kisayansi ni;
- Kunywa maji yenye chumvi
- Kunywa maji yaliyochanganywa na siki
- Kutumia tembe za dharura za kuzuia mimba (morning-after pill)
- Kutumia ibuprofen
- Kunywa chai ya majani ya raspberry
- Kunywa juisi ya nanasi