SoC02 Mfumo wa utoaji huduma za afya uanzie kwenye ngazi ya familia ili kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyo ambukizwa

Stories of Change - 2022 Competition

Kiche Jr

Member
Sep 7, 2022
5
13
Magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ni magonjwa ambayo hayasambazwi kwa mtu mwingine kwa kuwa hayana vimelea vinavyohusiana na magonjwa hayo, magonjwa hayo ni Kisukari, Pumu, Selimundu, Saratani, Magonjwa ya Akili, Magonjwa ya Figo, Magonjwa ya Moyo mfano shinikizo la damu na kiharusi. Kutokana na report mbalimbali za Shirika la Afya duniani (WHO), WHO Ukanda wa Afrika na riport mbalimbali za hapa nchini zikiongozwa na report ya wizara ya Afya zote zimetaarifu kuongezeka maradufu kwa vifo vitokanavyo na magonjwa haya.

Taarifa ya wizara ya Afya hapa nchini iliyotolewa na Katibu Mkuu wizara ya Afya Prof Abel Makubi ya tarehe 29/4/2021 ilieleza kuwa Magonjwa haya yameendelea kuathiri jamii yetu na yanachangia kwa kiasi kikubwa katika Idadi ya vifo vinavyotokea nchini yakichangia kwa asilimia 40-45 kwa sasa ikilinganishwa na asilimia 33 kwa Miaka 5 iliyopita.

Mwaka mmoja na miezi minne baada ya Riport hiyo ya Prof Makubi tunapokea taarifa nyingine kutoka wizara ya Afya juu ya uhatari wa Magonjwa haya Waziri wa Afya Mh Ummy tarehe 1/9/2022 alisema " Kuna ongezeko kubwa la idadi ya wahanga wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza nchini. Hii inaongezea mzigo wa gharama za matibabu kwa Serikali na watu binafsi. " Mh Ummy aliendelea kusema kuwa kulingana na Takwimu zilizopo, gharama za magonjwa haya zimeongezeka kutoka Bil 35.65 mwaka 2016/17 mpaka bil 99.09 mwaka 2021/22 . hii hapa ni link ya taarifa ya Mh Ummy Mwalimu Udanganyifu, magonjwa yasiyo ya kuambukiza tishio NHIF

Taarifa ya Mwisho ni utafiti uliofanywa katika Hospitali ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), ulifanywa na Dr Pedro Pallangyo, Dr Makrina Komba na Prof Mohamed Janabi kuanzia Mwaka 2019-2020 na ulifanywa kwa ndugu wa wagonjwa ambao walifika hospitalini hapo wakiwasindikiza wagonjwa katika siku zao za Klinki, Utafiti ulikuwa dodoso juu ya tabia hatarishi zinazopelekea Magonjwa hayo yasiyo ya kuambukizwa, riport yao inasema waliwadodosa watu 40,000 na majibu ya utafiti wao yanasema zaidi ya asilia 96% ya watu wote waliowafanyia utafiti walionekana kuwa na tabia zaidi ya moja hatarishi zidi ya magonjwa haya yasiyo ya kuambukizwa, hii apa ni link ya utafiti huo Non-Communicable Disease Risk Factors Among Caregivers of Patients Attending a Tertiary Cardiovascular Hospital in Tanzania

Taarifa zote hizo tatu, mbili za Wizara na moja ya kutoka Hospitali ya JKCI
zinatuonesha kuwa tunapaswa kuchukua hatua ya udharula ili kuyakabili hayo magonjwa, kama tutachelewa kuchukua hatua sitahiki na za haraka kudhibiti magonjwa haya tutatumia mabilioni ya pesa kutibu magonjwa haya, taifa litapoteza nguvu kazi kubwa, Familia kwa mamilioni zitaendelea kupoteza wazazi na tutaendelea kutengeneza yatima na tegemezi mitaani.

Yafatayo ni mapendekezo yangu kuyakabili magonjwa hayo
1 Wizara ya Afya ianzishe kitengo maalum kwenye vituo vya kutolea tiba hususani katika Idara ya Magonjwa ya nje(OPD) cha kuchunguza(screening) kila mtu anaefika hospitali awe mgonjwa ama ndugu wa mgojwa juu ya tabia/sifa hatarishi za magonjwa hayo, yeyote atakae kutwa na sifa kuanzia mbili ama zaidi utaratibu niliouwelezea katika pendekezo langu la pili kipengele kidogo cha pili (2-II), Utumike.

2. Wizara ya Afya itengeneze sera itakayo waruhusu Madaktari, Nesi, Wataalam wa Maabara, wafamasia na Wataalam wa Ushauri na saa watengeneze muunganiko/Ushirika ambao utasajiliwa kisheria na kuruhusiwa kutoa huduma za afya majumbani (Kwenye ngazi ya familia) Kwa watu wenye sifa hatarishi, dalili na wenye magonjwa yasiyo akuambukizwa, napendekeza jumuiya hizi ziitwe Tasisi ndogo za kutoa huduma za Afya kwenye ngazi ya familia,

Muundo wa Tasisi hizi uwe kama ifatavyo
Tasisi hizi ili zikidhi viwango vya kuanzishwa angalau ziwe na timu ifatayo;
Madaktari : M.D 1/ Clinic Officer 2/ Clinical Assistants 2, Wauguzi 4, Ushauri nasaha; 3 mfamasia 1

Angalau iwe na Wataalam wa Afya wasiopungua 9 wote wawe na leseni na wasiwe watumishi wa serikali ama watumishi wa vituo na hospital binafsi kuondoa mgongano wa kimasirahi .

Kazi zitakazofanywa na Tasisi hizi
I. Kufanya kazi kwa kushirikiana na watumishi wa afya ngazi ya jamii kwa kuibua watu wenye sifa hatarishi za magonjwa haya kwenye jamii na kuanzishiwa utaratibu maalum wa kiafya mfano Tiba rishe, mazoezi n.k ili kutokomeza kabisa mazingira chochezi ya magonjwa haya.

II. Wagonjwa wote wenye dalili za mwanzo za magonjwa haya wanaoibuliwa hospitali kupitia kitengo cha uchunguzi wa awali kwenye idara ya magonjwa ya nje (OPD) waunganishwe na tasisi hizi za eneo husika wanalotoka, ili kuwapatia Elimu ya namna ya kuepuka usugu wa magonjwa haya.

III. Tasisi hizi ziruhusiwe kuingia makubaliano na mgojwa ama ndugu wa Mgojwa ili kumpelekea huduma ya matibabu nyumbani kutokana na hali aliyonayo, mfano huduma ya kuosha vidonda, Elimu na mazoezi ya kupunguza uzito, Huduma za wazee na watu wasio weza kujihudumia.

Hii ni taarifa juu ya Idadi ya watu wanaojiua kwa kujinyonga, kunywa sumu ama kujipiga risasi sababu kubwa ikiwa ni Msongo wa mawazo au Magonjwa mengine ya akili, taarifa hii inasema mwaka 2016 Watanzania zaidi ya 3,000 walijitoa uhai na Tanzania tukuwa nchi ya 4 Afrika kwa kuwa na visa vingi vya watu waliojiua, riport ya dunia inasema kwenye kila sekunde 40 kuna mtu mmoja anajiuwa, ukiachilia mbali riport hiyo ya miaka 6 iliyopita hivi sasa hapa nchini matukio ya watu kujitoa uhai yamekithiri kuliko kipindi chochote kile, hili tatizo nalo tutalitatua kwa kusogeza huduma za ushauri nasaha kwenye ngazi za familia kupitia hizi Tasisi ndogo za afya ninazo zipendekeza Suicide rates rise sharply in Tanzania amid economic, social woes

Faida zitakazo tokana na tasisi hizi ndogo za Afya
Daktari atapata nafasi ya kufika nyumbani kwa mgonjwa jambo ambalo litasaidia si tu kutibu ugonjwa ila pia kuondoa Mazingira kwa magonjwa mengine ya kuambukizwa na yasiyo ya kuambukizwa

Wagonjwa na watu wengine wenye matatizo ya Kiafya watapata muda wa kutosha kuzungumza na kushauriana na Daktari kuliko ilivyo sasa

Jambo hili litatoa mwanya kwa mashirika yaliyo ya kimataifa na ya ndani ya nchi kutoa Misaada ya rasilimali Fedha, vifaa na maarifa ili kutokomeza tatizo hili.

Tutatengeneza Ajira nyingi kwa vijana wetu wanaomaliza vyuo vikuu na vyuo vya Afya na hawapati kazi.

V. Tutapunguza visa vya kulazwa hospitalini kwa wagonjwa wenye Magojwa haya yasiyo ya kuambukizwa.

VI. Tutapunguza Idadi ya vifo na vilema vya kudumu ikiwemo kukatwa Miguu na kushindwa kufanya tendo la ndoa kutokana na athari za magonjwa haya yasiyo ya kuambukizwa.

Ahsante sana
 
Hizo nia zako zote hazitasaidia..hapo utakua unapambana natatizo na wala sio chanzo cha tatizo...ndicho ambacho serikali yako kupitia wizara ya afya inachokifanya.

Kamwe hamuwezi kushindana na magonjwa kwa kusubiri wagonjwa hospitali.

Nakushauri angalia zaidi public health approaches kwenye masuala ya NCD ndio sualuhu pekee ya kudumu kukabiliana na magonjwa hayo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hizo nia zako zote hazita saidia..hapo utakua unapambana natatizo na wala sio chanzo cha tatizo...ndicho ambacho serikali yako kupitia wizara ya afya inacho kifanya...
Asante sana Jiwe kwa ushauri wako, Ukisoma mapendekezo yangu Katika kipengere cha pili Nimependekeza namna ya kuipata task force ambayo itahudumu kuanzia kwenye ngazi ya familia ambapo ndipo chimbuko la magonjwa haya,

Jiwe Tatizo la nchi yetu siyo kwamba hatuna Approaches za kupambana na NCD hapana tatizo letu hatuna task force ya kuzi-Implement hizo Approaches kwenye ngazi ya familia kwenye kiini cha tatizo lenyewe.,

lakini sambamba na hilo ni lazima tuendelee kutibu wale ambao tiyari wanaoyo Magojwa haya na kuwakinga wasipate madhara makubwa ya magonjwa haya ikiwemo ukilema wa kudumu, vifo na n.k

Asante Jiwe Naomba Kura yako.
 
Back
Top Bottom