Life begins at 40 Vs Midlife crisis

Life begins at 40 Vs Midlife crisis

Usianze kuudharau mto kabla haujaufikia ukaona uhalisia kama una kina kirefu au upana gani au una wanyama wakali kabla haujaufikia.

Subiri ufikie midlife crisis kisha uongee khs maokoto ndiyo Kila kitu. Kuna wengine wanayo lakini hawana furaha, moto unawaka kwenye familia zao.
Midlife inakuja na mengi.
E.g. Nguvu za kiume, wakike menopause na majanga yake ya frigidity, magonjwa mengine mengi kama sukari, magonjwa ya moyo, Sonona, n.k.
Mkuu si tunaambiwa maokoto ni ulinzi rejea alichosema mfalme suleimani mhubiri 7:12...
 
Ndugu zangu tusipeane pressure,.sina mke sina mtoto bado najitafuta na nimezaliwa mwanzoni mwa miaka ya 90s,.kwani ndugu zangu maisha ni nini?Why tuko hapa?Lengo la kua hapa ni nini?Muda ambao tupo duniani tunapaswa kuutumia vipi?
Mkuu nasubiria majibu...
 
Maneno "life begins at 40" yana maana kuwa mtu akifika umri wa miaka 40, maisha yanakuwa bora zaidi, labda kwa sababu tayari mtu keshapata skills, experiences na namna bora ya kuyafurahia maisha. Msemo huu ulitungwa na mwanafalsafa Pitkins na umejipatia umaarufu mkubwa hapa duniani.

Katika kusomasoma kwangu nimekuja kufaham kwamba kumbe kuna watu wakifikia 40 wanapata hofu ya maisha(hapo hata mimi nikaanza kuwa na hofu), wanahisi uzee unakuja, ujana unaondoka, vile walivyokuwa wakiyafurahia maisha kama kujirusha, kula ujana vyote vinapotea ghafla.

Tunapoingia umri huu wa 40+, tunaanza kujitambua zaidi, kutambua thamani yetu zaidi na kutojali maisha na mawazo hasi ya wengine. Na hapa ndio hoja inapokuja, kwamba kwa mwafrika wa kawaida je ni kweli kwamba life begins at 40? Maana yapo mengi sana tunafatiliana, mtu kaacha yake anasumbukia ya jirani ili mradi tu amuumize au apate furaha kumuona mwenzake anaumia.

Wanasema at 46 life is at the peak, yaani kumbe ukifika 46 ndio umefikia peak ya maisha yako, baada ya hapo ile graph inaanza kushuka taratibu hadi upigwe chepe. Na wengine wanasema ukifika 40+ unatakiwa uwe tayari umefikia malengo yako kwa asilimia 90, kuzaa, kulea, career, kujenga, kusomesha...

Sasa je, nini kinaleta midlife crisis?

Kwanini katika umri huo mara nyingi tunasemwa kuwa we're going through midlife crisis?

Je, ni kwa sababu huenda hatujafikia malengo yetu ya kimaisha na hivyo kufanya maisha kuwa na ukakasi?

Imagine katika umri huu:
● Huna mke/familia(very optional)
□ Watoto wadogo hawajaanza hata chekechea(kina sie).
● Hujawa na sehemu ya kujibanza(kijumba).
○ Hujawa stable career wise, bado unajitafuta.
Ni lazima kichwa kiwake moto, lazima stress levels ziwe juu na usipoangalia unaweza kupata sonona.

Msije na hoja ya maokoto tu.

Happy Sunday, mtuombee sie wakosefu!!
Kwa upande wangu nadhani sababu kubwa ni hali ya kuridhika na ujana, tunaona kama tutabaki vijana milele wakati muda unazidi kwenda, kuna siku nilipewa ushauri na mzee wangu alinambia "mwanang ukiona maisha yako yanaenda kwa asilimia flani kama ulivotarajia tafuta mwanamke oa anzisha familia mapema iwezekanavyo, hakuna muda sahihi 100% wa kuoa, kila siku kuna changamoto ndogondogo ambazo haziishi ila ukiona una uhakika wa kipato cha kutunza mwanamke oa achana na mambo ya ujana unapoteza muda tuu"
Haya maneno hadi leo yanakumbuka, ni ushauri mzuri ila kweny masikio ya vijana wengi ni kama makelele.
Kuna siku nilimuuliza mzee kwann alinambia hivo akanipa haya majibu;
-ukiwahi kuoa na kupata mtoto wa kwanza kabla hujavuka miaka 25 kichwa kinapata moto haraka sana wakati bado una nguvu(kijana), hii hali itaku-push kupambana sana kwa sababu kuna watu wanakutegemea home
-ukiwahi kuoa na kupata watoto mawazo yako, fikra zako na malengo yako yatakuwa yamenyooka, malengo yako yatakuwa na muelekeo flani, nguvu zako zote utazielekeza kweny maendeleo yako na familia yako, huta kuwa na muda wa kupoteza wa kukaa vijiweni au kwenda viwanja kujirusha.
-ukizaa kabla hujavuka 25, hadi mtoto wako let's say amalize diploma(sidhani kama kuna mwanang nitampeleka advance) atakuwa na miaka 19 plus na yako ww utakuwa 44, uzuri wa hii utakuwa angalau umemaliza part kubwa ya expenses za shule za watoto kabla hujafika uzeeni, ogopa sana kusomesha watoto uzeeni, ukisomesha mtoto wa mwisho uzeeni haina shida ila sio kwa kwanza aisee. Alaf faida nyingine una enjoy watoto wako wakati bado na ww una nguvu, dogo ana miaka 15 ww una 40 inapendeza sio dogo ana 15 ww una 50 ushaanza kuchoka inakuwa haipendez kiasi flani.
-Anyway huu ni ushauri tuu mzee alinipa nadhari tutajifunza kitu humu.
 
Kwa hiyo ulifuata ushauri wa mzee wako?
 
Nilikua natamani sana kufikia third floor, nilivyofikisha nimejiona mwenye furaha sana na naamini my 40 will be much more happier. Eenhe Mwenyezi Mungu nisaidie.

Cheers to this 🥂
 
Niko 77 na ndiyo kwanza kunakucha huniambii kitu ng'wanawane 😁💪

Hizi ni perception za jamii tu ili pengine kuwatia hamasa na kuwaasa walioko huku nyuma wasikakawane kwenye nira za ujana bali wamakinikie zaidi kuanza maandalizi mapema maana ukifika huko 40+ hata process nyingi za mwili zinaanza kukuwashia indiketa kuwa sasa tunahama kwenye msimbo wa ujana na tunaingia kwenye utu uzima sasa.

Hii ni sawa tu na ile perception kwamba eti binti akivuka miaka 30 hajaolewa basi jua lake jema na lililong'aa sana hapo nyuma sasa linaingia machweoni. Na kuna mabinti wasiojitambua ambao kweli wakivuka 30 na bado hawajaolewa wala kuwa na familia wanapaniki badala ya kutulia na kuwekeza katika wao kama wao. Hata katika hili wapo wengi tu wanaofikia hiyo 40+ huku ramani za maisha bado zipo zigzag wanapata sonona hasa wakijilinganisha na baadhi ya waliosoma nao ambao wanakuwa wameshapiga hatua kubwa.

Binafsi kama ningeambiwa leo hii muda urudishwe nirudi huko kwenye 40s kitu pekee ambacho ningekirekebisha ni kuutunza mwili na kujali afya yangu sana. Nisingekunywa mipombe kupindukia na minyama choma hii. Japo ukiwa kijana huwezi kuona madhara yake, ukivuka 45 huku ndiyo sasa utaona kosa ulilofanya - na hapo kama una bahati hujapata presha, kisukari, matatizo ya figo, magonjwa ya moyo na ishu zingine kibao.

Miaka ya 40....kijana linda sana afya yako. Kila kitu kifanye in moderation (ikiwemo ulaji wa mbususu na hata CHAPUTA). Mengine yote ni madogo tu hasa kama unajitambua.

Hint: Usijilinganishe na classmates wako. Hypertension itakuhusu ufe mapema uache makorokocho yako yote uliyoyahangaikia kwa kujinyima sana 😁😁🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🖐

View attachment 2760494
Tawile tawile!
 
Kwa upande wangu nadhani sababu kubwa ni hali ya kuridhika na ujana, tunaona kama tutabaki vijana milele wakati muda unazidi kwenda, kuna siku nilipewa ushauri na mzee wangu alinambia "mwanang ukiona maisha yako yanaenda kwa asilimia flani kama ulivotarajia tafuta mwanamke oa anzisha familia mapema iwezekanavyo, hakuna muda sahihi 100% wa kuoa, kila siku kuna changamoto ndogondogo ambazo haziishi ila ukiona una uhakika wa kipato cha kutunza mwanamke oa achana na mambo ya ujana unapoteza muda tuu"
Haya maneno hadi leo yanakumbuka, ni ushauri mzuri ila kweny masikio ya vijana wengi ni kama makelele.
Kuna siku nilimuuliza mzee kwann alinambia hivo akanipa haya majibu;
-ukiwahi kuoa na kupata mtoto wa kwanza kabla hujavuka miaka 25 kichwa kinapata moto haraka sana wakati bado una nguvu(kijana), hii hali itaku-push kupambana sana kwa sababu kuna watu wanakutegemea home
-ukiwahi kuoa na kupata watoto mawazo yako, fikra zako na malengo yako yatakuwa yamenyooka, malengo yako yatakuwa na muelekeo flani, nguvu zako zote utazielekeza kweny maendeleo yako na familia yako, huta kuwa na muda wa kupoteza wa kukaa vijiweni au kwenda viwanja kujirusha.
-ukizaa kabla hujavuka 25, hadi mtoto wako let's say amalize diploma(sidhani kama kuna mwanang nitampeleka advance) atakuwa na miaka 19 plus na yako ww utakuwa 44, uzuri wa hii utakuwa angalau umemaliza part kubwa ya expenses za shule za watoto kabla hujafika uzeeni, ogopa sana kusomesha watoto uzeeni, ukisomesha mtoto wa mwisho uzeeni haina shida ila sio kwa kwanza aisee. Alaf faida nyingine una enjoy watoto wako wakati bado na ww una nguvu, dogo ana miaka 15 ww una 40 inapendeza sio dogo ana 15 ww una 50 ushaanza kuchoka inakuwa haipendez kiasi flani.
-Anyway huu ni ushauri tuu mzee alinipa nadhari tutajifunza kitu humu.
Vipi wewe uliufata huu ushauri??? na ilikuaje..
 
Wadada wengi hawapendi forty Kwa vile tunaambiwa officially we are out of market....Binafsi I don't care I count is as a blessings Kuna watu wameondoka mapema sana
Sad fact
Women age like milk(mtindi)
Men age like wine(fine wine)
 
Shaggy ft Rayvon kwenye wimbo wa Angel
Kuna Verse inasema:

Life is one big party when you are still young, But who's gonna have your back when it's all done, it's all funny when you are little when you have pure fun
 
Niko 77 na ndiyo kwanza kunakucha huniambii kitu ng'wanawane 😁💪

Hizi ni perception za jamii tu ili pengine kuwatia hamasa na kuwaasa walioko huku nyuma wasikakawane kwenye nira za ujana bali wamakinikie zaidi kuanza maandalizi mapema maana ukifika huko 40+ hata process nyingi za mwili zinaanza kukuwashia indiketa kuwa sasa tunahama kwenye msimbo wa ujana na tunaingia kwenye utu uzima sasa.

Hii ni sawa tu na ile perception kwamba eti binti akivuka miaka 30 hajaolewa basi jua lake jema na lililong'aa sana hapo nyuma sasa linaingia machweoni. Na kuna mabinti wasiojitambua ambao kweli wakivuka 30 na bado hawajaolewa wala kuwa na familia wanapaniki badala ya kutulia na kuwekeza katika wao kama wao. Hata katika hili wapo wengi tu wanaofikia hiyo 40+ huku ramani za maisha bado zipo zigzag wanapata sonona hasa wakijilinganisha na baadhi ya waliosoma nao ambao wanakuwa wameshapiga hatua kubwa.

Binafsi kama ningeambiwa leo hii muda urudishwe nirudi huko kwenye 40s kitu pekee ambacho ningekirekebisha ni kuutunza mwili na kujali afya yangu sana. Nisingekunywa mipombe kupindukia na minyama choma hii. Japo ukiwa kijana huwezi kuona madhara yake, ukivuka 45 huku ndiyo sasa utaona kosa ulilofanya - na hapo kama una bahati hujapata presha, kisukari, matatizo ya figo, magonjwa ya moyo na ishu zingine kibao.

Miaka ya 40....kijana linda sana afya yako. Kila kitu kifanye in moderation (ikiwemo ulaji wa mbususu na hata CHAPUTA). Mengine yote ni madogo tu hasa kama unajitambua.

Hint: Usijilinganishe na classmates wako. Hypertension itakuhusu ufe mapema uache makorokocho yako yote uliyoyahangaikia kwa kujinyima sana 😁😁🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🖐

View attachment 2760494
Ma Story Moob.....
 
Life is how you make it. No matter what age you are. Ukivuka 40 years na kama una uwezo wa kuenjoy, ndiyo usiende kujirusha kwa sababu umevuka umri wa kujirusha? Nani kwani anaweka hizi cut-off points/boundaries? Enjoy kama una uwezo. Life is too short. Kwanza usipoenjoy ndiyo kwanza unajiongezea ma-stress bure. Mara BP hiyo inabisha hodi. Mara kisukari. Mara matatizo ya moyo. Yanini uteseke roho? Narudia, life is how you choose to make it. Has no age boundaries. Do what makes you happy. Muhimu tafuta pesa, na tumia pesa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom