Life begins at 40 Vs Midlife crisis

Life begins at 40 Vs Midlife crisis

Niko 77 na ndiyo kwanza kunakucha huniambii kitu ng'wanawane 😁💪

Hizi ni perception za jamii tu ili pengine kuwatia hamasa na kuwaasa walioko huku nyuma wasikakawane kwenye nira za ujana bali wamakinikie zaidi kuanza maandalizi mapema maana ukifika huko 40+ hata process nyingi za mwili zinaanza kukuwashia indiketa kuwa sasa tunahama kwenye msimbo wa ujana na tunaingia kwenye utu uzima sasa.

Hii ni sawa tu na ile perception kwamba eti binti akivuka miaka 30 hajaolewa basi jua lake jema na lililong'aa sana hapo nyuma sasa linaingia machweoni. Na kuna mabinti wasiojitambua ambao kweli wakivuka 30 na bado hawajaolewa wala kuwa na familia wanapaniki badala ya kutulia na kuwekeza katika wao kama wao. Hata katika hili wapo wengi tu wanaofikia hiyo 40+ huku ramani za maisha bado zipo zigzag wanapata sonona hasa wakijilinganisha na baadhi ya waliosoma nao ambao wanakuwa wameshapiga hatua kubwa.

Binafsi kama ningeambiwa leo hii muda urudishwe nirudi huko kwenye 40s kitu pekee ambacho ningekirekebisha ni kuutunza mwili na kujali afya yangu sana. Nisingekunywa mipombe kupindukia na minyama choma hii. Japo ukiwa kijana huwezi kuona madhara yake, ukivuka 45 huku ndiyo sasa utaona kosa ulilofanya - na hapo kama una bahati hujapata presha, kisukari, matatizo ya figo, magonjwa ya moyo na ishu zingine kibao.

Miaka ya 40....kijana linda sana afya yako. Kila kitu kifanye in moderation (ikiwemo ulaji wa mbususu na hata CHAPUTA). Mengine yote ni madogo tu hasa kama unajitambua.

Hint: Usijilinganishe na classmates wako. Hypertension itakuhusu ufe mapema uache makorokocho yako yote uliyoyahangaikia kwa kujinyima sana 😁😁🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🖐

images (38).jpg
 
Asiwadanganye mtu wanangu. Maisha yanakuja jinsi yalivyo na hakuna wa kujua kesho. Hiyo 40 kama utafika ni uwezo wake Mola kwa wanaoamini hili

Wengi mna bahati kwa sasa kupata nasaha na kushauriwa humu, wengine wamekula maisha bila kujua
Wengine pia hata umshauri vipi bado atakula Bata bila kuwaza kuwekeza

Mimi sikuwa mtu wa starehe bali ni mtu wa kusafiri sana na kuiona Dunia, yaani ndio hobby yangu ila sasa nimepunguza kiasi ingawa bado nasafiri.

Vijana kuweka akiba ni muhimu sana na 40 isiwatishe kwani nina over 60 na bado napiga kazi sana
Nani kawaambia ukifika 46 umezeeka sio kweli.

Pigeni kazi sana mkiwa vijana ili msiwe watu wa kuomba omba baadae.
 
Maneno "life begins at 40" yana maana kuwa mtu akifika umri wa miaka 40, maisha yanakuwa bora zaidi, labda kwa sababu tayari mtu keshapata skills, experiences na namna bora ya kuyafurahia maisha. Msemo huu ulitungwa na mwanafalsafa Pitkins na umejipatia umaarufu mkubwa hapa duniani.

Katika kusomasoma kwangu nimekuja kufaham kwamba kumbe kuna watu wakifikia 40 wanapata hofu ya maisha(hapo hata mimi nikaanza kuwa na hofu), wanahisi uzee unakuja, ujana unaondoka, vile walivyokuwa wakiyafurahia maisha kama kujirusha, kula ujana vyote vinapotea ghafla.

Tunapoingia umri huu wa 40+, tunaanza kujitambua zaidi, kutambua thamani yetu zaidi na kutojali maisha na mawazo hasi ya wengine. Na hapa ndio hoja inapokuja, kwamba kwa mwafrika wa kawaida je ni kweli kwamba life begins at 40? Maana yapo mengi sana tunafatiliana, mtu kaacha yake anasumbukia ya jirani ili mradi tu amuumize au apate furaha kumuona mwenzake anaumia.

Wanasema at 46 life is at the peak, yaani kumbe ukifika 46 ndio umefikia peak ya maisha yako, baada ya hapo ile graph inaanza kushuka taratibu hadi upigwe chepe. Na wengine wanasema ukifika 40+ unatakiwa uwe tayari umefikia malengo yako kwa asilimia 90, kuzaa, kulea, career, kujenga, kusomesha...

Sasa je, nini kinaleta midlife crisis?

Kwa nini katika umri huo mara nyingi tunasemwa kuwa we're going through midlife crisis?

Je, ni kwa sababu huenda hatujafikia malengo yetu ya kimaisha na hivyo kufanya maisha kuwa na ukakasi?

Imagine katika umri huu:
● Huna mke/familia(very optional)
□ Watoto wadogo hawajaanza hata chekechea(kina sie).
● Hujawa na sehemu ya kujibanza(kijumba).
○ Hujawa stable career wise, bado unajitafuta.
Ni lazima kichwa kiwake moto, lazima stress levels ziwe juu na usipoangalia unaweza kupata sonona.

Msije na hoja ya maokoto tu.

Happy Sunday, mtuombee sie wakosefu!!
Kwa Tanzania hiyo principle haifanyi kazi.

Mtu anamaliza chuo at 30.

Anapata kazi at 35.

Anaoa at 36

Hiyo forty inakuwaje?
 
Mi naona Life begins at 25, ukifika miaka 25 akili zote za utoto zinakuwa zimeisha huwazi tena kupiga picha kali, kucheza games, kama ramani hazijakaa sawa na una akili timamu hata usingizi huwa unakata katkat ya usiku wa manane.

Na ukiendekeza mitandao ya kijamii unaona vijana wa umri wako wametoboa unaweza kujikuta hata furaha unakosa kabisa, ni umri mgumu sana vijana wengi wanajitoa uhai hapa 25-35, kwasababu changamoto za maisha zimeanza rasmi.
 
Mi naona Life begins at 25, ukifika miaka 25 akili zote za utoto zinakua zimeisha huwazi tena kupiga picha kali,kucheza games, kama ramani hazijakaa sawa na unaakili timam hata usingizi huwa unakata katkat ya usiku wa manane

Na ukiendekeza mitandao ya kijamii unaona vijana wa umri wako wametoboa unaweza kujikuta hata furaha unakosa kabisa, ni umri mgumu sana vijana wengi wanajitoa uhai hapa 25-35, kwasababu changamoto za maisha zimeanza rasmi
At 25 career wise bado, family bado, maendeleo bado, huenda hata shule bado kumaliza.
 
Asiwadanganye mtu wanangu
Maisha yanakuja jinsi yalivyo na hakuna wa kujua kesho
Hiyo 40 kama utafika ni uwezo wake Mola kwa wanaoamini hili
Wengi mna bahati kwa sasa kupata nasaha na kushauriwa humu, wengine wamekula maisha bila kujua
Wengine pia hata umshauri vipi bado atakula Bata bila kuwaza kuwekeza
Mimi sikuwa mtu wa starehe bali ni mtu wa kusafiri sana na kuiona Dunia, yaani ndio hobby yangu ila sasa nimepunguza kiasi ingawa bado nasafiri

Vijana kuweka akiba ni muhimu sana na 40 isiwatishe kwani nina over 60 na bado napiga kazi sana
Nani kawaambia ukifika 46 umezeeka sio kweli
Pigeni kazi sana mkiwa vijana msiwe watu wa kuomba omba
Sijasema at 46 umezeeka, ila wanasema umri huo upo katikati ya lifespan yako, nguvu na akili zipo kwenye peak yake.

Tatizo ni kujipanga hasa ukiwa kijana, kuna vitu vya msingi mtu anatakiwa kuviangalia ili mambo yasije kuwa mengi katika umri fulani.
 
Huu msemo upo kama inspiration ya kupambana na kujiandaa vyema kwa walio chini ya 40 yrs, kutokana na uhalisia wa maisha ya binadamu akifikisha miaka 40 uwezo wake kwenye mambo mengi unakuwa sio sawa na ilivyokuwa kabla.

Nimejaribu tu kuwaza huenda huwa ni hivyo naomba wale ambao ni 40+ watupe experience yenye uhalisia.
Tofauti utaiona ukiwa apeche alolo, majukumu ni mengi yanakuangalia huna jinsi ya kusolve unajiona hopeless...ukiwa na ukwasi 40 is just a number.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom