ERoni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 43,678
- 90,162
Maneno "life begins at 40" yana maana kuwa mtu akifika umri wa miaka 40, maisha yanakuwa bora zaidi, labda kwa sababu tayari mtu keshapata skills, experiences na namna bora ya kuyafurahia maisha. Msemo huu ulitungwa na mwanafalsafa Pitkins na umejipatia umaarufu mkubwa hapa duniani.
Katika kusomasoma kwangu nimekuja kufaham kwamba kumbe kuna watu wakifikia 40 wanapata hofu ya maisha(hapo hata mimi nikaanza kuwa na hofu), wanahisi uzee unakuja, ujana unaondoka, vile walivyokuwa wakiyafurahia maisha kama kujirusha, kula ujana vyote vinapotea ghafla.
Tunapoingia umri huu wa 40+, tunaanza kujitambua zaidi, kutambua thamani yetu zaidi na kutojali maisha na mawazo hasi ya wengine. Na hapa ndio hoja inapokuja, kwamba kwa mwafrika wa kawaida je ni kweli kwamba life begins at 40? Maana yapo mengi sana tunafatiliana, mtu kaacha yake anasumbukia ya jirani ili mradi tu amuumize au apate furaha kumuona mwenzake anaumia.
Wanasema at 46 life is at the peak, yaani kumbe ukifika 46 ndio umefikia peak ya maisha yako, baada ya hapo ile graph inaanza kushuka taratibu hadi upigwe chepe. Na wengine wanasema ukifika 40+ unatakiwa uwe tayari umefikia malengo yako kwa asilimia 90, kuzaa, kulea, career, kujenga, kusomesha...
Sasa je, nini kinaleta midlife crisis?
Kwanini katika umri huo mara nyingi tunasemwa kuwa we're going through midlife crisis?
Je, ni kwa sababu huenda hatujafikia malengo yetu ya kimaisha na hivyo kufanya maisha kuwa na ukakasi?
Imagine katika umri huu:
● Huna mke/familia(very optional)
□ Watoto wadogo hawajaanza hata chekechea(kina sie).
● Hujawa na sehemu ya kujibanza(kijumba).
○ Hujawa stable career wise, bado unajitafuta.
Ni lazima kichwa kiwake moto, lazima stress levels ziwe juu na usipoangalia unaweza kupata sonona.
Msije na hoja ya maokoto tu.
Happy Sunday, mtuombee sie wakosefu!!