Life begins at 40 Vs Midlife crisis

Life begins at 40 Vs Midlife crisis

Bongo kijana analipwa 1.5 take home, ndani ya five years kajenga ghorofa, ana magari, afa ya mtoto wake Feza schools wala haifanani na kipato chake halisi, huu ni wizi mtupu, kwa wenzetu hakuna mifumo ya maisha ya hivi.
Una uhakika wote wanategemea hela ya mishahara tu kufanya hayo mambo umetaja?

Vipi ikiwa ana biashara zake au ni hela mikopo ya benki au zinatokana na asset za familia?
 
Una uhakika wote wanategemea hela ya mishahara tu kufanya hayo mambo umetaja?

Vipi ikiwa ana biashara zake au ni hela mikopo ya benki au zinatokana na asset za familia?
Hivi ni visingizio tu, Wabongo tunajuwana.

Mtu gari ameweka sticker this car is protected by blood of Jesus halafu jitu ni lishirikina balaa.
 
Hapo kwenye kufurahia life kila siku ni mtihani kweli kweli. Unajua wengi wetu tunaona kama furaha ni kitu cha kukipata ukifanikisha jambo flani lakini ukilifikia, bado unaweka vigezo vingine na mwisho wa siku unakuwa si wa kuyafurahia maisha..

Sometimes nawish ningekuwa na mindset kama ya wamama wa uswazi, unakuta anakaanga mihogo ya kuuza asubuhi ili apate hela ya unga na fungu la dagaa. Baada ya hapo anasindikiza jua kwa umbeya na kama mlevi anakunywa double kiki yake. Maisha yanaenda bila stress

Ila haya ya kuangalia huna gari, nyumba, stable career mara utengeneze image ya kuendana na wenzio, yaani expectations kubwa kubwa ni stress tupu hadi tunashindwa enjoy simple things in life.
Kweli kabisa tuna complicate sana maisha , Mimi binafsi nikipata mahitaji yote ya msingi inatosha na nikifika uzeen nisiwe mtu wa kuhangaika na kuombaomba.
 
Hivi ni visingizio tu, Wabongo tunajuwana.

Mtu gari ameweka sticker this car is protected by blood of Jesus halafu jitu ni lishirikina balaa.
Tanzania bado kuna fursa nyingi sana ya kupiga maokoto ya kutosha, tatizo vijana wengi wanapenda kuajiriwa

Ajira zinapoteza future billionaires wengi sana

Jana vijana 12,332 walikuwa kwenye interview ya TRA inayohitaji custom officer 24 tu

Inasikitisha sana
 
Sidhani kwamba ni kweli wanapenda ajira rasmi, tatizo ni mifumo duni ya kumuandaa kijana kujiajiri, elimu duni toka utotoni(elimu za kukaririshwa).

Mindset zetu ni kuamka asubuhi na kunyonga tai, kupaka kiatu chako rangi king'ae uende "ofisini". Neno "nipo ofisini" linawachanganya wengi sana mkuu.
 
Mimi nimeishi kwenye mifumo mingi duniani, kama hujatembea huwezi kunielewa hata siku moja.

Mifumo ya wenzetu kila mwenye uwezo wa kufanyakazi atafanyakazi na atatimiza majukumu yake yote ya kujikimu.

Kuna watu wa class zote, lakini wizi wa Mali za umma au ubinafsi uliopitiliza hakuna hivyo vitu.

Mbongo anaishi yeye na ana hofu na kesho ya watoto wake wakati mifumo ndio inatakiwa kuamuwa hatima za watu.

Bongo kijana analipwa 1.5 take home, ndani ya five years kajenga ghorofa, ana magari, ada ya watoto wake Feza schools wala haifanani na kipato chake halisi, huu ni wizi mtupu, kwa wenzetu hakuna mifumo ya maisha ya hivi.

Angalia mfumo wa maisha ya Wahindi wengi ni raia halali wa Tanzania umeshawahi kuwaona kuhangaika na ujenzi wa nyumba kwa ajili ya future za familia zao? Wana mifumo yao, kama ya kimagharibi.
Kinachotuua ni mifumo na mindset.

"Upo TRA na hujanunua gari mwaka wa tano huu?" Haya ndio maswali wanaulizwa. "Yani upo NSSF hujajenga hata apartments mbili?". So mtu akiingia huko anapambana hadi kuiba ili afike watu wanapotaka.
 
Nafikiri jambo la msingi ni maokoto tu... ukiwa nayo hiyo mid-life crisis utaisikia kwa jirani......

N.B: Currently nipo kwenye quarter life Crisis
Usianze kuudharau mto kabla haujaufikia ukaona uhalisia kama una kina kirefu au upana gani au una wanyama wakali kabla haujaufikia.

Subiri ufikie midlife crisis kisha uongee khs maokoto ndiyo Kila kitu. Kuna wengine wanayo lakini hawana furaha, moto unawaka kwenye familia zao.
Midlife inakuja na mengi.
E.g. Nguvu za kiume, wakike menopause na majanga yake ya frigidity, magonjwa mengine mengi kama sukari, magonjwa ya moyo, Sonona, n.k.
 
Ndugu zangu tusipeane pressure,.sina mke sina mtoto bado najitafuta na nimezaliwa mwanzoni mwa miaka ya 90s,.kwani ndugu zangu maisha ni nini?Why tuko hapa?Lengo la kua hapa ni nini?Muda ambao tupo duniani tunapaswa kuutumia vipi?
 
Sidhani kwamba ni kweli wanapenda ajira rasmi, tatizo ni mifumo duni ya kumuandaa kijana kujiajiri, elimu duni toka utotoni(elimu za kukaririshwa).

Mindset zetu ni kuamka asubuhi na kunyonga tai, kupaka kiatu chako rangi king'ae uende "ofisini". Neno "nipo ofisini" linawachanganya wengi sana mkuu.
Hapa ndipo inapobidi wabadili mindset zao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom