Life begins at 40 Vs Midlife crisis

Life begins at 40 Vs Midlife crisis

Maneno "life begins at 40" yana maana kuwa mtu akifika umri wa miaka 40, maisha yanakuwa bora zaidi, labda kwa sababu tayari mtu keshapata skills, experiences na namna bora ya kuyafurahia maisha. Msemo huu ulitungwa na mwanafalsafa Pitkins na umejipatia umaarufu mkubwa hapa duniani.

Katika kusomasoma kwangu nimekuja kufaham kwamba kumbe kuna watu wakifikia 40 wanapata hofu ya maisha(hapo hata mimi nikaanza kuwa na hofu), wanahisi uzee unakuja, ujana unaondoka, vile walivyokuwa wakiyafurahia maisha kama kujirusha, kula ujana vyote vinapotea ghafla.

Tunapoingia umri huu wa 40+, tunaanza kujitambua zaidi, kutambua thamani yetu zaidi na kutojali maisha na mawazo hasi ya wengine. Na hapa ndio hoja inapokuja, kwamba kwa mwafrika wa kawaida je ni kweli kwamba life begins at 40? Maana yapo mengi sana tunafatiliana, mtu kaacha yake anasumbukia ya jirani ili mradi tu amuumize au apate furaha kumuona mwenzake anaumia.

Wanasema at 46 life is at the peak, yaani kumbe ukifika 46 ndio umefikia peak ya maisha yako, baada ya hapo ile graph inaanza kushuka taratibu hadi upigwe chepe. Na wengine wanasema ukifika 40+ unatakiwa uwe tayari umefikia malengo yako kwa asilimia 90, kuzaa, kulea, career, kujenga, kusomesha...

Sasa je, nini kinaleta midlife crisis?

Kwa nini katika umri huo mara nyingi tunasemwa kuwa we're going through midlife crisis?

Je, ni kwa sababu huenda hatujafikia malengo yetu ya kimaisha na hivyo kufanya maisha kuwa na ukakasi?

Imagine katika umri huu:
● Huna mke/familia(very optional)
□ Watoto wadogo hawajaanza hata chekechea(kina sie).
● Hujawa na sehemu ya kujibanza(kijumba).
○ Hujawa stable career wise, bado unajitafuta.
Ni lazima kichwa kiwake moto, lazima stress levels ziwe juu na usipoangalia unaweza kupata sonona.

Msije na hoja ya maokoto tu.

Happy Sunday, mtuombee sie wakosefu!!
Kwani babe uko na mid life crisis?
 
Niko 77 na ndiyo kwanza kunakucha huniambii kitu ng'wanawane 😁💪

Hizi ni perception za jamii tu ili pengine kuwatia hamasa na kuwaasa walioko huku nyuma wasikakawane kwenye nira za ujana bali wamakinikie zaidi kuanza maandalizi mapema maana ukifika huko 40+ hata process nyingi za mwili zinaanza kukuwashia indiketa kuwa sasa tunahama kwenye msimbo wa ujana na tunaingia kwenye utu uzima sasa.

Hii ni sawa tu na ile perception kwamba eti binti akivuka miaka 30 hajaolewa basi jua lake jema na lililong'aa sana hapo nyuma sasa linaingia machweoni. Na kuna mabinti wasiojitambua ambao kweli wakivuka 30 na bado hawajaolewa wala kuwa na familia wanapaniki badala ya kutulia na kuwekeza katika wao kama wao. Hata katika hili wapo wengi tu wanaofikia hiyo 40+ huku ramani za maisha bado zipo zigzag wanapata sonona hasa wakijilinganisha na waliosoma nao ambao wanakuwa wameshapiga hatua kubwa.

Binafsi kama ningeambiwa leo hii muda urudishwe nirudi huko kwenye 40s kitu pekee ambacho ningekirekebisha ni kuutunza mwili na kujali afya yangu sana. Nisingekunywa mipombe kupindukia na minyama choma hii. Japo ukiwa kijana huwezi kuona madhara yake, ukivuka 45 huku ndiyo sasa utaona kosa ulilofanya - na hapo kama una bahati hujapata presha, kisukari, matatizo ya figo, magonjwa ya moyo na ishu zingine kibao.

Miaka ya 40....kijana linda sana afya yako. Kila kitu kifanye in moderation (ikiwemo ulaji wa mbususu na hata CHAPUTA). Mengine yote ni madogo tu hasa kama unajitambua.

Hint: Usijilinganishe na classmates wako. Hypertension itakuhusu 😁😁🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🖐

View attachment 2760494
Hapo kwa wanawake imeongea ukweli mtupu. Wakina dada wakiwekeza kwa wao kama wao watafika mbali sana. Haijalishi wapo umri gani. Kuna traits binti anakuwa nazo,mwanaume unatamani kuweka ndani regardless ya umri kabila au dini. Hii ipo hata kwenye kazi na fursa nyingine. Unaweza kuwa a potential wife Material regardless of your age. You have to invest in your worthiness.
 
Kuhusu kujenga huwa naona watu wanajibana sana, kwanini ukimbilie kujenga?? Mimi binafsi huwa sioni sababu ya kujenga mapema, labda nitajenga nikiwa hapo kwenye 40 - 45. Ukishayapangilia vyema maisha yako around 27 - 30 ukajua either nahitaji kuwa na familia au la, nahitaji kujenga nikiwa na 40 yrs au la, Career yangu ni hii au la etc then maisha yako ukiwa 40 yrs natumaini yatakua matamu sana
Mimi naungana na wewe kidogo ni muhimu kuwekeza kwenye ardhi. Yaani usiache shamba ukipiga mshindi au kama una hela badala ya kuweka bank nunua ardhi.
 
Niko njian kuongeza mke sijafika 40 na niko over 35 na maokoto ni wastani tu no mater wht
Sio mbaya mkuu jitaidi uwahi....kuna umri ukifika kufanya maamuz magumu kama ayo ni kujitafutia kifo tu...

mi nko naingia 30....nmeshajipanga mwakani nafanya maamuzi magumu naoa wawili Ndani ya wiki moja.....ili ikifika uzeeni in shaa Allah nijue nani wa kula nae maokoto..
 
Huu msemo upo kama inspiration ya kupambana na kujiandaa vyema kwa walio chini ya 40 yrs, kutokana na uhalisia wa maisha ya binadamu akifikisha miaka 40 uwezo wake kwenye mambo mengi unakuwa sio sawa na ilivyokuwa kabla.

Nimejaribu tu kuwaza huenda huwa ni hivyo naomba wale ambao ni 40+ watupe experience yenye uhalisia.
kabisa tujiandae japo kama vile tumechelewa hivi
 
Sio mbaya mkuu jitaidi uwahi....kuna umri ukifika kufanya maamuz magumu kama ayo ni kujitafutia kifo tu...

mi nko naingia 30....nmeshajipanga mwakani nafanya maamuzi magumu naoa wawili Ndani ya wiki moja.....ili ikifika uzeeni in shaa Allah nijue nani wa kula nae maokoto..
Sahihi kabisa
 
Kibongobongo ni hivyo hivyo 40 Mwili unaanza kukukataa lazima uwekeze mapema ukifika 40 uanze kula pension yako ya kile umeweka before 40 Ila tafsiri yake nmekuelezea vizuri

Hujaelewa kwanini wanasema unapoomba kazi usivuke 45? Hapo Mwili tayari ushaanza kukukataa Ila unaulazimisha hivyo hivyo tu utafanyaje na wewe unataka upige maokoto
Ujumbe wako nimurua sana, brother!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom