Life begins at 40 Vs Midlife crisis

Life begins at 40 Vs Midlife crisis

I Think maisha hua yanaanza kuonekana yako speed pale unapoanza kupata watoto.
Because, hapo ndo hua tunaanza ku calculate umri.
Mfano umepata mtoto wa kwanza at 35 yrs as a man unapiga hesabu kuwa on average hadi amalize form six ni 19 yrs. So ukijumlisha na 35, unakua na 54yrs, tayari ndo unastaafu at 55. Hapo bado hajaenda chuo.
Na hapo hujapata wengine. Hiyo ndo inafanya kichwa iwake moto kabisaaaa
Kuna usenge tulikuwa tunaambiwa kuhusu maisha tusingeufuata pengine tusingekuwa na majuto kama hivi.
 
Hakuna kitu inavuruga kama kukimbilia kupata watoto haraka haraka. Mimi na 26yrs watoto 2 mama tofauti wananipeleka puta hadi sometimes najuta. Mpaka kufika hiyo 40 nitakuwa nishachoka

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
 
Well I am 41. I think naweza kusema kidogo. Kwanza, ni neema ya Mungu kwamba nimeweza kufika huu umri. Pili katika umri huu nimeweza kuwa na familia nikimaanisha mke na watoto. Tatu walau maisha ya kawaida ya kula na kunywa na kusomesha watoto shule zinazoitwa "english medium" hayasumbui. Nne nimeona at 40 kama Mungu amekujaalia afya bora ya mwili na akili unaweza kuiinjoy dunia hii kuliko kipindi kingine katika maisha yako. Uwezo wa kiuchumi unakuwepo, na pia usipoharibu sana heshima katika jamii unakuwa nayo.
 
Hakuna kitu inavuruga kama kukimbilia kupata watoto haraka haraka. Mimi na 26yrs watoto 2 mama tofauti wananipeleka puta hadi sometimes najuta. Mpaka kufika hiyo 40 nitakuwa nishachoka

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
Utakuja kuiona faida yake braza very soon..Mimi pia case yangu ilikua kama ya kwako. Kwako hiyo ni bonge la advantage unaweza usione saa hii kwakua ni mziki kuwatunza.
But believe me ugumu unaokutana nao kumbuka bado una nguvu za ku force..imagine unakua na vitoto vidogo ukiwa na 40 halaf mishe haziend..!!ungepagawa mara 100.

Mimi nilizaa at 22 mwaka wa 1 chuo.
 
Miaka 40+ wanasema umefikia peak ya graph ya maisha.
Nimepitia maoni kadhaa! Wachangiaji wengi bado vijana na hamjui miaka 40 ni umri wenye tafsiri hipi katika muktadha wa kutambulika katika jamii!. Miaka 40 bado sana una nguvu na fursa nyingi za kujitafuta na kujipata! Hata ajira serikalini bado hazijakutupa mkono. Umri wa kuanza kuwa na wasiwasi ni kuanzia 55 mpaka 60! Huu umri kama umepitia msoto wa kuminya ubora wa lishe, malazi, na mahusiano, huwe na uhakika fikra zako zitakuwa hovyo (mkubwa lakini hovyo) na mizania ya mwonekano utakuwa wa kushuka chini na kiwango chako cha uzalishaji au kuchangia kimawazo katika jamii unawa umedhoofu!. Lakini kwa wengi wa watu ambao makuzi na malezi yao yalikuwa bora, umri huu wa 56 - 60 ni umri wa mchango wao katika jamii kuwa mkubwa! Watu wakubwa katika jamii kiuchumi, kisiasa, kielimu, kiushawishi katika nyanja mbalimbali za kimaisha angalia umri wao ni beyond 60s. Kwahiyo, vijana kama una umri wa 40, bado sana kupambana!
 
Ni kweli Maisha yanaanza 40, umri huo unategemewa uwe umejiandaa na uzee, umeshawekeza, unamalizia malizia vitu vidogo vidogo ili ukifika 50 upumzike ule mafao, uenjoy maisha yaliyobaki, ujiandae na magonjwa na jinsi ya kupambana nayo,

Ukifika 40, bado huna ramani lazima hofu ikuingie, uwe depressed na wengi huanza kukata tamaa kwa kujihisi ndio basi, kumbe 40 inakupa last chance ya kupambania kujiandalia 50 yako,

Wito wangu kwa vijana tupige kazi bila kuchoka, fainali uzeeni.
😘😘
 
Japo under 40 wanajiona bado vijana na pengine wana fursa kibao mbele yao lakini at 40+ unakuwa katika nafasi ya kutengeneza fursa kwa wale walio chini yetu kiumri. Hizi umri hazipaswi kuwa vita, tunategemeana sana.
 
Atoto how old are you🤪🤪(najua hatutuhusiwi kuwauliza wadada umri), have u ever thought ukiapproach 40 itakavyokuwa?
 
Sababu pesa ni chombo cha kufanyia kazi kiuchumi, sasa kukiweka ndani ni kuzuia kufanya kazi hivyo ni sawq na kuwa na shamba usilolima

Pua pesa inashuka thamani kila kukitokea mfumko wa bei, japo ni kwa kiasi kidogo sana cha asilimia ila taratibu thamani inashuka kila mwaka 1%-6%

Badala ya kutunza pesa, kinachotakiwa ni kuitoa pesa ikafanye kazi na wewe kukusanya mali (asset) ila usinunue viti vinavyohitaji pesa kuvitunza (liability).

Au kama sio kununua mali, basi itoe pesa yako ikafanye kazi kwa njia ya hisa au mitaji kwenye biashara za watu, sio lazima kila mtu afanye biashara ila ni muhimu kila mwenye pesa aitoe ikafanye biashara/uzalishaji.

Mimi sio mtaalamu wa uchumi, ila ni jambo nililojifunza kwenye mihangaiko ya maisha Mkuu, so sitaweza kujibu maswali technical ya kiuchumi.

Labda kama una maswali yahusuyo sheria, mf. Namna gani unaweza itoa pesa yako ikafanye kazi kwenye biashara za watu na ubaki salama huku ukipata faida, hapo ntakujibu kwa ufasaha.
Umenielewa vibaya nikisema Tunza kibunda chako huwa namaanisha kuivest pesa yako either kwenye biashara......nk ili iongezeke kadri siku zinavyokwenda na uweze kumeki faidi.sjui apo umelewa??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom