LHRC, THRDC na JUKATA wasema Kutoa elimu ya Katiba kwa miaka mitatu, itafika 2030 bila Katiba mpya

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Wanaharakati wa Katiba na Haki za Binadamu wamekosoa kauli ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro juu ya kutoa elimu ya Katiba kwa kipindi cha miaka mitatu, wakidai mpango huo unalenga kuchelewesha mchakato na upotezaji wa fedha za umma.

Tamko hilo limetolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) na Jukwaa la Katiba (JUKATA) likieleza Elimu ya Katiba mpya imeshatolewa na Tume ya Jaji Warioba na Bunge la Katiba, hivyo fedha zilizotengwa zitumike kuanzisha mijadala kuendesha mchakato shirikishi na waharaka.

Wanapendekeza muda wa kuandaa Katiba hadi ipatikane na kutumika usizidi miaka mitano, kwa kuwa kutoa elimu kwa miaka mitatu kunaweza poteza muda mwingi wa kuandaa mchakato na inaweza kufika Mwaka 2030 wakati wa Uchaguzi Mkuu pasipokuwa na Katiba mpya.

LHRC.JPG

Wanaharakati wa Haki za Binadamu wakizungumza na Waandishi wa habari wakati wakitoa tamko la kupinga mpango wa Serikali wa kutoa elimu ya katiba kwa miaka mitatu wakidai hatua hiyo ni kupoteza muda na fedha za wananchi.
Tamko la Pamoja katiba_page-0001.jpg

Tamko la Pamoja katiba_page-0002.jpg

Tamko la Pamoja katiba_page-0003.jpg

Tamko la Pamoja katiba_page-0004.jpg
 
Hii serikali ya CCM inashangaza sana. Inafanya mambo yake kwa kujilinda zaidi badala ya kutazama maslahi mapana ya watu wote..

Na ishangaza zaidi kwa sababu, kile serikali na CCM wanachopaswa kufanya nyakati na majira haya hawakifanyi na badala yake wanafanya kisichopaswa kufanywa sasa.

Hivi tunadhani CCM wataponaje kwa mwendo wao huu? Hivi hii serikali ya CCM chini ya Rais Samia Suluhu Hassan itaepukaje anguko lake kama wanaishi katika giza la upofu mkuu namna hii..?

Sasa kwenye mchakato wa katiba unawaita na kuwashirikisha wazee mawaziri wakuu na viongozi wengine wastaafu tena wote toka CCM ili iweje?

Ni kana kwamba swala la katiba mpya linawahusu wastaafu wa CCM badala ya kuelewa kuwa ishu ya katiba mpya ni ishu ya wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa au imani zao..!

Oooh, Asante Mungu Yehova uishiye milele kwa maana umemtia wazimu na upofu wa fikra FARAO WA TANGANYIKA ili utukomboe watu wako toka ktk kongwa na gereza liitwalo CCM...
 
Mi mwenyewe najiuliza miaka 3 yote hiyo ni elim gani hiyo itatokewa na gharama zote hizo abebeshwe huyo huyo anaeelimishwa hadi mchakato uje uishe na katiba kupatakana more than 5 years!

Hivi ccm inawachukuliaje wanchi wa Tanzania?

Wao ccm ndo wanahitaji elimu ya uongozi.
 
Back
Top Bottom