Leonardo Da-Vinci

Leonardo Da-Vinci

Kwanini ni lazima?

Yesu alisema "mimi ndio njia ya kweli na uzima,mtu haji kwa baba ila kwa mimi"
Kwanini unadhani nahitaji dhehebu?

umenibana kwenye kona. ila nitachomoka
kwa asili ya ukristo huku kwetu afrika kuzijua habari hizi lazima utakuwa ni muumini wa moja kati ya madhehebu ambapo utakuwa umesoma biblia.
najua utasema umemjua yesu kupitia biblia ambayo haina dhehebu. sawa sitakataa ila kwetu sisi hata hiyo biblia na mafunzo yake mostly ni kupitia makanisa. huwezi niambia from no where umeanza kusoma tu biblia peke yako nyumbani kwako kama hujajishikiza katika dhehebu fulani la ukristo.
 
Kwanini ni lazima?

Yesu alisema "mimi ndio njia ya kweli na uzima,mtu haji kwa baba ila kwa mimi"
Kwanini unadhani nahitaji dhehebu?

kuwa na dhehebu si lazima, lakini kwetu mfn hapa tanzania hakuna mtu ambaye ni mkristo tu.
hata ulokole ni aina ya dhehebu.
 
Bila samahani!
Mimi ni mkristo lakini sina dhehebu!

inaonesha mimi na wewe tunafanana kimtazamo ila najaribu kutafuta tunapopishana wapi bado hapajawa clear kwangu. inaelekea ni padogo sana.
 
umenibana kwenye kona. ila nitachomoka
kwa asili ya ukristo huku kwetu afrika kuzijua habari hizi lazima utakuwa ni muumini wa moja kati ya madhehebu ambapo utakuwa umesoma biblia.
najua utasema umemjua yesu kupitia biblia ambayo haina dhehebu. sawa sitakataa ila kwetu sisi hata hiyo biblia na mafunzo yake mostly ni kupitia makanisa. huwezi niambia from no where umeanza kusoma tu biblia peke yako nyumbani kwako kama hujajishikiza katika dhehebu fulani la ukristo.

Kwanza ni kweli watu wengi wamekuwa Wakristo kwa kuwa wamezaliwa akakuta wazazi wao wako kwenye madhehebu
Lakini namna yako ya kufikiri kuwa ni LAZIMA kila mfuasi wa kristo awe ameanzia kwenye dhehebu ina matobo matobo sana

Siku hizi watu wanazipata habari za Yesu bila kuanzia kwenye dhehebu lolote,hivyo kusema na lazima utakuwa umejiweka kwenye mazingira mabaya sana

Halafu sijaona msingi wa wewe kujua dhehebu langu kwenye mjadala huu japokuwa nimekujibu swali lako,naomba tu uamini kuwa mimi ni mfuasi wa Kristo,hiyo inakutosha!
 
kuwa na dhehebu si lazima, lakini kwetu mfn hapa tanzania hakuna mtu ambaye ni mkristo tu.
hata ulokole ni aina ya dhehebu.

Unaendelea kujifunga kwenye kamba ambayo hutaweza kujifungua!
Kwanini unasema hapa tanzania hakuna mtu ambae ni mkristo asiekuwa na dhehebu?
Inaonekana wewe unaishi kimazoea sana!

Ni uchunguzi gani umeufanya ukajua hakuna Mtanzania ambae hana dhehebu?
 
nimemjua kupitia tafakari zangu juu ya mambo mengi, ukijumlisha na habari mbalimbali ambazo wengine waliziandika kumuhusu. lakini pia nimemuexperience.

Kitendo cha wewe kusema kuwa unamuamini Mungu wa Ibrahim,Isaka na Yakobo tayari wewe ni muamini wa Biblia,sasa niambie ni kitu gani kimekufanya umuamini huyu Mungu ambae ameandikwa kwenye maandiko ambayo huyaamini?[rejea maswali yako uliyoniulia kuwa hayo maandiko umejuaje ni neno la Mungu?]

N kumbuka huyu Mungu hata kama umemjua kupitia tafakari zako bado ni yule wa kwenye Biblia!
 
inaonesha mimi na wewe tunafanana kimtazamo ila najaribu kutafuta tunapopishana wapi bado hapajawa clear kwangu. inaelekea ni padogo sana.

Tofauti yangu mimi na wewe ni hii:
Wewe hauiamini Biblia kama ni neno la Mungu na ni kamilifu
Mimi naiamini Biblia kama ni neno la Mungu na ni kamilifu!
 
kulikoni hata ukafikia kusema hayo? na mambo gani?

Ni mambo mengi sana
Kuanzia madai yao ya kwamba Petro ni papa wa kwanza wa kanisa hilo
Historia nzima ya Ukristo n.k
Mambo ni mengi sana lakini nakushauri kitafute kitabu cha William Shao kinachoitwa MIAKA 2000 YA UKRISTO,HISTORIA ILIYOPOTOSHWA,kitakufungua macho!
 
Ha ha ha.. Ukweli utabaki kuwa ukweli na kamwe hautopotoshwa na mtu yeyote....Labda jina pope linakupa taabu..Kwa kifupi ni kwamba St. Peter ndo kiongozi wa kwanza wa Kanisa...Period...

Kanisa katoliki ndo lime-compile na ku-edit bible hiyo unayoisoma sasa...Injili zilikuwa 23..Kanisa(Holy catholic) imezichambua ikatupa 4 ambazo hazina ishabiki ndani yake...Ukitaka kujua zilizo baki kavunje Vatcan uzichukue uzisome na ujue ni kwanini zomeondolewa.....

Petro atabaki kuwa the first pope upende usipende...Historia huwa haipotoshwi...

Halafu kwanini unataka kutuaminisha kuwa huyo William Shao ndo mkweli...? Ukweli kwako unaweza ukawa si ukweli kwangu....Ndugu wewe ndo unahitaji kufunguliwa macho yako maana upo gizani na mafundisho ya kupotoshwa...
 
Ha ha ha.. Ukweli utabaki kuwa ukweli na kamwe hautopotoshwa na mtu yeyote....Labda jina pope linakupa taabu..Kwa kifupi ni kwamba St. Peter ndo kiongozi wa kwanza wa Kanisa...Period...

Kanisa katoliki ndo lime-compile na ku-edit bible hiyo unayoisoma sasa...Injili zilikuwa 23..Kanisa(Holy catholic) imezichambua ikatupa 4 ambazo hazina ishabiki ndani yake...Ukitaka kujua zilizo baki kavunje Vatcan uzichukue uzisome na ujue ni kwanini zomeondolewa.....

Petro atabaki kuwa the first pope upende usipende
Sawa lakini naomba ushahidi wa madai yako haya!
...Historia huwa haipotoshwi...
Una uhakika na haya maelezo yako?

Halafu kwanini unataka kutuaminisha kuwa huyo William Shao ndo mkweli...? Ukweli kwako unaweza ukawa si ukweli kwangu....
Wapi nimetaka kuwaaminisha?
Mimi nimesema katafute hicho kitabu wewe unasema nataka kuwaaminisha,kivipi?
Ndugu wewe ndo unahitaji kufunguliwa macho yako maana upo gizani na mafundisho ya kupotoshwa...
Nimepotoshwa kwa mujibu wa nani?
 
Umepotoshwa kwa mujibu wa huyo muandishi
huyo William Shao anayetaka kukuaminisha uongo kuwa ni kweli...Mkuu Ant-Catholic wengi huwa wanapotosha mafundisho ya kanisa.....Ukweli ndo huo....Hata hiyo biblia unayoisoma ina vitabu lukuki vilivyo ondolewa na Kanisa kwasababu vilikuwa vya kishabiki zaidi.....Kwakifupi hata hiyo biblia yako imekuwa edited na Kanisa sana sana upande wa agano jipya...

Mfano ni Injili ya Maria, Injili ya Barnaba, Injili ya Thomas, Matendo ya Petro na vitabu vingine vingi viondolewa na kanisa(Catholic) kwasababu vimejaa ushabiki.....Kama unasema kanisa limepotosha basi ni Bora uitupe hiyo Bible yako mbali maana kanisa unalosema limepotosha mambo mengi ndo lime-edit na ku-compile hiyo bible yako.....
 
Ingekuwa hayo ni maandishi ya Marko au Luka kungekuwa na cha maana
Hivi si u-google tu ili ujue huyo jamaa aliishi mwaka gani?

Halafu jiulize ni kwanini michoro yake ichukuliwe serious kiasi hiki?
Kwani Da vinch ni nani?

Kila mtu anajua hiyo ni picha ya kubuni ni sawa na yule jamaa aliecheza filam ya Yesu aitwe au kuchukuliwa ndie Yesu!
Pathetic!!

Wewe Mchungaji na Yesu wako! Kila akitajwa au akipewa challenge kidogo tu unapagawa! Yeye myahudi na wewe mmatumbi wapi na wapi?

Besides hivi wewe unaweza kutoa criticism yoyote ile dhidi ya Da Vinci kweli? Katika uwanda upi utampinga? Science, maths, astronomy, painting, etc?
 
Ni mambo mengi sana
Kuanzia madai yao ya kwamba Petro ni papa wa kwanza wa kanisa hilo
Historia nzima ya Ukristo n.k
Mambo ni mengi sana lakini nakushauri kitafute kitabu cha William Shao kinachoitwa MIAKA 2000 YA UKRISTO,HISTORIA ILIYOPOTOSHWA,kitakufungua macho!

Mchungaji,

William Shao ni nani?
 
namuamini mungu aliyeumba mbingu na dunia na vyote vilivyomo, aliyekuwapo yupo na atakuwapo milele. mungu huyo wengine wametokea kumuita yehova, lakini ndiye mungu huyo aliyekuwa wa wa musa yakobo isaya na wengine wengi.

mungu hana jina. ni mungu.
nafikiri nimejaribu kukujibu.

huyo Mungu unayemuongelea ni wa watu watatu, Ibrahim, Isaka na Yakobo na labda wajukuu wao. Sasa wewe mmatumbi huyo Mungu hawezi kuwa wako. Wako yuko huku Africa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom