Alafu hebu nikwambie jambo moja kuu ambalo huenda ukawa hujanisoma, Kitakachotofautisha kuabudu Mwenyezi MUNGU na kumuabudfu shetani ni matendo yako. Nasema hivo kwasababu wachamungu wa kweli wana sifa zo zilizojipambanua na ukweli wa nafsi zao, unaombatana na matendo. mfano,Utasema unamuabudu Mwenyezi MUNGU wa kweli, lakini matendo yako yatasema unamuabudu yupi kwani hayo hayakosei kitu, unakwenda nyumba ya ibada kila siku lakini ni mwizi, unawatendea ubaya wazazi, unauwa, mla rushwa, unawdharau walemavu, una wazini wake wa jamaa zako, mlawiti, mwongo ........... obviously wewe utakwenda kwa huyo mungu unaemuabudu ambaye ana tabia hizo, kwakuwa hizo ndio tabia zake basi na kwakuwa yeye ana nguvu kukushinda wewe maana ulishajisalimisha kwake sasa we ndio utaanza kulipa kwani atakufanyia hayohayo.
Kama unawatendea wazazi wema, unawajali kila kiumbe bila kudharau maumbile yao, si mlawiti, si mwongo, ................. hakika utakwenda kwa MUNGU mwenye sifa hizo. Nadhani umenisoma bro. Kama unadhani mti ndio umeumba dunia na kila kilichomo basi uabudu huo na huko kwa huo mti ndio yatakuwa marejeo yako halafu huo mti utasema nawe aidha ukubali kuwa wenyewe ni MUNGU MUUMBA wa kila kitu ama ukukatalie kuwa sivyo hivyo, Hapo utajua ukikataliwa na huo mti utakwenda wapi? Tafakari juu ya UUNGU inahitaji hekima kubwa sana, si mhemko wa nafsi, ama matamanio yako ama ya dhehebu lako kama unavolazimisha tutaje jina la MUNGU, Jina lake ni YUPO AMBAYE YUPO, Yeye mwenyewe husema "MIMI NIPO AMBAYE NIPO". Halafu kwa kukusaidia tu, ni kwamba MUNGU hatambuliwi kwa jina bali kwa sifa zake ambazo ndizo UTUKUFU WAKE. Sifa hizo ndizo walizofundisha manabii, hawakuwa busy kufundisha jina la MUNGU bali walifundisha sifa zake na nini cha kufanya ili hatimaye akakupokee katika himaya yake na kukupa yaliyo mema. Ukiniambia huyu mbuzi ni MUNGU, Mi nakuja namchinja halafu nakwmbia nimechinja MUNGU WAKO, haya kaumbaje dunia na vilivyomo kama yeye mwenyewe amechinjwa na ameliwa? Akili kichwani Mwako. Ahsante