Leo nimeota nacheza Mpira namba 11 ambapo mimi nachezea mguu wa kulia. Hii ina maana gani?

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,327
8,243
Habarini wakuu,

Leo nimeota ndoto ya ajabu, naiita ya ajabu kwasababu ni mambo ambayo sipendi kuyafanya kwasasa japo nilikua nikifanya zamani.

Nimeota nacheza mpira namba 11 ambapo mimi nachezea mguu wa kulia. Japo mara ya mwisho kucheza mpira ni miaka kumi iliyopita.

Ndoto ilianza hivi nikaota tupo uwanjani timu mbili zikawa zinacheza. Timu inayocheza kutokea gori la kushoto kwenda kulia ikawa inafungwa. Sikuelewa kilichoendelea baadaye nikajikuta nipo ndani ya uwanja namimi nacheza namba 11 kufunga kwenye gori la kushoto.

Kiukweli nilikua nacheza vizuri, nakumbuka nilipewa pasi ndefu nikaipokea nikapiga shuti la mbali nikafunga gori Ila sikumbuki nilipokelea mguu gani. Ila yale mazingira yalikua ya nambali 11.

Wale wapinzani wetu muda huohuo wakarudi kushambulia gori letu wakafunga gori lingine.

Baadaye tena nikapewa mpira nikapiga chenga mpaka golini, hadi golikipa nikampiga chenga nikampasia ule mpira mshambuliaji mwenzangu akafunga. Baada ya hapo nikashituka toka usingizini nikaamka.

Sasa hii ndoto ina maana gani, siwezi kusema kwamba ina maana mimi ni mchezaji wa mpira, mpira mimi siupendi hata nusu. Ila ninahakika itakua na maana nyingine.

Karibuni.
 
Ni kama lipo jukumu utapewa kwa vile umeaminika ila nalo litakushinda.

Zingatia sala na dua.

Mamndenyi bana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom