Leo nimeamini Uswazi kuna Great Thinkers wa ukweli

Leo nimeamini Uswazi kuna Great Thinkers wa ukweli

Mkuu mfumo umeleta yote haya,utakuta watu wa serikali watakaomfikia kwanza ni TRA na kumuuliza haya unayoyafanya umelipa kodi?
sasa unajiuliza kodi mbona mkulima anayetumia ubunifu wake akalima haulizwi kodi?
nilitegemea cha kwanza kiwe kumuwezesha ili kipawa chake kiinuke afu ndo alipe kodi ya maana.

Watu kama hawa wapewe grace period kama tunavyowafanyia wawekezaji na wakiisha inuka basi
walipe kodi,badala ya kuwaua wangali tumbuni.

Mkuu kwenye mchango wako kuna ninayoyakubali na machache ninayopingana nayo. Kwenye swala la kodi hilo halina mjadala; inatubidi tutambue kuwa ni wajibu kwa kila mwananchi wa nchi hii kulipa kodi kwenye kila tunachokipata. Kama tusifofanya hivyo rushwa haitaisha na taifa halitaendelea.

Pia serikali ina wajibu wa kutengeneza sera ambazo zitatengeneza mazingira ambayo yatamwezesha siyo watu wenye vipaji tu hata wakulima waweze kujinufaisha kwenye wigo wa uwezo wao na wakati huohuo wawe wanalipa kodi.

Grace period huwa zinatengeneza loop holes ambazo zinaweza kuikosesha serikali mapato halali. Cha msingi ilitakiwa kuwe na kiwango ambacho ukipata kwa mwaka basi hutalipa kodi.
 
kwani dogo NICE kapelekwa wapi? Mimi nadhani huyu ni zaidi ya dogo nice!
 
Kuna suala la patent kwa mvumbuaji, akisahau patent hatakuwa na haki iwapo uvumbuzi wake ukidupliketiwa na kutumika kibiashara. Patent ni kama cheti cha umiliki wa uvumbuzi, sasa kama hana hiyo a/c ya 15k, soon itakuwa innovation idea ya Hun Cheng Ki.
 
semina na warsha, kutengeneza vipeperushi na tisheti,......yaani il mradi kuna 10%
Ni kweli mkuu wapo waliojenga na kununua magari ya kifahari kutokana na semina, warsha, tshirt a vipeperushi. Nane nane ni mtaji kwao.
 
As JF members, how do we help him develop his innovations?? We can.
 
Mkuu Transistor uko wapi hebu pitia huku basi. Hivi ina maana hukuna hata member wa JF au makampuni hapa JF wanaoweza kumchangia huyu dogo ili aweze kutoka?? Au kama kuna mchakato waweza wekwa wa kumchangia huyu dogo watu tukajitolea kidogo tulichonacho basi tumuwezeshe.
 
Kijana yuko safi sana, anaonyesha anafikiri kabla ya kufungua mdomo.

Na hili swali la "unataka serikali ikufanyie nyinyi?" linaniuzi sana, na kila kipindi kinachohusu jamii utakuta waandishi wanaliuliza. Wanajenga tamaduni mbaya sana kwenye vichwa vya watu.

Yaani wameshafanya Mtanzania hawezi kujikomboa/kujiwezesha mwenyewe kupitia uwezo wake binafsi ni mpaka aletewe msaada na serikali.


Think critically..unatumia muda gani kuchat?
Je Yale mambo unayochat hayachukui nafasi katika ubongo wako?
Kama ndiyo fikiria ni namna gani unapunguza muda wa kutuliza akili na kutafakari mambo katika scope iliyo nzuri zaidi.

Wakuu hayo ni maneno yenu au ni maneno ya uyo dogo genius? Daaah natamani nikione icho kipindi, Zembwela pliiiiiiiiz, hebu jiongeze kidogo tupia youtube bhanaa
 
Dogo kalamba one million ya mshindi wa wazo bomba ila nilibahatika kushika jina lake moja "OMBENI "
Hongera sana zembwela kama si wewe dogo asingepata hiyo pesa....
 
Juzi niliona kipindi ITV cha wajasiriamali vijana kinachifadhiliwa na Dk. Mengi. Nadhani ndio huyo kijana amajishindia zawadi ya kwanza 10,000,000.00. Kwa kweli anastahili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom