Jumanne Ngoma: Mgunduzi wa Tanzanite anayetaabika

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,191
674
Jumanne Ngoma: Mgunduzi wa tanzanite anayetaabika

images

- Pia amegundua madini ya jasi yanayotengeneza saruji
- Apigania kupata sehemu ya mauzo yake bila mafanikio
- Mkubwa serikalini alimpora sarafi yake Soko la Dunia
- Ahoji iweje Williamson alipwe kwa kugundua almasi?

UTAMBULISHO SIKU YA UVUMBUZI WA TANZANITE NA TANZANITE FOUNDER FOUNDATION (TAFFO)

OK+BLOG+3.jpg

Mvumbuzi wa madini ya Tanzanite, Jumanne Ngoma akiongea na waandishi wa habari Dar es Salaam, katika siku ya maadhimisho ya miaka 46 toka ugunduzi wa madini hayo, Mkoani Arusha eneo la Merelani. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taasis ya Tanzanite Founder Foundation (TAFFO), Asha Ngoma.

Leo katika historia ya Tanzania tar 23/9/1967 siku kama ya leo, miaka 46 iliyopita ndio siku ambayo yalivumbuliwa madini ya Zoisite ambayo kwa leo yanajulikana kama "TANZANITE" yanayo patikana nchini Tanzania pekee, duniani.

Mzee Jumanne Ngoma ndiye mvumbuzi wa madini haya, mwenye shahada ya Uvumbuzi alizotunukiwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maandhimisho ya sherehe za Mei Mosi Mbeya mwaka 1984.

Mzee Jumanne Mhero Ngoma (Mvumbuzi) wa madini haya ya Tanzanite, alizaliwa mwaka 1939 katika kijiji cha Marwa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.
Wazazi wake walikuwa wafugaji wa Ng'ombe na mbuzi hivyo waliishi maisha ya kuhamahama ili kupata malisho bora ya mifugo kama ilivyo hulka na tabia za wafugaji.

Wakati akiendelea na shule ya msingi, mwaka 1952 wazazi wake walihama kutoka Hedaru na kwenda kuishi Mererani. Mzee Jumanne Mhero Ngoma, aliweza kusafiri na wazazi wake hadi Mererani, akaendelea na masomo yake katika shule iliyokuwa ikiitwa Town School iliyopo Arusha mjini, ambako ilibidi akae na mjomba yake, Ruben Mkali aliyekuwa akiishi Arusha Mjini wakati huo.

Mwaka huo 1965, alifunga ndoa na Bi Fatma Mauya, na kupata watoto nane

Mzee Jumanne Ngoma alijiunga na kozi fupi ya madini iliyokuwa ikitolewa na Wizara ya Madini wakati huo. Baada ya kumaliza kozi ya madini katika ofisi ya madini Morogoro, Juni 1, 1966 alipata leseni ya madini baada ya kuhitimu mafunzo hayo.

Siku chache baada ya kumiliki leseni ya utafiti wa madini, Mzee Jumanne Mhero Ngoma alirejea nyumbani kwake Makanya.

Alipokuwa Makanya aliamua kuanza utafiti wake kijiji chake cha Makanya. Mzee Ngoma aliaza shughuli za utafiti wa madini, ndipo akagundua Madini ya Gypsum, na kuwa mtu wa kwanza aliyegundua Gypsum maeneo ya kijiji cha Makanya, sasa hivi eneo hilo linaitwa Chang'onko

Hivyo alipopata elimu hiyo ya madini aliamua kwenda Meralani, katika eneo la Lalouo kijiji cha Naisunyai kufanya utafiti wa yale mawe aliyoyaona wakati anachunga mifugo ya baba yake. Mwaka 1967 Januari, aliamua kuyapeleka mawe yale katika ofisi ya madini Moshi kwa uchunguzi. Alishauriwa na afisa wa madini kipindi hicho Bwana Bills, ofisi ya madini Moshi ikayapeleka kwenye maabara ya taifa Dodoma kwa uchunguzi zaidi.

Mnamo tarehe 23 Septemba 1967 maabara ya Dodoma ilithibitisha kuwa ni madini ya Zoisite ambayo kwa wakati huo hayakuwa na soko, lakini wakashauri huenda yakawa na soko siku zijazo.

Mnamo Mwaka 1984, Serikali ya Jamhuri ya muungano ilipotambua rasmi Mvumbuzi ya madini hayo na kuyapa jina la "TANZANITE" jina lililotokana na jina la nchi, yaani Tanzania na Zoisite na likapatikana jna hilo. Hapo alimtunukia cheti cha uvumbuzi katika sherehe ya siku ya wafanyakazi zilizofanyika mkoani Mbeya.

Kutokana na historia fupi hii ya uvumbuzi wa madini haya, leo tunaienzi siku hii ya leo na kuweka kumbukumbu sahihi na kuitambulisha asasi inayotokana na kuenzi jitihada za mvumbuzi huyu wa madini pekee yanayopatikana Tanzania pekee.

Asasi hii mpya ya kiraia itakua inajulikana kwa jina la TANZANITE FOUNDER FOUNDATION, kwa kifupi "TAFFO", ambayo yeye (mvumbuzi) ni mmoja wa waanzilishi wake.

TAFFO ni asasi isiyo ya kiserikali itakayojishughulisha na wachimbaji wadogo wadogo wa madini vijana, wanaofanya shughuli za madini yote yanayopatikana ndani ya nchi yetu ya Tanzania yakiwemo TANZANITE.

Malengo makubwa ya asasi hii ni:

1. Kuwawezesha vijana kupata utaalam (elimu) katika sekta ya madini.

2.Kuwawezesha kupata nyenzo za uchimbaji madini kutoka vyanzo mbali mbali ikiwemo Serikali, mashirika ya ndani na nje ya nchi, Asasi, mabenki na Mtu mmoja mmoja atakayeguswa na huduma za asasi hii.

3.Kuenzi na Kuhifadhi historia ya uvumbuzi wa madini ya TANZANITE kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Taasisi hiyo imeshukuru serikali kupitia wizara ya Nishati na Madini na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kwa kuwawezesha kapata usajili wa asasi hii.

========

Tanzanite ni madini ghali duniani yanayozalishwa nchini Tanzania pekee. Mwandishi Wetu MAYAGE S. MAYAGE amefanya mahojiano na mgunduzi wa madini hayo, Jumanne Ngoma kijijini kwake Makanya, Same, Kilimanjaro. Katika sehemu hii ya kwanza ya makala, pamoja na mambo mengine, Ngoma anaeleza jinsi alivyodhulumiwa haki yake na jitihada anazoendelea kufanya ili walau familia yake ifaidike na sehemu ya mauzo ya madini hayo.

"MAONI yangu ni kuwa utundu na uvumbuzi popote duniani, hulipwa na unatiliwa thamani sana katika nchi za kikabaila na kijamaa. Pendekezo langu, alipwe haki zake zote anazostahili."

Hilo ni dokezo la aliyekuwa Msaidizi wa Rais (Uchumi), Profesa Simon Mbilinyi, katika jalada lililokuwa na barua ya Jumanne Mhero Ngoma, ambayo alikuwa akiiomba Serikali imlipe haki yake ya kuwa mgunduzi wa madini ya tanzanite ambayo yametokea kuwa na thamani kubwa sana katika soko la dunia.

Ngoma, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 68, ndiye mgunduzi wa madini hayo ambayo kama Serikali ingekuwa makini tangu ayagundue mwaka 1967, yangekuwa yameiweka nchi hii katika ramani nyingine kabisa ya kiuchumi.

Hata hivyo, pamoja na dokezo hilo la Ikulu, la Oktoba 8, 1980, tena kutoka kwa Mshauri wa Rais katika Masuala ya Uchumi, Ngoma aliambulia hundi ya Sh 352,448.25 tu kutoka serikalini, ambayo ililipwa kutokana na ushauri huo.

Kana kwamba Serikali inatambua, na wala haina shaka juu ya ugunduzi wake huo, iliendelea kumuenzi Ngoma kwa kazi yake nzuri hiyo, kwa kuwa miongoni mwa watu waliotunukiwa tuzo ya ngao na cheti, pamoja na fedha taslimu Sh 50,000 katika sherehe za Mei Mosi, zilizofanyika kitaifa mkoani Mbeya mwaka 1984.

Kwa mujibu wa Ngoma, heshima hiyo aliyopewa na Serikali ilikuwa inaambatana na safari ya nje, ya kwenda kutembelea soko la dunia la tanzanite pamoja na kuzuru viwanda maarufu duniani vinavyotengeneza bidhaa zinazotokana na madini hayo ya tanzanite.

Hata hivyo, katika hali ya masikitiko makubwa, Ngoma anasema safari hiyo hakuwahi kuipata, na badala yake mjanja mmoja mkubwa tu katika Serikali hiyo ya Awamu ya Kwanza, tena anayemtaja kwa jina, ingawa kwa sasa ni marehemu, aliipora safari yake hiyo kimya kimya, na akampeleka mtoto wake wa kiume, ambaye bila aibu alisafiri kwa jina halisi la Jumanne Ngoma, kama mgunduzi wa tanzanite.

Ngoma aliugundua vipi ujanja wa mtu huyo? Anasimulia: "Baada ya kukabidhiwa ngao, cheti na kiasi hicho cha fedha (Sh 50,000) na Mzee Rashid Kawawa kule Mbeya, aliniambia nikishafika nyumbani nijiandae, Serikali ilikuwa imeniandalia safari (tour) ya kwenda kutembelea nchi mbalimbali zinazosifika kwa kuwa na migodi ya madini huko Ulaya, soko la dunia la tanzanite na viwanda vinavyotengeneza bidhaa zitokanazo na tanzanite.

"Nilifika nyumbani kwangu hapa Makanya (Same, Kilimanjaro), nikajiandaa nikisubiri barua ya kuitwa Dar es Salaam tayari kwa safari. "Siku moja nikiwa shambani, alikuja mtu mmoja akaacha barua hapa. Nilipotoka shamba watoto wakaniambia; baba kuna barua yako hapa&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];nikajua, safari yangu imeiva. Niliingia ndani nikatulia, na kisha nikaifungua. Humo nikakuta boarding ticket (kipande kinachomruhusu abiria kuingia ndani ya ndege) zilizokwishatumika, kadi ya chanjo ya homa ya manjano na vikorokoro vingine vinavyoelezea nchi na mahali mtu huyo alikotembelea, vyote vikiwa na jina langu."

Kwa hakika, ukimsikiliza Ngoma katika masimulizi yake juu ya vitimbi alivyofanyiwa na mamlaka zinazohusika na madini pamoja na Serikali kwa ujumla, kama ni mtu unayeguswa, unaweza ukatokwa machozi.

Katika muda wote wa mazungumzo haya yaliyofanyika nyumbani kwake, kijijini Makanya, Same, mkoani Kilimanjaro, Ngoma alikuwa ni mtu wa kulaani, kulalamika na kujiapiza.

Na hafichi kuonyesha ghadhabu yake kwa michezo yote michafu anayofanyiwa na wasiomtakia mema.

Anasema kwa mfano: "Kwa bahati nzuri sana, wote walionifanyia vitimbi na kunizibia riziki yangu, wamekufa vifo vibaya. Wengi wao hawapo duniani. Mungu ananilipa, anawaadhibu na naamini ataendelea kuwaadhibu wote wanaokalia haki yangu."

Hata baada ya kupata taarifa ya kufikiwa na Rai, ili pamoja na mambo mengine azungumzie ugunduzi wake huo, Ngoma hakuwa na hamu ya kufanya hivyo, akisema haoni faida yoyote ya yeye kuendelea kuzungumza na vyombo vya habari juu ya ugunduzi wake huo, kwa maelezo kwamba hafaidiki chochote, si tu kutoka kwenye vyombo vyenyewe vya habari, bali hata serikalini.

Kwa mfano, katika moja ya karatasi alizokuwa ameandika maelezo yake kwa mkono wake tayari kwa mahojiano haya, Ngoma anaandika:

"Karibu sana kijijini kwetu hapa Makanya, jisikie uko nyumbani. Mimi ndiye Jumanne Mhero Ngoma mgunduzi wa madini ya tanzanite. Nimehojiwa mara nyingi sana na magazeti mbalimbali nchini pamoja na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD), lakini sijaona faida ya mahojiano hayo.

"Nimehojiwa na waandishi wa habari wa BBC (Shirika la Utangazaji la Uingereza) mwaka jana, nikiwa Arusha, ambao ni Abdallah Majura na Tido Mhando, na mahojiano hayo yakarushwa hewani na BBC, London. Nawe leo unanifuata. Je, ni kwa faida ya kuuza magazeti yenu tu au na mimi nitafaidikaje juu ya mahojiano haya?"

Kwa ufupi, Ngoma alitaka kwanza ahakikishiwe ni kifuta jasho kiasi gani ambacho angelipwa kwa mahojiano haya. Na kwa kuwa mwandishi hakuwa amejiandaa kwa hilo, na kutokana na ukweli kwamba swali lenyewe hilo la malipo lilikuwa ni la kiutawala, ilibidi ifanyike juhudi kidogo kumshawishi ili kufanikisha mahojiano haya.

Kwa wanaokifahamu kijiji cha Makanya, wanatambua kwamba moja ya sifa za kijiji hicho ni kuwa na madini mengi ya jasi (gypsum), ambayo ni muhimu sana katika viwanda vya saruji nchini kwa uzalishaji wa saruji. Aidha, madini hayo hutumika katika utengenezaji wa chaki na POP zinazotumika hospitalini.

Mgunduzi wa madini hayo ya jasi kijijini hapo si mwingine, bali ni Ngoma. Huyo ndiye alikuwa msambazaji (supplier) wa kwanza wa madini hayo wakati Kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill kilipoanza uzalishaji wa bidhaa hiyo miaka ya katikati ya sitini.

Kutokana na ugunduzi wake huo wa jasi, madini ambayo ndiyo tegemeo la kiuchumi kwa wakazi na pato la Kijiji cha Makanya, uongozi wa kijiji hicho, katika kumuenzi Ngoma, umemsamehe kushiriki katika shughuli yoyote ya uchangiaji wa miradi ya maendeleo kama vile shule, zahanati na/au miradi ya maji.

Anasema: "Nashukuru sana, uongozi wa kijiji na wanakijiji wenzangu wanatambua mchango wangu katika maendeleo ya hapa. Katika kuenzi ugunduzi wangu wa madini ya jasi, wamenisamehe nisishiriki aina yoyote ya &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];msaragambo' (harambee ya kuchangia maendeleo)."

Hata hivyo, pamoja na Ngoma kuenziwa na wanakijiji wenzake kuhusu ugunduzi wake huo wa madini ya jasi, madini ambayo kwa kiasi kikubwa yamechangia katika kukua kwa uchumi wa wanakijiji cha Makanya, ana malalamiko mengi kwa watawala wa nchi hii kwa kutotaka afaidike na ugunduzi wake madini ya tanzanite.

Anasema juhudi zake zote za kutaka Serikali imsaidie kumpatia Hati ya Ulindaji wa Kazi za Kigunduzi (Intellectual Property Protective &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; IPP), ambayo ingemsaidia kutambuliwa kimataifa na hivyo kufaidika na ugunduzi wake huo kama ambavyo mgunduzi wa almasi ya Mwadui, Williamson anavyofaidika, zimegonga mwamba.

Katika kilio hicho, anasema: "Kama familia ya Williamson, mgunduzi wa almasi Mwadui, inavyofaidika na ugunduzi huo, nami naomba Serikali isimamie kwa kuwapo maandishi yanayosema kwamba nitakuwa napata asilimia fulani ya mapato yanayotokana na mauzo yote ya tanzanite kwa maisha yangu yote na kizazi changu hadi madini hayo yatakapokwisha.

"Msajili wa Kulinda Haki za Ugunduzi, aliniandikia barua akisema ugunduzi tu wa madini katika ardhi, hauwezi kupewa Hati ya Kulinda Kazi za Ugunduzi. Sawa; lakini mbona Williamson yeye alipewa? Yeye aligundua almasi ya Mwadui angani, kwenye mwezi au baharini? Si ni katika ardhi hii hii ya Tanzania, ambamo nami nimegundua tanzanite?"

Ni katika mkanganyiko huo, Ngoma alitumia fursa hii kuiomba rasmi Kamati ya Madini ya Rais, chini ya Jaji Mark Bomani, kabla ya kuhitimisha kazi yake hiyo, imwite mbele ya kamati hiyo ili aweze kuwasilisha maoni yake juu ya nini kifanyike katika sekta ya madini.

Lakini pia, Ngoma haachi kulaani baadhi ya kauli za viongozi waandamizi serikalini ambao wamekuwa wakimwekea &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];ukuta' kila anapofuatilia haki zake, wakisema ni mtu asiyetosheka hata akipewa fedha inayolingana na Mlima Kilimanjaro.

"Hivi Sh 352,448.25, nilizopewa na Serikali ndizo ninazosimangiwa kwamba sitosheki hata nikipewa fedha zinazolingana na Mlima Kilimanjaro? Kama ni kutosheka, kwa nini viongozi hao hao wao hawataki kutosheka na madaraka yao?

"Mbona wamestaafu, lakini juzi tumewaona wakichukua fomu za kuomba uongozi wa juu katika chama?" anahoji Ngoma bila kutaja jina la kiongozi wa ngazi ya juu katika Serikali ya Awamu ya Tatu, ambaye alipata kumwambia kwa ukali kwamba hatosheki hata akipewa fedha zinazolingana na Mlima Kilimanjaro.

Ngoma aliyagundua vipi madini ya zoisite, ambayo baadaye yalikuja kubadilishwa jina na kuitwa tanzanite kutokana na ushauri wa kampuni moja ya Kimarekani, iliyokuwa ikifanyia biashara yake mjini Arusha, ikijulikana kwa jina la Tiffany kwa Serikali?

Je; unayajua maisha anayoishi mgunduzi huyo wa tanzanite, na ndoto zake alizonazo katika umri wake wa sasa, juu ya ugunduzi mwingine wa madini, yakiwamo hayo ya tanzanite?

Unafahamu kama Ngoma ana kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam dhidi ya kampuni ya kigeni ya AFGEM, kwa sasa Tanzanite One, akitaka kampuni hiyo imlipe fidia ya Sh bilioni mbili taslimu kwa madai kwamba kampuni hiyo, kwa makusudi tu, imepotosha katika jarida lao linalochapishwa nchini Afrika Kusini, kwa kuandika kwamba mgunduzi wa tanzanite ni mtu mmoja anayetajwa kwa jina la Ali juu ya watu, na si yeye Jumanne Ngoma?
***************************

KILA mwaka, madini aina ya Tanzanite huiingizia Tanzania kiasi cha dola milioni 20 (zaidi ya Sh bilioni 30). Duniani kote, madini hayo hayo huingiza wastani wa dola milioni 500 (zaidi ya Sh bilioni 800).

Wakati mabilioni yote hayo yakiingia mfukoni mwa serikali na wafanyabiashara, mgunduzi wa madini hayo, Jumanne Mhero Ngoma (74), anaishi kwa kutegemea ruzuku za watoto.

Mapato yake kwa mwaka ni shilingi za Tanzania sifuri!
Nilikutana na Mzee Ngoma siku chache zilizopita jijini Dar es Salaam katika ofisi ya mmoja wa wanawe. Pamoja na masahibu na mikasa mbalimbali iliyomkumba katika maisha yake, bado aliweza kunipokea kwa bashasha na tabasamu.

Amefanya mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari na pengine ameanza kuchoka sasa. Mvi kichwani kwake na kwenye eneo la ndevu ni ishara kwamba umri unaanza kumtupa Mzee Ngoma.

Nimekaa namtazama. Huyu ndiye mtu aliyegundua madini ya Tanzanite. Alipaswa kuwa utambulisho wa Watanzania. Katika nchi nyingine zinazothamini watu wake, huyu alitakiwa kufahamika na watu wote waliomaliza elimu ya msingi.

Kama ambavyo watoto wote wa Kimarekani wanavyomfahamu Thomas Edison (mbunifu mashuhuri na mfanyabiashara wa karne kadhaa zilizopita) . Lakini mbele ya macho yangu, alikaa mzee mmoja ambaye kama ningekutana naye kwenye daladala (na ndiyo usafiri wake mkuu), nisingemtazama mara mbili.

Namuuliza swali moja la msingi kwamba ilikuwaje yeye aliyagundua madini ambayo wakoloni (wazungu) walishindwa kuyabaini kwa muda wote waliokaa hapa nchini.

"Nakumbuka kila kitu kuhusu mara yangu ya kwanza kuona madini hayo. Mara ya kwanza kuyagundua madini haya nilikuwa mdogo sana. Nilikuwa na umri wa chini ya miaka 20 na nilikuwa porini nikichunga mifugo.

"Nilikuwa kwenye msitu ambao Wamasai walikuwa wameupa jina la Lalouo. Eneo ambako niliyaona lilikuwa linafahamika kwa jina la Naisunyai ambako kwa kawaida Wamasai walikuwa wakilitumia kunywesha mifugo yao.
"Siku hiyo niliona vitu vinavyowaka. Nikawa nashangaa vitakuwa ni vitu gani. Awali nilidhani pengine ni nyoka au wanyama wa hatari. Nikasogea nikiwa na upinde na mshale wangu tayari kwa lolote.

"Nilipogusa na mti niliokuwa nimeushika, nikashangaa mawe yanayong'aa yakitoka ardhini. Vipande vidogo vidogo vyenye rangi ya bluu. Kwa kweli nilivipenda sana.

"Nilishangaa sana lakini ghafla nikakumbuka kuwa nilikuwa nachunga mifugo. Kumbe ng'ombe na mbuzi niliokuwa nawachunga walikuwa wamekimbia tayari. Nikaacha shughuli hiyo na kwenda kuwafuata.

"Kwa bahati nzuri, nilifuatilia njia walizopita hadi nikawapata wote. Lakini ilikuwa kazi ngumu maana ule ulikuwa msitu mkubwa. Nikarudi nyumbani nikiwa na mifugo ile na nikawa nimesahau kabisa habari za madini yale kwa muda ule," anasema.

Mtoto wa Ngoma aitwaye Asha aliyekuwa mwenyeji wetu kwenye ofisi ile ananiuliza kama naweza kutumia kinywaji chochote. Namwomba samahani kwa kuwatia hasara maana nikaagiza vinywaji viwili badala ya kimoja. Maji na soda. Kwenye dunia hii ya kisukari, kunywa soda pekee bila kuchanganya na maji kunaleta hatari ya kuongeza sukari mwilini.

Mzee Ngoma yeye anaomba maji tu. Tunasubiri kidogo. Tunapiga mafunda mawili matatu na kisha tunaendelea na mazungumzo yetu.

Hata hivyo, mwaka 1966 ilitokea bahati iliyobadilisha maisha yangu. Mwanzoni mwa mwaka huo, serikali ilitangaza kuwepo kwa mafunzo kuhusu utafiti wa madini yaliyopangwa kufanyika mkoani Morogoro.

"Mimi wakati huo nilikuwa nafanya biashara zangu tu lakini nilikuwa mpenzi sana wa masuala ya madini na ndiyo nilipoyaona madini yale ya Tanzanite kwa mara ya kwanza nilishikwa na hamu ya kutaka kuyajua.

"Ulitakiwa kujilipia mwenyewe nauli na gharama nyingine halafu serikali inakulipia mafunzo hayo kwa muda wa wiki tatu. Nikazungumza na mke wangu kuhusu hilo na akaniruhusu niende kwenye mafunzo.

"Nilikwenda Morogoro na hatimaye nikafaulu kwenye mafunzo hayo. Ilipofika tarehe sita, mwezi wa sita mwaka 1966, nikapewa cheti cha utafiti ambacho ninacho hadi leo. Pamoja na mambo mengine, cheti hicho kilikuwa kinakuwezesha kufahamu madini na sifa zake mbalimbali," anasema.

Ni mafunzo hayo ambayo baada ya kuyamaliza yalimfanya Ngoma aweze kugundua madini hayo ya Tanzanite.

Lakini kabla ya madini hayo, mzee huyu kwanza aligundua madini aina ya Gypsum ambayo sasa yanatumika katika nyumba nyingi za Watanzania wenye kipato kuanzia cha kati hadi cha juu.

Aliyagundua madini hayo katika eneo la Chankoko, Makanya mkoani Kilimanjaro.
"Wakati nikigundua madini hayo, hayakuwa na kazi sana. Watu wengi hawakujua kazi yake. Kwa bahati nzuri, katika wakati huohuo, kukawa na kiwanda cha saruji cha WAZO ambacho kilitaka kuanza kufanya shughuli zake na gypsum ilikuwa ni malighafi nzuri sana.

"Kuna bwana mmoja aitwaye Petro Gerson Kizigha akanikutanisha na wazungu waliokuwa wakitaka kuanzisha kampuni hiyo na tayari wakiwa na taarifa za gypsum niliyoigundua.

"Nakumbuka majina ya wazungu hao yalikuwa ni Florench, Carter na Habel. Walikuja hadi Makanya kwa ndege binafsi na walishukia katika shamba la katani la bwana mmoja aliyekuwa akiitwa Hassan.

"Walipoona gypsum ile wakaipenda sana. Wakaagiza mara moja mzigo wa tani 36 ambao tuliupakia kwenye mabehewa. Kuna barabara kutoka Chankoko hadi stesheni ya reli ya Makanya yenye urefu wa kilomita 10 ilijengwa ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa hiyo.

"Mimi ndiye niliyepewa jukumu la ujenzi wa barabara hiyo. Nilipewa na wazungu wale kiasi cha Sh 8,000 kwa ajili hiyo. Kwa wakati huo, hiyo ni hela nyingi sana. Wajenzi walikuwa wakilipwa shilingi nne kwa siku na zilikuwa nyingi kiasi kwamba watu walikuja kuomba kazi kwa wingi hadi wengine nikawakataa, anasema.

Pamoja na mafanikio hayo katika biashara ya gypsum, kuna kitu kimoja kilikuwa kinamsumbua Ngoma kichwani kwake. Yale madini aliyoyaacha kule Umasaini, Marerani yalikuwa ni madini gani?

"Ndipo siku moja nikawachukua ndugu zangu na kuwaomba wanisindikize kwenda kwenye ule msitu wa Lalouo ili nikayachunguze tena yale madini. Niliomba kusindikizwa kwa sababu ule msitu ni mkubwa na nilitaka pia nipate watu wa kunisaidia kubeba.
"Nakumbuka tulichimba karibu kilo sita za madini hayo. Kuna jiwe moja lilikuwa na ukubwa wa takribani gramu 55 hivi. Jiwe kubwa tu. Ndilo lililokuwa kubwa zaidi.

"Nikalipeleka Moshi kwenye Ofisi ya Mkaguzi wa Madini aliyekuwa akiitwa Bills wakati huo. Mzungu huyo. Akayatazama na akasema hajawahi kuona kitu kama kile. Akahisi yanaweza kuwa Blue Tomaline, lakini tukakubaliana kuwa si yenyewe.
"Mimi nikamuuliza sasa mwenzangu unadhani haya ni madini gani? Unajua wazungu ni watu wakweli kidogo. Wana matatizo yao lakini hawapendi kusema uongo. Akasema kwa kweli siyajui. Inabidi tuyapeleke kwenye maabara ya serikali iliyokuwa iko Dodoma.
"Nikampa sampo yote niliyokuwa nayo lakini lile jiwe kubwa zaidi nikabaki nalo. Alipoliona, mke wa bwana Bills akawa amelipenda sana. Akaniomba abaki nalo.

"Nikakataa. Nikamwambia kama nikikupa, nitakuwa nakupa nini? Maana mumeo ambaye ndiye mtaalamu wa mambo haya ameshindwa kuyajua. Siwezi kukupa na nitabaki na hili kama kumbukumbu yangu.

"Ilipofika Septemba 23 mwaka 1967, ndipo nikapokea barua rasmi kutoka maabara ya Dodoma. Vipimo vikaonyesha madini yale yanafahamika kwa jina la Zoisite. Ndiyo maana tunasema madini hayo yaligunduliwa rasmi mwaka huo wa 1967 kwa sababu ndipo cheti kile cha maabara kilipotoka," anasema.

Katika simulizi kuhusu gunduzi mbalimbali za madini hapa nchini, zipo zinazoeleza namna wananchi wa Shinyanga walivyokuwa wakicheza bao kwa kutumia almasi kwa sababu hawakujua thamani yake.

Hali iko hivyo kwa Mzee Ngoma ambaye alikuwa akilitumia jiwe hilo la gramu 55 kwa ajili ya kuzuia karatasi zake zisipepee kutoka mezani kwake. Lilikuwa jiwe la kawaida kabisa ndani ya nyumba yake.

Nimeangalia bei ya sasa ya Tanzanite ili upate picha ya nini mzee huyu alikuwa nacho ndani kwake. Kwa sasa, bei ya madini hayo katika soko la dunia inacheza kati ya dola 500 hadi 700 kwa karati moja.
Zipo taarifa kwamba zipo sehemu duniani ambako watu wanauziwa hadi dola 1000 kwa karati moja. Tuseme wastani ni dola 600 (sh 800,000) kwa karati moja.

Karati moja ni sawa na gramu 0.2. Gramu 55 maana yake ni karati 275. Kama bei ya karati moja ni Sh 800,000, bei ya karati 275 ni sawa na takribani Sh milioni 220.
Mzee Ngoma alikuwa anatumia Sh milioni 220 kuzuia karatasi na magazeti yasipeperuke kutoka mezani kwake ! Mzee huyu hakujua kitu wakati huo.
Jiwe hilo kipenzi la mgunduzi huyu likaja kumpotea katika mazingira ya kutatanisha. Simulizi yake, ilinifanya niombe mahojiano haya yapumzike kidogo ili niweze kuvuta pumzi.

"Nilikuwa na marafiki wawili wenye asili ya kihindi waliokuwa wakiishi Handeni mkoani Tanga. Mmoja akiitwa Habib Esack Ismail na mwingine akijulikana kwa jina la Nuru Skanda. Walikuja siku moja nyumbani kwangu na wakaliona lile jiwe.
"Wakaniomba waende nalo kwao (Handeni) ili wakawaonyeshe wazazi wao wajue la kufanya. Wakati huo, Zoisite ama Tanzanite kama inavyofahamika sasa, haikuwa maarufu sana na matumizi yake hayakuwa yakijulikana.

"Walisema watalirudisha baada ya siku tatu. Nikawapa na wakaondoka nalo. Hawakurudi baada ya siku tatu na sijawaona tena tangu wakati huo. Siku moja nilikutana na aliyekuja kuwa Kamishina wa Madini hapa nchini aliyejulikana kwa jina la Luwena na akaniambia lile jiwe liko Ujerumani na waliuziwa kwa Sh 6000 kwenye miaka hiyo.

"Hizo ni hela nyingi sana. Ina maana akina Habib waliliuza na wakaondoka zao. Lile jiwe linaniuma sana maana kama ningebaki nalo pengine lingeweza kunipa fedha nyingi," anasema Ngoma.

Machungu ya Mzee huyu hayakuishia hapo. Kuna unyama mwingine mkubwa zaidi ambao alifanyiwa.

Baada ya kuibiwa jiwe lake hilo, akili ya Ngoma ilifanya kazi haraka na akaamua kwenda kupata leseni ya umiliki wa eneo ambako aliyapata madini yale.

Akapewa viwanja nane kwenye eneo lile la Lalouo ambako alilipia kiasi cha Sh 15 kwa kila kimoja. Akaweka alama zote muhimu na kuamini kwamba lile ni eneo lake halali kisheria na mara wakati utakapofika, ataanza kuchimba madini hayo.

"Siku moja mwezi Februari mwaka 1968, nikaenda kutembelea kwenye eneo lile. Nikamkuta kijana mmoja anaitwa Daudi Mayaya akiwa anachimba madini hayo kwenye eneo langu. Alikuwa ameyajaza kwenye ndoo.

"Nikamwambia kwanini amechimba madini hayo kwenye eneo langu? Akanijibu kwamba lile si eneo langu bali ni la mtu mmoja aiwaye De Souza (Huyu nitamweleza zaidi baadaye). Nikamwonyesha alama zangu zote nilizoweka pamoja na nyaraka nilizokuwa nazo.

"Nilipoenda kushitaki Polisi kuhusu huyu mtu anayeitwa De Souza, nikaambiwa ataitwa na atafika Jumatatu. Bila ya taarifa, kumbe huyo bwana akaja Jumamosi na akazungumza na polisi mapema.

"Mkuu wa Polisi kwenye eneo letu alikuwa akifahamika kwa jina la Herbert Kitenge. Huyu bwana akaniita Polisi na akaniambia ameamua kumpa De Souza vitalu (viwanja) vinne kati ya nane nilivyokuwa navimiliki.

"Sasa mimi nikabaki nimeshangaa, inakuaje mtu anapewa vitalu vyangu. Lakini afande Kitenge akasema ama nikubali hiyo dili au nitanyang'anywa vyote. Nikakasirika sana na nikasusa kabisa. Sikurudi tena kule kwenye machimbo. Nikaenda kufanya biashara zangu," anasema kwa huzuni.

Mzee Ngoma anamtaja De Souza mara nyingi katika maelezo yake. Manuel De Souza, mzaliwa wa Goa nchini India alikuja nchini Tanganyika mnamo mwaka 1933 akiwa na umri wa miaka 20 tu na tayari akiwa fundi cherehani mzuri.

Taarifa katika mitandao mbalimbali duniani inamtaja yeye kama mvumbuzi wa Tanzanite. Mtandao wa Ilios Jewellers unadai kwamba Julai mwaka 1967, kundi la Wamasai, lilimpeleka Mhindi huyo kwenye eneo ambako aligundua madini hayo.
Kwenye mtandao unaoheshimika zaidi duniani wa Wikipedia unamtaja fundi cherehani, Emmanuel Merishiek Mollel kama mgunduzi wa madini hayo.

Katika maelezo yake, mtandao huo unadai kwamba ni Mollel ndiye aliyempa De Souza madini hayo na yeye akayapeleka kwa wataalamu ambao waliyabaini kwamba ni Tanzanite.

Hata historia inapindishwa ili Mzee Ngoma akose hadhi na heshima anayostahili !
Kabla ya kuitwa Tanzanite, madini haya yalikuwa yakifahamika kwa jina la Zoisite. Jina hilo, kwa mujibu wa maelezo ya nyaraka mbalimbali, lilitokana na raia wa Austria, Siegmund Zois, ambaye alikuwa akifadhili safari mbalimbali za watu waliokuwa wakitafuta madini mbalimbali.

Kwa Kijerumani, neno Zoisite linafanana kimatamshi na neno la Kiingereza Suicide. Kampuni iliyokuwa ikifanya biashara ya Tanzanite ya Tiffany& Co. ndiyo ikaamua kubadili jina hilo na kuyaita madini hayo Tanzanite ili liwe na mvuto.

Hakukuwa hata na mmoja aliyeona yanafaa kuitwa Ngomanite au Ngomasite !
Mwaka 1984, serikali iliamka kutoka usingizini na kumtaja Mzee Ngoma kama mvumbuzi wa madini hayo.

Kama zawadi yake kwa uvumbuzi huo wa kihistoria, serikali ilimpa mzee huyo Ngao, cheti cha kumtangaza kama mvumbuzi na fedha taslim Sh elfu 50,000.
Kwa mujibu wa Wikipedia, katika kipindi cha kati ya mwaka 1967 hadi mwaka 1972 wakati serikali ilipoamua kutaifisha shughuli za uchimbaji wa Tanzanite, kiasi cha karati milioni mbili zilikuwa tayari zimechimbwa kutoka Mirerani.

Kwa bei ya sasa ya karati moja, maana yake ni kwamba kwa miaka hiyo mitano pekee, De Souza, washirika wake kama vile Ally Juyawandu na askari jeshi mmoja aliyekuwa na asili ya Ugiriki aliyefahamika kwa jina moja tu la Papanichalou, walifanikisha biashara yenye thamani ya takribani Sh trilioni 1.6 kwa thamani ya sasa !

Watoto wa De Souza aliyefariki dunia mwaka 1969 akiwa na umri wa miaka 56 kwa ajali ya gari, wametapakaa katika nchi mbalimbali kama vile Denmark, Malta na Uingereza, pengine wakila faida ya &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];ugunduzi' wa baba yao.

Kwa upande mwingine, Mzee Ngoma amejibanza katika ofisi ndogo ya mwanaye Asha katikati ya jiji. Fedha pekee ambayo ameitengeneza kutokana na kuipa Tanzania sifa na utajiri huu wa kipekee ni Sh elfu 50,000 zile alizopewa na Hayati Rashid Mfaume Kawawa !

Namuuliza shujaa huyu wa taifa anataka nini kutoka kwa serikali; "Sihitaji mambo makubwa sana. Ninachohitaji ni kuishi maisha yanayofanana na Tanzanite. Nataka mtu akiniona mimi aone Tanzanite," anasema.

Ni ombi ambalo linanisisimua. Watanzania wanapaswa kuwafahamu watu kama akina Ngoma. Serikali inapaswa kuwaenzi watu kama akina Mzee Ngoma.

Hawa watachochea watu wawe wagunduzi zaidi. Simulizi zao zitafanya watu wajenge akili ya kuhoji kila wanachokiona. Nani ajuaye, pengine kuna &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Tanzanite' nyingine katika maeneo mbalimbali hapa nchini lakini hazijulikani kwa vile hakuna akina Ngoma?

Nani atataka kuwa mgunduzi wa vitu vya thamani iwapo wagunduzi waliopo tunapanda nao daladala, tunashinda nao njaa na hawathaminiki?
Serikali imfanye Mzee Ngoma afanane na faida ambayo Tanzanite imeiletea nchi yetu.

Chanzo: Gazeti la RAI

-----------
Face to face with discoverer of Tanzanite

Imagine a gemstone so nice that it radiates a hundred rays of velvet blue and sensual violet from every facet. A gemstone so precious, it is found only in one place on earth. So extraordinarily rare, that in a single generation, there will be no more.

Tanzanite stones are used in all forms of jewelery and in some cases it has been chosen to replace diamond earrings, rings and necklaces. But who had actually discovered this precious stone is not a subject of human speculation.

My first encounter with the man who first spotted these gemstones, unfortunately rekindles sad memories of biting poverty among majority Tanzanians, whose country is endowed with massive natural wealth.

Using my own car; it took me almost six hours to reach Makanya Township in Kilimanjaro region, over 600 km from Dar, where Jumanne Mhero Ngoma- the man who first spotted Tanzanite lives.

Contrary to my imaginations, Mr. Ngoma lives an average village life with his family. He has nothing to boast off. Even his neighbours are wondering why this man remains poor despite his discovery of a multi million dollars business.

Ever since Mr. Ngoma stumbled upon sparkling blue crystals in the shadows of Mount Kilimanjaro; tanzanite has become one of the world’s most sought-after gemstones. No wonder. As anyone who has ever laid eyes on this gemstone can testify, and yet, when it was first discovered, Ngoma could hardly give it away:

-I found the tanzanite in Merelani, Arusha, in the area called Kiteto at the beginning of January 1967. I was on my way to visit some of my relatives who live in Kiteto, when walking through the bush I saw some crystals of a blue mineral lying on the ground. There were very nice… They were blue, some were transparent… In a few hours I collected about 5kg — they were all very lovely blue crystals.

-A friend told me to get on the bus and go to Nairobi, Kenya… where there was a much bigger gemstone market than in Arusha. So I borrowed some money for the journey and went to an overseas company who deals in precious stones… and I let them see the 5kg of tanzanite.

They didn’t even know what the mineral was. They told me, though, that as soon as they knew, they would let me know. I left them with the 5kg of tanzanite in exchange for a return ticket home, worth $5, four decades have passed and I’m still waiting for their answer! But I kept some samples for myself, he recounts.

Following this discovery, tanzanite quickly became one of the world’s most popular gemstones. Some credit is due to some promoters, who introduced it to market with a lovely name that pays tribute to the beauty of the land of its birth.

The name tanzanite was adopted by the then President of Tanzania Julius Nyerere who recommended that the precious stone be given a national status.
Tanzania government, through the ministry of Tourism and Natural Resources recognized Mr. Ngoma and awarded him some money in 1979, thus no other person should be linked with the rare discovery.

The commission for science and technology had also honored him in 1984 and awarded him a certificate of citation, a shield and a token 50,000 shillings.
Despite its discovery; Tanzanite has not been without controversy. For years now Mr. Ngoma has been involved in a fierce legal battle against AFGEM-the biggest Tanzanite mining company from South Africa for allegedly promoting another person as the discoverer of the stone.

Mr. Ngoma is confident that, whoever refutes that he was the one who first spotted tanzanite is dreaming since the government had already recognized him with tangible proof.

It’s a pity that some individuals and foreign companies involved in tanzanite business continue to embarrass him by denying his discovery.

On its discovery, it was enthusiastically celebrated by the specialists as the gemstone of the 20th century'. They held their breath in excitement as they caught sight of the first deep-blue crystals which had been found in Merelani hills.

The precious crystals grew in deposits on the inside of unusual elevations. It is interesting that for a long time they were hidden from the eye of man, until one day a passing pastoralist Mr. Ngoma noticed some sparkling crystals abundantly lying on the ground.

======

UPDATES: 06 April 2018

Hatimaye rais Magufuli atambua mchango wake.

Rais anasema ameambiwa tangia madini hayo yagunduliwe na mzee Jumanne Ngoma mwaka 1967, na barua ya Nyerere na barua ya Mjiolojia zilizondikwa kuonyesha kutambua ugunduzi huo ameziona

Hii inaonyesha Tanzanite haikugunduliwa na mtu kutoka nje, ila mtanzania huyo anaishi maisha magumu na ameparalaizi

Rais anasema naye amaegundua mambo kwenye kemia pia ila hajatambuliwa

AAnataka mzee huyo apande kama anaweza kuja ili atambuliwe kuwa yeye ndio mgunduzi wa madini ya Tanzanite, anapelekwa kwenye meza kuu

Rais Magufuli anasema serikali itamoa mzee huyo shilingi milioni 100 akazitumie katika matibabu yake na shughuli nyingine

Rais anatoa witonkwa Watanzania kuwathamini wanaofanya mazuri kwa nchi, wapo watu wamekuwa mabilionea kutokana na madini ya Tanzanite ambao hata sio watanzania lakini mzee amebaki hivyo hivyo.

Habari zaidi, soma=>LIVE - Yanayojiri Manyara: Rais Magufuli anazindua Ukuta wa Mirerani uliojengwa na JKT
 
Hi inasikitisha sana. Lakini ndiyo TZ yetu ilivyo. Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita Mtunzi wa mziki wa Malaika alikuwa akitaabika vivyo hivyo katika kufuatilia haki zake, na aliiomba serikali imsaidie ile yule Fadhili Williams( Mkenya) asile jasho lake.

Guess what, hakuna hata mtu aliyekuwa akimwangalia mzee wa watu. Alikuwa na ushahidi wote, na hata huyo malaika mwenyewe (aliyemtungia huo wimbo) alimtaja na kuonesha aishipo kama sikosei Arusha (wakati huo).

Na ilisikitisha sana kwani Fadhili Williams ailikuwa analamba Millioni 2 na nusu kwa mwaka ati royalities!!!, wakati mzee wa watu akiishi nyumba ya mbavu za mbwa.
 
Face to face with discoverer of Tanzanite

Imagine a gemstone so nice that it radiates a hundred rays of velvet blue and sensual violet from every facet. A gemstone so precious, it is found only in one place on earth. So extraordinarily rare, that in a single generation, there will be no more.

Tanzanite stones are used in all forms of jewelery and in some cases it has been chosen to replace diamond earrings, rings and necklaces. But who had actually discovered this precious stone is not a subject of human speculation.

My first encounter with the man who first spotted these gemstones, unfortunately rekindles sad memories of biting poverty among majority Tanzanians, whose country is endowed with massive natural wealth.

Using my own car; it took me almost six hours to reach Makanya Township in Kilimanjaro region, over 600 km from Dar, where Jumanne Mhero Ngoma- the man who first spotted Tanzanite lives.

Contrary to my imaginations, Mr. Ngoma lives an average village life with his family. He has nothing to boast off. Even his neighbours are wondering why this man remains poor despite his discovery of a multi million dollars business.

Ever since Mr. Ngoma stumbled upon sparkling blue crystals in the shadows of Mount Kilimanjaro; tanzanite has become one of the world’s most sought-after gemstones. No wonder. As anyone who has ever laid eyes on this gemstone can testify, and yet, when it was first discovered, Ngoma could hardly give it away:

-I found the tanzanite in Merelani, Arusha, in the area called Kiteto at the beginning of January 1967. I was on my way to visit some of my relatives who live in Kiteto, when walking through the bush I saw some crystals of a blue mineral lying on the ground. There were very nice… They were blue, some were transparent… In a few hours I collected about 5kg — they were all very lovely blue crystals.

-A friend told me to get on the bus and go to Nairobi, Kenya… where there was a much bigger gemstone market than in Arusha. So I borrowed some money for the journey and went to an overseas company who deals in precious stones… and I let them see the 5kg of tanzanite.

They didn’t even know what the mineral was. They told me, though, that as soon as they knew, they would let me know. I left them with the 5kg of tanzanite in exchange for a return ticket home, worth $5, four decades have passed and I’m still waiting for their answer! But I kept some samples for myself, he recounts.

Following this discovery, tanzanite quickly became one of the world’s most popular gemstones. Some credit is due to some promoters, who introduced it to market with a lovely name that pays tribute to the beauty of the land of its birth.

The name tanzanite was adopted by the then President of Tanzania Julius Nyerere who recommended that the precious stone be given a national status.
Tanzania government, through the ministry of Tourism and Natural Resources recognized Mr. Ngoma and awarded him some money in 1979, thus no other person should be linked with the rare discovery.

The commission for science and technology had also honored him in 1984 and awarded him a certificate of citation, a shield and a token 50,000 shillings.
Despite its discovery; Tanzanite has not been without controversy. For years now Mr. Ngoma has been involved in a fierce legal battle against AFGEM-the biggest Tanzanite mining company from South Africa for allegedly promoting another person as the discoverer of the stone.

Mr. Ngoma is confident that, whoever refutes that he was the one who first spotted tanzanite is dreaming since the government had already recognized him with tangible proof.

It’s a pity that some individuals and foreign companies involved in tanzanite business continue to embarrass him by denying his discovery.

On its discovery, it was enthusiastically celebrated by the specialists as the gemstone of the 20th century'. They held their breath in excitement as they caught sight of the first deep-blue crystals which had been found in Merelani hills.

The precious crystals grew in deposits on the inside of unusual elevations. It is interesting that for a long time they were hidden from the eye of man, until one day a passing pastoralist Mr. Ngoma noticed some sparkling crystals abundantly lying on the ground.
 
nenda pale sandton - johannesburg inavyotangazwa unaweza dhani south africa ndo wao wanao produce hiyo tanzanite, maana inatangazwa mno,na si sandton tu all over SA, maana hata rangi za magari wanayotengeneza utasikia kuna tanzanite blue/green etc ,kazi tunayo........
 
it was a great discovery, I wonder who actually benefit from our natural wealth? we all know that its not even our leaders "mafisadi", people from overseas are the one benefiting from these stones, i wonder if there is a day we are going to stand up and fight for our wealth.
 
even imf/world bank know that Tanzanian are nt getting any benefit despite the high hit record price in the world market
 
318_ngoma.jpg

KILA mwaka, madini aina ya Tanzanite huiingizia Tanzania kiasi cha dola milioni 20 (zaidi ya Sh bilioni 30). Duniani kote, madini hayo hayo huingiza wastani wa dola milioni 500 (zaidi ya Sh bilioni 800).

Wakati mabilioni yote hayo yakiingia mfukoni mwa serikali na wafanyabiashara, mgunduzi wa madini hayo, Jumanne Mhero Ngoma (74), anaishi kwa kutegemea ruzuku za watoto. Mapato yake kwa mwaka ni shilingi za Tanzania sifuri!

Nilikutana na Mzee Ngoma siku chache zilizopita jijini Dar es Salaam katika ofisi ya mmoja wa wanawe. Pamoja na masahibu na mikasa mbalimbali iliyomkumba katika maisha yake, bado aliweza kunipokea kwa bashasha na tabasamu.

Amefanya mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari na pengine ameanza kuchoka sasa. Mvi kichwani kwake na kwenye eneo la ndevu ni ishara kwamba umri unaanza kumtupa Mzee Ngoma.

Nimekaa namtazama. Huyu ndiye mtu aliyegundua madini ya Tanzanite. Alipaswa kuwa utambulisho wa Watanzania. Katika nchi nyingine zinazothamini watu wake, huyu alitakiwa kufahamika na watu wote waliomaliza elimu ya msingi.

Kama ambavyo watoto wote wa Kimarekani wanavyomfahamu Thomas Edison (mbunifu mashuhuri na mfanyabiashara wa karne kadhaa zilizopita) . Lakini mbele ya macho yangu, alikaa mzee mmoja ambaye kama ningekutana naye kwenye daladala (na ndiyo usafiri wake mkuu), nisingemtazama mara mbili.

Namuuliza swali moja la msingi kwamba ilikuwaje yeye aliyagundua madini ambayo wakoloni (wazungu) walishindwa kuyabaini kwa muda wote waliokaa hapa nchini.

"Nakumbuka kila kitu kuhusu mara yangu ya kwanza kuona madini hayo. Mara ya kwanza

kuyagundua madini haya nilikuwa mdogo sana. Nilikuwa na umri wa chini ya miaka 20 na nilikuwa porini nikichunga mifugo.

"Nilikuwa kwenye msitu ambao Wamasai walikuwa wameupa jina la Lalouo. Eneo ambako niliyaona lilikuwa linafahamika kwa jina la Naisunyai ambako kwa kawaida Wamasai walikuwa wakilitumia kunywesha mifugo yao.

"Siku hiyo niliona vitu vinavyowaka. Nikawa nashangaa vitakuwa ni vitu gani. Awali nilidhani pengine ni nyoka au wanyama wa hatari. Nikasogea nikiwa na upinde na mshale wangu tayari kwa lolote.

"Nilipogusa na mti niliokuwa nimeushika, nikashangaa mawe yanayong'aa yakitoka ardhini. Vipande vidogo vidogo vyenye rangi ya bluu. Kwa kweli nilivipenda sana.

"Nilishangaa sana lakini ghafla nikakumbuka kuwa nilikuwa nachunga mifugo. Kumbe ng'ombe na mbuzi niliokuwa nawachunga walikuwa wamekimbia tayari. Nikaacha shughuli hiyo na kwenda kuwafuata.

"Kwa bahati nzuri, nilifuatilia njia walizopita hadi nikawapata wote. Lakini ilikuwa kazi ngumu maana ule ulikuwa msitu mkubwa. Nikarudi nyumbani nikiwa na mifugo ile na nikawa nimesahau kabisa habari za madini yale kwa muda ule," anasema.

Mtoto wa Ngoma aitwaye Asha aliyekuwa mwenyeji wetu kwenye ofisi ile ananiuliza kama naweza kutumia kinywaji chochote. Namwomba samahani kwa kuwatia hasara maana nikaagiza vinywaji viwili badala ya kimoja. Maji na soda. Kwenye dunia hii ya kisukari, kunywa soda pekee

bila kuchanganya na maji kunaleta hatari ya kuongeza sukari mwilini.

Mzee Ngoma yeye anaomba maji tu. Tunasubiri kidogo. Tunapiga mafunda mawili matatu na kisha tunaendelea na mazungumzo yetu.

Hata hivyo, mwaka 1966 ilitokea bahati iliyobadilisha maisha yangu. Mwanzoni mwa mwaka huo, serikali ilitangaza kuwepo kwa mafunzo kuhusu utafiti wa madini yaliyopangwa kufanyika mkoani Morogoro.

"Mimi wakati huo nilikuwa nafanya biashara zangu tu lakini nilikuwa mpenzi sana wa masuala ya madini na ndiyo nilipoyaona madini yale ya Tanzanite kwa mara ya kwanza nilishikwa na hamu ya kutaka kuyajua.

"Ulitakiwa kujilipia mwenyewe nauli na gharama nyingine halafu serikali inakulipia mafunzo hayo kwa muda wa wiki tatu. Nikazungumza na mke wangu kuhusu hilo na akaniruhusu niende kwenye mafunzo.

"Nilikwenda Morogoro na hatimaye nikafaulu kwenye mafunzo hayo. Ilipofika tarehe sita, mwezi wa sita mwaka 1966, nikapewa cheti cha utafiti ambacho ninacho hadi leo. Pamoja na mambo mengine, cheti hicho kilikuwa kinakuwezesha kufahamu madini na sifa zake mbalimbali," anasema.

Ni mafunzo hayo ambayo baada ya kuyamaliza yalimfanya Ngoma aweze kugundua madini hayo ya Tanzanite.

Lakini kabla ya madini hayo, mzee huyu kwanza aligundua madini aina ya Gypsum ambayo sasa yanatumika katika nyumba nyingi za Watanzania wenye kipato kuanzia cha kati hadi cha juu.

Aliyagundua madini hayo katika eneo la Chankoko, Makanya mkoani Kilimanjaro.

"Wakati nikigundua madini hayo, hayakuwa na kazi sana. Watu wengi hawakujua kazi yake. Kwa bahati nzuri, katika wakati huohuo, kukawa na kiwanda cha saruji cha WAZO ambacho kilitaka kuanza kufanya shughuli zake na gypsum ilikuwa ni malighafi nzuri sana.

"Kuna bwana mmoja aitwaye Petro Gerson Kizigha akanikutanisha na wazungu waliokuwa wakitaka kuanzisha kampuni hiyo na tayari wakiwa na taarifa za gypsum niliyoigundua.

"Nakumbuka majina ya wazungu hao yalikuwa ni Florench, Carter na Habel. Walikuja hadi Makanya kwa ndege binafsi na walishukia katika shamba la katani la bwana mmoja aliyekuwa akiitwa Hassan.

"Walipoona gypsum ile wakaipenda sana. Wakaagiza mara moja mzigo wa tani 36 ambao tuliupakia kwenye mabehewa. Kuna barabara kutoka Chankoko hadi stesheni ya reli ya Makanya yenye urefu wa kilomita 10 ilijengwa ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa hiyo.

"Mimi ndiye niliyepewa jukumu la ujenzi wa barabara hiyo. Nilipewa na wazungu wale kiasi cha Sh 8,000 kwa ajili hiyo. Kwa wakati huo, hiyo ni hela nyingi sana. Wajenzi walikuwa wakilipwa shilingi nne kwa siku na zilikuwa nyingi kiasi kwamba watu walikuja kuomba kazi kwa wingi hadi wengine nikawakataa, anasema.

Pamoja na mafanikio hayo katika biashara ya gypsum, kuna kitu kimoja kilikuwa kinamsumbua Ngoma kichwani kwake. Yale madini aliyoyaacha kule Umasaini, Marerani yalikuwa ni madini gani?

"Ndipo siku moja nikawachukua ndugu zangu na kuwaomba wanisindikize kwenda kwenye ule msitu wa Lalouo ili nikayachunguze tena yale madini. Niliomba kusindikizwa kwa sababu ule msitu ni mkubwa na nilitaka pia nipate watu wa kunisaidia kubeba.

"Nakumbuka tulichimba karibu kilo sita za madini hayo. Kuna jiwe moja lilikuwa na ukubwa wa takribani gramu 55 hivi. Jiwe kubwa tu. Ndilo lililokuwa kubwa zaidi.

"Nikalipeleka Moshi kwenye Ofisi ya Mkaguzi wa Madini aliyekuwa akiitwa Bills wakati huo. Mzungu huyo. Akayatazama na akasema hajawahi kuona kitu kama kile. Akahisi yanaweza kuwa Blue Tomaline, lakini tukakubaliana kuwa si yenyewe.

"Mimi nikamuuliza sasa mwenzangu unadhani haya ni madini gani? Unajua wazungu ni watu wakweli kidogo. Wana matatizo yao lakini hawapendi kusema uongo. Akasema kwa kweli siyajui. Inabidi tuyapeleke kwenye maabara ya serikali iliyokuwa iko Dodoma.

"Nikampa sampo yote niliyokuwa nayo lakini lile jiwe kubwa zaidi nikabaki nalo. Alipoliona, mke wa bwana Bills akawa amelipenda sana. Akaniomba abaki nalo.

"Nikakataa. Nikamwambia kama nikikupa, nitakuwa nakupa nini? Maana mumeo ambaye ndiye mtaalamu wa mambo haya ameshindwa kuyajua. Siwezi kukupa na nitabaki na hili kama kumbukumbu yangu.

"Ilipofika Septemba 23 mwaka 1967, ndipo nikapokea barua rasmi kutoka maabara ya Dodoma. Vipimo vikaonyesha madini yale yanafahamika kwa jina la Zoisite. Ndiyo maana tunasema madini hayo yaligunduliwa rasmi mwaka huo wa 1967 kwa sababu ndipo cheti kile cha maabara kilipotoka," anasema.

Katika simulizi kuhusu gunduzi mbalimbali za madini hapa nchini, zipo zinazoeleza namna wananchi wa Shinyanga walivyokuwa wakicheza bao kwa kutumia almasi kwa sababu hawakujua thamani yake.

Hali iko hivyo kwa Mzee Ngoma ambaye alikuwa akilitumia jiwe hilo la gramu 55 kwa ajili ya kuzuia karatasi zake zisipepee kutoka mezani kwake. Lilikuwa jiwe la kawaida kabisa ndani ya nyumba yake.

Nimeangalia bei ya sasa ya Tanzanite ili upate picha ya nini mzee huyu alikuwa nacho ndani kwake. Kwa sasa, bei ya madini hayo katika soko la dunia inacheza kati ya dola 500 hadi 700 kwa karati moja.

Zipo taarifa kwamba zipo sehemu duniani ambako watu wanauziwa hadi dola 1000 kwa karati moja. Tuseme wastani ni dola 600 (sh 800,000) kwa karati moja.

Karati moja ni sawa na gramu 0.2. Gramu 55 maana yake ni karati 275. Kama bei ya karati

moja ni Sh 800,000, bei ya karati 275 ni sawa na takribani Sh milioni 220.

Mzee Ngoma alikuwa anatumia Sh milioni 220 kuzuia karatasi na magazeti yasipeperuke kutoka mezani kwake ! Mzee huyu hakujua kitu wakati huo.

Jiwe hilo kipenzi la mgunduzi huyu likaja kumpotea katika mazingira ya kutatanisha. Simulizi yake, ilinifanya niombe mahojiano haya yapumzike kidogo ili niweze kuvuta pumzi.

"Nilikuwa na marafiki wawili wenye asili ya kihindi waliokuwa wakiishi Handeni mkoani Tanga. Mmoja akiitwa Habib Esack Ismail na mwingine akijulikana kwa jina la Nuru Skanda. Walikuja siku moja nyumbani kwangu na wakaliona lile jiwe.

"Wakaniomba waende nalo kwao (Handeni) ili wakawaonyeshe wazazi wao wajue la kufanya. Wakati huo, Zoisite ama Tanzanite kama inavyofahamika sasa, haikuwa maarufu sana na matumizi yake hayakuwa yakijulikana.

"Walisema watalirudisha baada ya siku tatu. Nikawapa na wakaondoka nalo. Hawakurudi baada ya siku tatu na sijawaona tena tangu wakati huo. Siku moja nilikutana na aliyekuja kuwa Kamishina wa Madini hapa nchini aliyejulikana kwa jina la Luwena na akaniambia lile jiwe liko Ujerumani na waliuziwa kwa Sh 6000 kwenye miaka hiyo.

"Hizo ni hela nyingi sana. Ina maana akina Habib waliliuza na wakaondoka zao. Lile jiwe linaniuma sana maana kama ningebaki nalo pengine lingeweza kunipa fedha nyingi," anasema Ngoma.

Machungu ya Mzee huyu hayakuishia hapo. Kuna unyama mwingine mkubwa zaidi ambao alifanyiwa.

Baada ya kuibiwa jiwe lake hilo, akili ya Ngoma ilifanya kazi haraka na akaamua kwenda kupata leseni ya umiliki wa eneo ambako aliyapata madini yale.

Akapewa viwanja nane kwenye eneo lile la Lalouo ambako alilipia kiasi cha Sh 15 kwa kila kimoja. Akaweka alama zote muhimu na kuamini kwamba lile ni eneo lake halali kisheria na mara wakati utakapofika, ataanza kuchimba madini hayo.

"Siku moja mwezi Februari mwaka 1968, nikaenda kutembelea kwenye eneo lile. Nikamkuta kijana mmoja anaitwa Daudi Mayaya akiwa anachimba madini hayo kwenye eneo langu. Alikuwa ameyajaza kwenye ndoo.

"Nikamwambia kwanini amechimba madini hayo kwenye eneo langu? Akanijibu kwamba lile si eneo langu bali ni la mtu mmoja aiwaye De Souza (Huyu nitamweleza zaidi baadaye). Nikamwonyesha alama zangu zote nilizoweka pamoja na nyaraka nilizokuwa nazo.

"Nilipoenda kushitaki Polisi kuhusu huyu mtu anayeitwa De Souza, nikaambiwa ataitwa na atafika Jumatatu. Bila ya taarifa, kumbe huyo bwana akaja Jumamosi na akazungumza na polisi mapema.

"Mkuu wa Polisi kwenye eneo letu alikuwa akifahamika kwa jina la Herbert Kitenge. Huyu bwana akaniita Polisi na akaniambia ameamua kumpa De Souza vitalu (viwanja) vinne kati ya nane nilivyokuwa navimiliki.

"Sasa mimi nikabaki nimeshangaa, inakuaje mtu anapewa vitalu vyangu. Lakini afande Kitenge akasema ama nikubali hiyo dili au nitanyang'anywa vyote. Nikakasirika sana na nikasusa kabisa.

Sikurudi tena kule kwenye machimbo. Nikaenda kufanya biashara zangu," anasema kwa huzuni.

Mzee Ngoma anamtaja De Souza mara nyingi katika maelezo yake. Manuel De Souza, mzaliwa wa Goa nchini India alikuja nchini Tanganyika mnamo mwaka 1933 akiwa na umri wa miaka 20 tu na tayari akiwa fundi cherehani mzuri.

Taarifa katika mitandao mbalimbali duniani inamtaja yeye kama mvumbuzi wa Tanzanite. Mtandao wa Ilios Jewellers unadai kwamba Julai mwaka 1967, kundi la Wamasai, lilimpeleka Mhindi huyo kwenye eneo ambako aligundua madini hayo.

Kwenye mtandao unaoheshimika zaidi duniani wa Wikipedia unamtaja fundi cherehani, Emmanuel Merishiek Mollel kama mgunduzi wa madini hayo. Katika maelezo yake, mtandao huo unadai kwamba ni Mollel ndiye aliyempa De Souza madini hayo na yeye akayapeleka kwa wataalamu ambao waliyabaini kwamba ni Tanzanite.

Hata historia inapindishwa ili Mzee Ngoma akose hadhi na heshima anayostahili !

Kabla ya kuitwa Tanzanite, madini haya yalikuwa yakifahamika kwa jina la Zoisite. Jina hilo, kwa mujibu wa maelezo ya nyaraka mbalimbali, lilitokana na raia wa Austria, Siegmund Zois,

ambaye alikuwa akifadhili safari mbalimbali za watu waliokuwa wakitafuta madini mbalimbali.

Kwa Kijerumani, neno Zoisite linafanana kimatamshi na neno la Kiingereza Suicide. Kampuni iliyokuwa ikifanya biashara ya Tanzanite ya Tiffany& Co. ndiyo ikaamua kubadili jina hilo na kuyaita madini hayo Tanzanite ili liwe na mvuto.

Hakukuwa hata na mmoja aliyeona yanafaa kuitwa Ngomanite au Ngomasite !

Mwaka 1984, serikali iliamka kutoka usingizini na kumtaja Mzee Ngoma kama mvumbuzi wa madini hayo. Kama zawadi yake kwa uvumbuzi huo wa kihistoria, serikali ilimpa mzee huyo

Ngao, cheti cha kumtangaza kama mvumbuzi na fedha taslim Sh elfu 50,000.

Kwa mujibu wa Wikipedia, katika kipindi cha kati ya mwaka 1967 hadi mwaka 1972 wakati serikali ilipoamua kutaifisha shughuli za uchimbaji wa Tanzanite, kiasi cha karati milioni mbili zilikuwa tayari zimechimbwa kutoka Mirerani.

Kwa bei ya sasa ya karati moja, maana yake ni kwamba kwa miaka hiyo mitano pekee, De Souza, washirika wake kama vile Ally Juyawandu na askari jeshi mmoja aliyekuwa na asili ya

Ugiriki aliyefahamika kwa jina moja tu la Papanichalou, walifanikisha biashara yenye thamani ya takribani Sh trilioni 1.6 kwa thamani ya sasa !

Watoto wa De Souza aliyefariki dunia mwaka 1969 akiwa na umri wa miaka 56 kwa ajali ya gari,

wametapakaa katika nchi mbalimbali kama vile Denmark, Malta na Uingereza, pengine wakila faida ya ‘ugunduzi' wa baba yao.

Kwa upande mwingine, Mzee Ngoma amejibanza katika ofisi ndogo ya mwanaye Asha katikati ya jiji. Fedha pekee ambayo ameitengeneza kutokana na kuipa Tanzania sifa na utajiri huu wa kipekee ni Sh elfu 50,000 zile alizopewa na Hayati Rashid Mfaume Kawawa !

Namuuliza shujaa huyu wa taifa anataka nini kutoka kwa serikali; "Sihitaji mambo makubwa sana. Ninachohitaji ni kuishi maisha yanayofanana na Tanzanite. Nataka mtu akiniona mimi aone Tanzanite," anasema.

Ni ombi ambalo linanisisimua. Watanzania wanapaswa kuwafahamu watu kama akina Ngoma. Serikali inapaswa kuwaenzi watu kama akina Mzee Ngoma.

Hawa watachochea watu wawe wagunduzi zaidi. Simulizi zao zitafanya watu wajenge akili ya kuhoji kila wanachokiona. Nani ajuaye, pengine kuna ‘Tanzanite' nyingine katika maeneo mbalimbali hapa nchini lakini hazijulikani kwa vile hakuna akina Ngoma?

Nani atataka kuwa mgunduzi wa vitu vya thamani iwapo wagunduzi waliopo tunapanda nao daladala, tunashinda nao njaa na hawathaminiki?

Serikali imfanye Mzee Ngoma afanane na faida ambayo Tanzanite imeiletea nchi yetu.

Chanzo. Raia Mwema - Ameipa Tanzania utajiri, yeye amebaki masikini
 
MziziMkavu asante sana kuleta hili simulizi la babu yangu Mzee Ngoma hapa JF.
Huyo ni babu yangu mdogo kabisa wa tumbo moja na babu nyamgluu mwenyewe. Hili jina la nyamgluu pia limetokana na aina ya gundi alitengeneza babu na kisha kuishia wapi sijui.
Halafu hii trend ya kufanya ugunduzi na kisha kubaki bila credit nahisi ina run ukoo mzima. Kuna ugunduzi nilifanya nchi flani na nikazinguliwa patent sababu ya u foreigner nikikwambia leo wanatumia huo ugunduzi wangu kwenye nini utabaki mdomo wazi!
Ila naapa mwanangu akija gundua kitu tu aisee nitakishupalia mpaka kieleweke kuua hii chain ya ugunduzi bila credit!
 
Kazi ipo yaleyale ya mzungu kagundua mlima kirimanjaro

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Ndiyo maana hii nchi haifanikiwi kwa mambo mengi,ni kwa sababu ya vijilaana vya namna hii,sasa tanzanite yenyewe inaishia bila hata kuinufaisha tanzania,mwadui imebaki mashimo matupu kwa ajili ya ujinga kama huu huu.
 
Back
Top Bottom