Mimi alinisikitisha aliposema alifungua studio, akakosa fedha ya kuendelea kulipia pango. Kwa sasa vifaa vyake amewekeza kwa mtu.
Ki-ukweli ukimwangalia hata afya yake siyo nzuri coz alisema anaingia hasara , kwani vitu vingi anavyogundua vinahitaji fedha ili kuviweka katika matendo.
Kama alivyosema kama kuna makampuni binafsi yanayoweza kumfadhili, ni vema yakafanya hivyo ili apate fedha ya kununulia vifaa vya kufanyia miradi yake ya ugunduzi. Nadhani makampuni yanayodhamini mpira, miss Tanzania, hata Mzee wetu Mengi ambaye amesaidia wengi katika nyanja tofauti tofauti wamwangalie na huyu.
Kijana anajituma, aliniacha hoi aliposema hata waganga wa kienyeji kule Makambako waliwahi kumtumia abuni vitu vya kushangaza wateja wao ili wapige fedha. Alionyesha mdoli mmoja ambao anauwekea umeme unatikisika bahati mbaya sikuyapata vizuri maelezo yake. Unaweza kuona waganga walikiona kipaji chake wakataka kukimis-use.
Vipaji kama hivi vikiachwa mtaani tu ni hatari, hata majambazi wanaweza kuvitumia kutegua mitambo inayozuia wezi au alarm za magari. Nchi za wenzetu kuwachukua watu kama hawa inalenga mbali sana ukiachia mbali suala la kumsaidia mhusika.