Leo nimeamini Uswazi kuna Great Thinkers wa ukweli

Leo nimeamini Uswazi kuna Great Thinkers wa ukweli

Marire

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Posts
12,333
Reaction score
5,314
Wakuu,

Nilikuwa natazama kipindi cha uswazi cha EATV. Kuna dogo mmoja ana akili sio mchezo na ni mgunduzi wa vitu mbalimbali

- Ana kifaa kimoja kina uwezo wa kufundisha masomo kadri utakavyo feed

- Amebuni njia ya kutoa maji japo hii sikuona toka mwanzo

- Ameulizwa maswali ilikiwa akikutana na waziri wa elimu atamuuliza nini akasema atamwambia apunguze masomo ya shule ya msingi kwani masomo ni mengi wakati maisha ni kitu kimoja.

- Akaulizwa kama Rais ajaye anataka wa namna gani akasema hajaona Rais anayemtaka maana wao wanaamini hakuna vichwa uswazi.

- Akaulizwa kwanini kila mara anamtaja Mwalimu Nyerere, akasema kwake Nyerere bado hajafa anaishi.

Tafadhali mtazame kesho maana naamini hiki kipindi kitarudiwa ila mimi nimebaki kichwa wazi. Pia ana AC katenegeneza yeye anauza 15,000/=.
 
Nimependa sana mtazamo wake. Ana maarifa sana exceptional.
Amesema hapendi marafiki wengi kwa sababu wengi hawana mchango wa maarifa zaidi ya story tu.

Ameulizwa kuhusu anaiambia nini Serikali juu ya kusaidia watu wabunifu kama yeye, amejibu kuwa Serikali ina mambo mengi ambayo haijafanya vizuri kwa hiyo haiwezi kumsaidia labda watokee Watu kutoka sekta binafsi.

Amesema tupo nyuma sana sababu kubwa ni mawazo (hatufikiri vyema).
Zembwela kamuuliza pia Vijana wengi wanashindwa kuwa wabunifu kwa sababu ya starehe, yeye akasema hilo si kubwa sana kibaya ni matumizi ya smart phone yanapunguza sana utendaji. Na mtu anayetumia muda mrefu kuchat uwezo wake wa kufikiri unapungua.

Kifupi yupo smart sana.
 
Ameelezea kuhusu maji sikumpata vyema sana
 
Nchi za wenzetu madogo kama hawa wana kijiji chao wanakua wanawezeshwa kila kila kitu. Bongo pesa inayotengwa kwa research sijui zinaishiaga wapi.
 
platozoom nilitaka nikiangalie mwanzoni hadi mwisho nikapuuzia, du! kumbe kilikuwa kizuri hvyo!
 
Last edited by a moderator:
aiseh kwaiyo kuchati chati mno kuna maliza akili ya kufikiri mambo mengi duhu apo mbona pagumu
 
Supermen Kavumbua AC inatoa baridi kuliko hiyo ya mzungu inatumia umeme na barafu. Kesho wanarudia kipindi, just watch it!!!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom