Leo ni leo huku kwetu Arusha (Mkutano wa CHADEMA)

sawa sawa kabisa,.... mnasonga kuelekea kaburini, tena kwa kasi ya ajabu msiyoitarajia.<br />
<br />
Kumbe na wewe ni jobless!!
Naona kila siku watu wanaikimbia CDM,
Walikuwa wanatarajia mengi kutoka CDM, lakini so far hakuna kitu CDM imefanya! Hamtafika 2015!
 
Hebu wadau linganisheni na habari hii ya gazeti la Uhuru

[h=2]Mbowe akata tamaa Arusha[/h] Wednesday, 10 August 2011 19:18 newsroom




* Amtwisha zigo Lema
* Yeye arejea hotelini

NA MWANDISHI WETU, ARUSHA

MIKUTANO midogo ya viongozi wa CHADEMA iliyofanyika jana jijini Arusha kwa lengo la kuwapaka tope madiwani wake waliovuliwa uanachama, imedorora baada ya kususiwa na wananchi. Jumatatu wiki hii, kamati kuu ya chama hicho, ilitangaza kuwafukuza uanachama madiwani Estomih Malla, John Bayo, Charles Mpanda, Reuben Ngowi na Rehema Mohammed. Chanzo cha wawakilishi hao wa wananchi kufukuzwa CHADEMA ni kushiriki katika mazungumzo na hatimaye kufikia muafaka kuhusu mvutano uliojitokeza kuhusu nafasi ya meya wa Jiji la Arusha. Mbinu ya mikutano midogo iliyoambatana na uzinduzi wa mashina ya uanachama na viongozi wa kitaifa kutembea kwa miguu, akiwemo Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, ilianzia katika eneo la Mianzini na kuhudhuriwa na wananchi wachache.
Iliendelea katika eneo la Soko Kuu lililopo kata ya Kati, huku Mbowe akiwa mstari wa mbele, lakini mahudhurio ya wananchi yalikuwa hafifu.
Kutokana na mapokezi hayo, Mbowe alionekana wazi kukata tamaa na kumuachia shughuli hiyo mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema aendelee katika maeneo yaliyobaki na yeye kurejea hotelini. Lema aliendelea katika kata ya Levolosi na hali ikawa ile ile ya kususiwa na wananchi, vivyo hivyo katika Soko la Mbauda, Sanawari Mataa, Phillips, viwanja vya Soweto na Sombetini. Hata mikutano iliyofanywa na kamati maalumu iliyoongozwa na mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje, haikufanikiwa kutokana na wananchi kuwasusia wakidai hawapendi vurugu zinazoendelezwa na Lema.

Mkutano uliofanyika katika viwanja mbele ya Hospitali ya Mtakatifu Thomas, uliowajumuisha viongozi hao chini ya Mbowe ulionekana kudorora, huku ukitawaliwa na kejeli kutoka kwa wananchi waliohudhuria.

Mikutano mingine ilifanyika katika kata za Kimandolu, Elerai na Sokon One, ambapo mahudhurio yalikuwa hafifu, licha ya viongozi kutembea kwa miguu katika baadhi ya maeneo ili kuwashawishi wananchi kuwafuata.

Katika eneo la Shule ya Sekondari Kimandolu, zilikuwepo dalili za vurugu kutokana na baadhi ya wananchi kuahidi kufanya fujo iwapo viongozi hao wangefika jambo lililosababisha wanafunzi kutokwenda shule.

Lema, katika hali ya kushangaza alitembea kwa miguu kutoka kituo kikuu cha polisi mjini hapa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha, ili kuwashawishi wananchi kumfuata lakini hakufanikiwa kwa kuwa kila mtu alikuwa na shughuli zake za kujitafutia riziki.
"Yeye (Lema) akitembea, akisimama au akikaa mshahara wake, posho zake viko pale pale, sasa mimi nikiacha biashara zangu nitapata wapi pesa, wabunge hawana shida bwana," alisema Sadick Mashauri, mwananchi aliyezungumza na gazeti hili kuhusu mikutano hiyo.
gazeti la uhuru na magamba ni mtu na baba yake-kwa hiyo habari kama hii si ya kushangaa-ndio maana hata leo bungeni kuna mbunge kasema kila chama kina magazeti yake-so hawa wapo pamoja
 
umati.jpg
photo1.jpg


Haya wakuu picha hizo hapo kwa uchache, kwa hisani ya n00b
chadema-leo.jpg
 
Naona kila siku watu wanaikimbia CDM,
Walikuwa wanatarajia mengi kutoka CDM, lakini so far hakuna kitu CDM imefanya! Hamtafika 2015!

chadema huwa inafukuza wajinga wajinga kama wale "madiwani" mliowafisadi.

na kutokana na umakini huo wanamagamba wasio na fikra finyu wanahamia airtel(chadema). Ila bahati mbaya wewe ukihamia hautapokelewa.
 
Daffi, usikimbilie sehemu ambapo unajua hupati msaada wowote!
Wanajidai kuwa wakombozi lakini so far hawajafanya lolote!

angalia picha hapo nimekuwekea, usiendelee kuzurura mwishowe ukakosa taarifa muhimu za kumpelekea nape.
 
Kwa kifupi idadi ya watu waliojitokeza ni aibu kwa hao madiwani, ccm na Pinda kwa ujumla! Watu walikuwa wengi sana! Wanatofautiana kidogo sana na waliohudhuria mkutano wa kuaga maiti tar 11, jan.
Kiukweli, ccm hawana chao Arusha. Wasahau tu waendelee na majimbo mengine!
 
nitamueleza mbunge wangu apeleke hoja bungeni ili chama cha chadema kifutwe; kwasababu kinatishia amani ya nchi pia anampango wa kumuondoa madarakani rais aliyechaguliwa kidemokrasia kimabavu; hili ni kosa kwa mujibu wa katiba!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom