Usalama wa wasafiri Arusha siku ya leo, Julai 3, 2023

SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
2,923
2,003
Ninaanza kwa masikitiko makubwa sana sina muda wa salamu.

Kila Mtanzania anajua kinachoendelea Arusha leo sitaki kuelezea hilo, ila nitaenda moja kwa moja kwenye mada, mnisamehe kwa uandishi mmbovu.

Leo hii jiji kubwa la Arusha liko kwenye kadhia kubwa ya usafiri wa umma kutokana na mgomo wa wasafirishaji wa abiria, kinachoniumiza sijasikia wale ambao hawapendi kuona maafa ya ajari za barabarani au vifo vya uzembe wakitoa tamko la kukumea vyombo ambavyo si salama kubeba abiria kama kirikuu na pikipiki za matairi matatu leo ndio zimeupamba mji zikibeba roho za watanzania wengi kuwafikisha waendako bila maofisa usalama barabarani kukemea hali hiyo.

Guta leo inabeba raia. Uongozi wa mkoa wa Arusha hauna magari ambayo hata tungeyaona barabarani muda huu walau yakijari hata watoto wanafunzi ambao ni taifa la kesho kuwachukua vituoni na kuwafikisha waendako?

Mwisho sio Serikali peke yao tu nimeona hadi CHADEMA wakizunguka mitaani kunadi mkutano wao wa kesho bila kujari mafuta wanayoyatumia yangetumika hata kubebea wananchi kwa leo tu kupunguza adha hii.

Tuna majeshi kariba na mkoa wetu wanayo magari mengi yangesaidia kupunguza adha hii ambayo wallpa mishahara wao wanapitia.

Pia soma: Mgomo wa Daladala Jijini Arusha asubuhi hii ya Julai 3, 2023
 
Yote hayo kwa sababu ya tatizo la ajira, matokeo yake kila Kijana anataka kuingia barabarani kutafuta chochote kitu.
 
Back
Top Bottom