At Calvary
JF-Expert Member
- Aug 22, 2018
- 4,530
- 3,586
Spika wa Bunge Job Ndugai leo November 30,2020 atawaapisha Wabunge wawili walioteuliwa na Rais Magufuli, Wabunge hao ni Humphrey Polepole ambaye ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM na Riziki Said aliyekuwa Mbunge Viti Maalum katika Bunge la 11 kupitia CUF.
Shughuli za uapisho zitafanyika katika Viwanja vya Bunge Jiji Dodoma saa 10:00 Jioni.
Spika Ndugai: Wako rafiki zetu ambao hivi karibuni wamejipambanua kwa kukejeli shughuli za bunge, niwatahadharishe na kuwakumbusha labda wamesahau kwamba ni jambo lisilokubaika kwa mtu yeyote kudharau shughuli za Bunge, kudhalilisha Bunge, kudhalilisha uongozi wa Bunge na hata kudhalilisha wabunge waliokwisha kuapishwa.
Kufikiri kwamba Bunge ni ukumbi wa Bunge peke yake ni fikra finyu sana. Kwa hiyo wabunge wote wa Bunge la 12 tuliowaapisha tunaendelea kuwatambua ni wabunge kamili ikiwa ni pamoja ni pamoja na wale 20 wa chama cha CHADEMA, kumi na tisa na yule mmoja aliechaguliwa ambae ni mheshimiwa Aida Khenan. Nashangaa wanawasonga hawa 19, yule mmoja wamemgwaya? Wakiweza wamfukuze basi lakini sisi tumeshamuapisha na tunamtambua kwamba ni mbunge wa Bunge la 12, hayo yanayoendelea huko yakwao.
Hebu waacheni wastaafu wetu wapumzike, tuwaache wapumzike wazee wetu wamefanya kazi nzuri iliyotukuka, mambo huku nyuma yao yanabadilika kwa hiyo mnapowafata wakati wao wana kumbukumbu zile za wakati ule na huku kuna mambo mapya yanaendelea mnataka kuwachonganisha wazee hawa na wananchi wa Tanzania na si haki.
Si vizuri baadhi ya vyombo vya habari mnaofanya namna hii, waacheni wazee wapumzike.
Kwa hiyo wale waliokuwa na wasiwasi wale wabunge 19, niwahakikishie wale ni wabunge kamili wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania na niwakumbushe wanahabari, kila mnapowatamka majina yao muanze na neno mheshimiwa.
Yupo rafiki yangu mmoja nimtaje tu jina, mheshimiwa Freeman Mbowe tulianza nae ubunge mwaka 2010, tunafahamiana vizuri japo alipigwa chini hapo katikati, mimi nimeendelea moja kwa moja. Mwenzangu alipigwa chini, mzoefu wa kuanguka kwenye chaguzi hizi wala sio mara ya kwanza.
Amesimama akaanza kuwatukana hadharani waheshimiwa wabunge hawa wanawake, kwa mtu mzima na mwanaume wa kitanzania uliyefundwa ni aibu kubwa kutukana wanawake hadharani, ningependa kuchukua nafasi kumuonya na kumkanya hadharani asione sifa katika jambo hilo.