Barua ya wazi kwa Job Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
BARUA YA WAZI KWA MHE SPIKA NDUGAI.

Na Elius Ndabila
0768239284

Mhe Spika Ndugai Shikamoo! Ni matumaini yangu Mungu anaendelea kukupigania katika hali yako kiafya. Jana wakati unazungumza na vyombo vya habari ulisema unachangamoto ya kiafya.Ninakuombea kwa Mungu upate tahafifu.

Mhe Spika, wiki iliyopita baada ya matamshi yako kuzagaa mitandaoni Mimi ni sehemu ya walitoa ushauri kwako juu kauli ile. Ushauri wangu nilisema katika mataifa yanayosimamia utawala bora Kwa vitendo na kuheshimu mila na desturi ulipaswa uwe umejiuzulu nafasi ya Uspika.


Nilisema uwe umetamka yale maneno kwa Bahati mbaya au kwa kutafsiriwa vibaya, ulipaswa kujiuzulu. Nilienda mbali kuwa kujiuzulu siyo fedheha bali ni kuonyesha kuwajibika kwenye jambo ambalo limeleta shida ktk taifa.Jana niliposikia umeita vyombo vya habari nilidhani unataka kujiuzulu mbele ya Camera.

Mhe Spika, ninajua msamiati kujiuzulu Kwa Waafrika ni mgumu sana hasa pale ambapo kazi inakuwa si utumishi tena inakuwa ni ajira. Madaraka ni kama kilevi. Madaraka ukiyavaa yanalevya na unakuwa kwenye sayari nyingine.

Mhe Spika, jana baada ya kutazama Video yako ukionyesha utetezi wa kile ambacho ulikizingumza Mimi nilisema Mhe Spika tumsamehe. Nilisema Mimi ninamsamehe, Kwa maana ya kupunguza hisia ya kile nilichokuwa nimekiweka kichwani. Sikujua kama kuna agenda kubwa na kauli haikuwa ya bahati mbaya.

Mhe Spika, leo sikupata nafasi ya kumsikila Rais Mhe Samia. Lakini nilipowasha simu nilikutana sms kadhaa kwenye Simu zikiniuliza umemsikia Mama? Lakini Kwa kuwa nilikuwa sijui chochote niliingia kwenye mtandao ambao binafsi ninauamini kama chanzo kizuri Cha tetesi. Niliingia Jamii Forum. Nilikutana na nukuu za Mhe Rais ambazo zilinifanya nikimbilie YouTube kupata madini haswaa.

Mhe Spika, sisi kwenye Sheria uliuweze kuamua unapaswa kusikiliza pande Mbili za watu. Wiki iliyopita na jana nilipa fursa ya kukusikiliza wewe. Leo nimepata fursa ya kumskiliza Mhe Rais. Mhe Spika kwa katiba na Sheria zetu Mhe Rais ana vyanzo vingi vya taarifa kuliko mtu yeyote nchini. Rais ndiye anayejua Kila Siri
Ya nchi hii.

Mhe Spika, Mimi binafsi baada ya hotuba ya Mhe Rais ninakushauri Kwa masilahi mapana ya Taifa hili jiuzulu nafasi yako ya Uspika. Taifa haliwezi kuendelea kama Bunge na serikali mnapishana. Mhe Spika kwa kauli ya Mhe Rais wewe na wengine unaowajua mnamhujumu Mhe Rais.

Mhe Spika, ninakushauri ili kulinda heshima yako jiondoe kwenye nafasi ya Uspika kabla Wabunge hawajafikia uamzi wa kukuondoa. Mhe Spika, maneno yako yameshatengeneza ufa mkubwa Kati ya Serikali na Bunge, ili kazi ziende unatakiwa kuondoka.

Mhe Spika, sisi wananchi ambao tunaona spidi ya maendeleo huku vijijini hatutakubali hujuma yoyote kwa Mhe Rais. Kugombea ni haki ya kila mtu, lakini tusitumie haki hiyo kuwaumiza wengine.

Mhe Spika, nitasikitika kuendelea kukalia hicho kiti. Hutakuwa kiongozi wa kwanza kujiuzulu. Ili Rais aweze kufanya kazi yake vizuri unatakiwa uondoke. Sisi tunahitaji maendeleo, wananchi hatuhitaji ugomvi. Walishajiuzulu Mzee Mwinyi, Mzee Mrema, Mzee Lowasa na wewe hutakuwa wa Kwanza kuonyesha kuwajibika kwenye kauli uliyozua nongwa na hisi za 2025.

Mhe Spika, nimalizie Kwa kusema CCM ni maarufu kukiko sisi sote. Umaarufu tunaojivunia ni Kwa kuwa CCM imetupatia, kinyume cha hapo sisi siyo maarufu bali ni mashuhuri.

Kuwa na imani katika ubinadamu. Binadamu ni kama bahari; ikiwa na matone machache bahari inakuwa chafu, yaani bahari nzima inakuwa chafu. " - Mahatma Gandhi
 
Masaa 72 ya Gwajima kumwondoa Amaleki yanakaribia. Amaleki jipime uone kama bado unafaa kuendelea kukalia hicho kiti cha uspika.
 
Rekebisha kujiuzulu ondoa dhu, rejea zako za kimataifa spika Ana haki na Samia kakiri hilo kwa jamii komavu na yenye welevu spika hana kosa, ila utopolo wetu Tanzania ni aibu kupingwa sio hoja muhimu jitetee kwa kupinga hoja. Ndugai hoja anayo na mipasho ya Samia sio afya kwa Taifa, awe na tahadhari sana watanganyika wapo wanamuangalia
 
#Shame kwamba tunampinga Ndugai wakati ya jikoni hatuyajui!

Tanzania ingekuwa nchi ambayo wananchi wake walau robo wangekuwa wanajitambua hakika ccm ya SSH ingepata wakati mgumu sana.
Maoni ya mtu kama Spika si ya kupuuzwa. Kuna jambo analijua haliko sawa. Spika ni zaidi ya mtu au kiongozi wa kawaida. Zaidi ya kutoka chama kimoja na SSH, ni kiongozi wa mhimili wa Bunge unaojitegemea.
Kuna mengi mengi hayapo sawa. Ingekuwa ni nchi nyingine yenye wananchi wanaojielewa tusingesubiri akina Bashiru, Kassim, Pole Pole, et al ndo watusaidie kuelewa ubovu wa ccm??
Wengi wanaogopa ndo kama hivyo wakiongea ukweli wanalazimishwa kujiuzulu...

NB: Tungekuwa na upinzani makini hakika Ndugai asingeishia tu kujiuzulu Uspika... Angejiuzulu ubunge na nafasi zake zote ndani ya ccm na hapo ndipo nchi ingeshuhudia mtikisiko mkubwa ndani ya ccm. Mtikisiko ambao ungekuwa na faida lukuki kwa nchi yetu!
ccm inatakiwa iwekwe pending kama KANU Kenya kwa maslahi mapana ya taifa na waTanzania.
 
Rekebisha kujiuzulu ondoa dhu, rejea zako za kimataifa spika Ana haki na Samia kakiri hilo kwa jamii komavu na yenye welevu spika hana kosa, ila utopolo wetu Tanzania ni aibu kupingwa sio hoja muhimu jitetee kwa kupinga hoja. Ndugai hoja anayo na mipasho ya Samia sio afya kwa Taifa, awe na tahadhari sana watanganyika wapo wanamuangalia
Umeleta hoja nzuri sana!!
Sasa watu dizaini ya mleta hoja ndo wapo wengi Tanzania. Na ndo maana tutachelewa sana kutoka hapa tulipo!
Ndugai ana mapungufu yake lakini ana hoja inayohitaji majibu muafaka kwenye sakata lake na SSH.
Sioni mwisho mwema wa SSH kama waTanganyika wataamua kufunguka akili.
 
Back
Top Bottom