Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Aliyekuwa Dc wa Hai Ole Sabaya baada ya kuhukumiwa amewatoa wasiwasi wafuasi wake kwa kuwapa kauli ya kiroho , Amesema hivi , Nanukuu , MSIJALI MAANA MUNGU YUKO KAZINI , Mwisho wa kunukuu .

Chanzo : Mwananchi

Nachukua nafasi hii mimi binafsi kuipa pole sana familia ya Ole Sabaya kwa shida iliyotokea kutokana na hukumu aliyopewa kijana wao .
Pamoja na alikuwa bedui lakini inaumiza kijana kufungwa, ameacha binti mrembo sana
 
Duh!!!? Siasa ni hatari,

enzi hizo nikiwa chuo nilikua active Sana Katika politics, hao akina makonda na madogo hao akina Sabaya wakiwa wajanja wajanja tu, hata kujenga hoja walikua hawawezi, Kuna mbunge vito maalum Alice ...jina la kihaya hovyo kabisa, akina Happy.

Ghafla baba angu akaniita, akaniambia politics ina risks nyingi Sana, ikiwemo assassinations, Kufungwa,kuchafuliwa.
Akaongeza, 'my son, you have been the best in every class you go through, I am sure you deserve better than taking risks of that level'

Akaishia hapo. Kwa shingo upande nikawaacha Hawa jamaa. Kwa sasa babaangu ni marehemu, nipo comfortable na secluded life.
Namkumbuka Sana baba yangu hasa nikiona haya yanatokea.

NB; Kwa formula ya political calculations, nina wasisi Kama Mbowe atachomoka.

ni mawazo binafsi yasiofungamana na upande wote.
 
Back
Top Bottom