Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Hilo la jambazi unalisema wewe siyo mahakama!
Kwani aporae Kwa kutumia silaha huko lumumba mnamwitaje manka? Au jambazi huko lumumba mnamwita malaika mlinzi? Sishangai Kwa utetezi wako kwani nawe ni mmoja wao mnaojificha huko ccm! Siku zako zahesabika na huenda zisitimie arobaini!
 
Mchumba mwenyewe

IMG_20211015_150258.jpg
 
Wanajukwaa poleni kwa kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa Taifa letu,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Bila shaka baada ya Hukumu ya Lengai Ole Sabaya kuhairishwa tarehe 1/10/2021 ilipangwa kwamba itatolewa leo. Hivyo tuelekeze masikio yetu katika viunga vya mahakama.

=======

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili leo Ijumaa Oktoba 15, 2021 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusikiliza hukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Amalia Mushi aliahirisha hukumu hiyo Oktoba Mosi, 2021 baada ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, kutokamilisha kuandika hukumu hiyo.

Agosti 24 mwaka huu, Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura walikamilisha kujitetea mahakamani hapo baada ya Jamhuri kukamilisha mashahidi 11 na vielelezo vinane.

Sabaya alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 4, mwaka huu baada ya kukamatwa Mei 27 wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Chanzo: Mwananchi

UPDATE: MAHAKAMA YAMKUTA NA HATIA OLE SABAYA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imemkuta na hatia Lengai Ole Sabaya na wenzake katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha.

Mahakama ilimpatia nafasi Ole Sabaya ajitetee(Shufaa) kwanini asipewe adhabu kali naye aliiomba Mahakama imuonee huruma kwani si yeye bali alikuwa anatekeleza amri ya mamlaka ya uteuzi, pia ameomba mahakama imuonee huruma kwani ana mchumba anayetegemea kufunga naye ndoa na mahari ameshalipa.

UPDATE: SABAYA NA WENZAKE MIAKA 30 JELA

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wamehukumia na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.

WASIFU WA OLE SABAYA

Lengai Ole Sabaya amezaliwa 26/12/1986 mkoani Arusha. Amesoma Shahada ya Sayansi katika Elimu Chuo Kikuu cha Mtakatifu John Dodoma (St. John University).

Ole Sabaya aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) Mkoa wa Arusha na pia aliwahi kushika wadhifa wa Udiwani katika kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha Mjini mwaka 2015.

Ole Sabaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro tarehe 28 Julai 2018 ya aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano, Hayati John Pombe Magufuli.

Sabaya alitenguliwa nafasi hiyo ya ukuu wa Wilaya ya Hai tarehe 13 Mei 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan ili kupisha uchunguzi wa makosa yaliyokuwa yakimkabili ikiwemo unyang’anyi wa kutumia silaha. Tarehe 15 Oktoba 2021 Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha imemhukumu Sabaya na wenzake kifungo cha miaka 30 jela.
Hili ni fundisho,wenye mamlaka msiwe mnatumia madaraka vibaya kwa visingizio vya kutekeleza amri ya mamlaka ya uteuzi au aliye juu.

Awamu ya tano ikiendesha magenge ya kihalifu yakifadhiliwa na wanaoitwa wenye mamlaka imeumiza Sana watu,imagine waliopotea hawajulikani waliko.

Safi Sana mahakama hii iwe fundisho na Kwa wengine wenye kutumia mamlaka ndivyo sivyo.
 
Mbowe anafungwa tuombe tu Mungu na tuendelee kuwepo

Hukumu ya sabaya hii 30 na bado ana kesi nyingine je akiukumiwa Tena 30 maana yake 60 hapa Kuna harufu ya siasa .

Aliokuwa akifaya nao Kazi wamemzunguka na kumtosa!!

Ila nawashauri msije kujaribu kumfunga Mbowe kitanuka street wajeda lazima watakinukisha tu!!
Acha kuwachafua wanajeshi wetu mpuuzi wewe, wakinukishe kivip??

Kesi ya mbowe mwanzo tu ishaonyesha Kuna kasoro kibao ambazo zitamfanya aachiwe mapema Sana
 
Mnamfunga wanini? Huyo sabaya angeny'ongwa tu biaahara iishe pumbavu zake
 
Hivi mkewe/mchumba ana watoto? Pengine anaweza kumngoja akirudi na 40-50yrs
Kama hakufunga magoli sidhani kama huyo mke atamngoja
 
Back
Top Bottom