Lema: Sikuogopa nilipoona mwanajeshi anapiga picha na mimi

Lema: Sikuogopa nilipoona mwanajeshi anapiga picha na mimi

Doulbe standards, kuna sheria na kanuni kibao CCM wanazikiuka makusudi kwa maana ya kwamba kwao ni sahihi, Mfano watumishi wa Uma kuhudhuria mikutano ya CCM na kueleza mipango ya kufanikisha wizi wa wakubwa zao...nk. Kifungu kwa kifungu... tutawakamata... Watu siku hizi wanachimba mistari, hakuna kulala, kugonga meza na kuitikia ndi.......o!

Sorry, nje ya topic: Hakuna kitu sikipendi kama utaratibu huu wa kuhoji wanaoafiki waseme Ndiyo na wasioyo afiki waseme Hapana! Sipati picha namna Spika anavyohesabu sauti hizo.. Katiba Mpya ilione hili.
 
Ujumbe alioutoa Lema ni kwamba ni sawa kwa CHADEMA kufanya makosa iwapo makosa hayo pia yanafanywa na vyama vingine. Naona mashabiki wa CHADEMA mnashangilia hili, sijui kama mmeelewa ina implication gani in the future!

Lema anasema "Hili ni jaribu kubwa kwa Serikali ya Kikwete na kama Mbunge ningeshauri fanyeni kama hamjaona jambo hili..." : hapa anamaanisha kuna makosa yanatakiwa kufumbiwa macho ili kukidhi mahitaji ya kisiasa. Je, huu ndio uongozi mnaoutaka watanzania? Hayo ndio mabadiliko yanayowafanya muandamane barabarani kila siku?

Safari barabarani, akili kichwani...
Mkuu bado hujaelewa kabisa.
Swali je ni kosa kwa Askari yule kupiga picha na wabunge wa Chadema?

Na kama kitendo kile kitaweza kutafisiriwa kuwa ni kujihusisha na siasa kwa askari basi hatua za kisheria zinapaswa kuchukuliwa lakini sio kwake tu na kwa Maafisa wa juu wa jeshi(akiwemo Kanali Ndomba ambaye kwa sasa ni mnadhimu mkuu wa JWTZ)
Vinginevyo itakuwa ni Double standard.
 
Lema ndiyo kaandika au kaandikiwa haya maelezo.

Akiandika au kuandikiwa yote sawasawa kubwa kitu kimesimama -na mashiko yake yanagusa na kuweza kufanyanimpact nzuri!!!n he can stand for it
 
Ujumbe alioutoa Lema ni kwamba ni sawa kwa CHADEMA kufanya makosa iwapo makosa hayo pia yanafanywa na vyama vingine. Naona mashabiki wa CHADEMA mnashangilia hili, sijui kama mmeelewa ina implication gani in the future!

Lema anasema "Hili ni jaribu kubwa kwa Serikali ya Kikwete na kama Mbunge ningeshauri fanyeni kama hamjaona jambo hili..." : hapa anamaanisha kuna makosa yanatakiwa kufumbiwa macho ili kukidhi mahitaji ya kisiasa. Je, huu ndio uongozi mnaoutaka watanzania? Hayo ndio mabadiliko yanayowafanya muandamane barabarani kila siku?

Safari barabarani, akili kichwani...

Kuondoa siasa katika analysis ni kazi ngumu.

Kuna watu hapa wana unazi, kiasi kwamba ukihoji mambo fulani ni sawa na kumwambia mtu wa miaka 30 "huyu unayefikiri ni baba yako si baba yako". Mnaweza kupigana hata kama una majibu ya DNA test.

Lema is a disappointment if you want to look at this with non partisan eyes.
 
lema alitegemea wale polisi kuwajibika kwanza na alipona hawajaona shida aliona lazima kuna uhalali.pengine ni ulinzi mpya kapewa.Wale polisi ndio vimeo au walishiriki kufanya hila kwa CDM.Bahati yao mbaya Lema na CDM ndio wanapiga score.
 
Kuondoa siasa katika analysis ni kazi ngumu.

Kuna watu hapa wana unazi, kiasi kwamba ukihoji mambo fulani ni sawa na kumwambia mtu wa miaka 30 "huyu unayefikiri ni baba yako si baba yako". Mnaweza kupigana hata kama una majibu ya DNA test.

Lema is a disappointment if you want to look at this with non partisan eyes.

kweli wewe una kiranga!
 
kwani wewe Riz mbona watu wamesema mara nyingi kuwa unamuandikia mtu fulani maelezo
 
Kuondoa siasa katika analysis ni kazi ngumu.

Kuna watu hapa wana unazi, kiasi kwamba ukihoji mambo fulani ni sawa na kumwambia mtu wa miaka 30 "huyu unayefikiri ni baba yako si baba yako". Mnaweza kupigana hata kama una majibu ya DNA test.

Lema is a disappointment if you want to look at this with non partisan eyes.
Acha wivu na hasira ndugu yangu.
Jenga hoja kama unaweza.
Kama imekuuma sana kaa kimya tu kama mimi hapa na utakuwa umefanya jambo la maana.

Lema ndio karudi kwenye Ubunge wake, utapata shida sana kama utaendelea kumchukia.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Wivu kwa kipi hasa? Uharisho?

Hasira? Hasira imenikasirikia mie kwa amani niliyo nayo.

Hoja? Hoja hata ukiiona utaijua wewe? Umesoma mabadniko yangu hapo juu na kuyaelewa?

Kuniuma? I am beyond kuumia. Kukaa kimya? Mie ntapaka sawasawa na huwezi kuninyamazisha hapa.

Lema hata akiwa rais, acha mbunge, hii habari itabaki kuwa uharisho katika rekodi yake.
 
Kuondoa siasa katika analysis ni kazi ngumu. Kuna watu hapa wana unazi, kiasi kwamba ukihoji mambo fulani ni sawa na kumwambia mtu wa miaka 30 "huyu unayefikiri ni baba yako si baba yako". Mnaweza kupigana hata kama una majibu ya DNA test. Lema is a disappointment if you want to look at this with non partisan eyes.
Ni mtizamo kama huu wako ndio umelifikisha taifa letu la Tanzania hapa tulipo...watu kujidanganya kuwa kwa kutetea upuuzi kama unavyojaribu kufanya eti ndio to look at an issue with non partisan eyes, non partisan eyes my foot! Wahenga wana msemo kuwa ukitupa kombora halafu ukasikia kilio cha uchungu, ujue kombora limempata mtu! Lema katupa ndoana na kama kawaida ya wakurupukaji kibao ndani ya jamhuri yetu inayoitwa Tanzania, wako walioimeza hook, line and sinker! Sasa wanajiumbua wenyewe kwa kutawaliwa na fikra za unafiki na undumilakuwili!

Hivi kazi ya jeshi ni kuilinda ama kuitii serikali iliyo madarakani? Serikali iliyoko madarakani inawajibika kwa wananchi walioiweka madarakani, sasa inakuwaje hiyo serikali inapoacha kuheshimu mkataba baina yake na wananchi kama katiba...hapo jeshi linatakiwa lisimame upande gani...wa wananchi au serikali? Binafsi naamini kazi ya jeshi si kuilinda serikali bali nchi na wananchi wake, jeshi linatakiwa liwe rafiki na si adui wa mwananchi na ikitokea wananchi wanaamua kukatisha mkataba waliowekeana na serikali yao, chombo kama jeshi kinatakiwa kukaa kando.

Kuna namna nyingi ya kufikisha ujumbe na hasa kwa serikali iliyoundwa na chama kinachoamini kina hati miliki ya kutawala na inayojifanyia mambo hovyo with impunity kama tunavyoshuhudia. Jeshi limekimbilia kutoa tamko kwa sababu njia iliyotumika kutuma ujumbe is effective...ndio wanaoweza kuielewa kwa haraka hawa walevi wa madaraka. Mwaka 2010 ilipoonekana kuna hatari ya wananchi kuikataa CCM, jeshi lilijisahau na haraka likatoa tamko kama kitengo cha CCM la kuwatisha na kuwaonya wananchi, jeuri ambayo inaonekana ni kawaida sana kwa nchi kama zetu.

Nasema na ninarudia, hakuna kosa lolote kwa mwanajeshi kupiga picha ama na mbunge wake au mwanachi yoyote yule na kama kuna watu hawaafiki basi ujumbe umefika.
 
Ni mtizamo kama huu wako ndio umelifikisha taifa letu la Tanzania hapa tulipo...watu kujidanganya kuwa kwa kutetea upuuzi kama unavyojaribu kufanya eti ndio to look at an issue with non partisan eyes, non partisan eyes my foot!

Upuuzi ni upi sasa? Kutazama vitu with non partisan eyes ndo upuuzi? Kwa hiyo wote tutazame mambo kwa macho ya CHADEMA vs CCM. Chochote atakachofanya kada wa CHADEMA poa kwa sababu ni kada wa CHADEMA, chochote atakachofanya kada wa CCM kibaya kwa sababu ni kada wa CCM? And vice versa for the other side?

Wahenga wana msemo kuwa ukitupa kombora halafu ukasikia kilio cha uchungu, ujue kombora limempata mtu!

Kwa hiyo hata ukiharishia watu wasiseme umewaharishia kwa sababu ya kuogopa kusemwa wamepatwa na kombora? Kombora ni lipi hapa? Huu uharisho wa Lema asiyejua hata kuandika utetezi? Ndo kombora hilo?

Hivi wewe unaweza kusoma hicho alichokiandika huyo Lema ukaniambia for real kwamba "This is the leadership we want in Tanzania"? Labda you can't see past a certain level of uharisho.

Lema katupa ndoana

Damn right katupa ndoana. Kwa airheads watakaoona picha ya mwanajeshi na kupiga kelele "ndiyo kamandaa" bila kuangalia the larger implication kwamba vita ya wenyewe kwa wenyewe inaweza kuanza kimasihara hivi hivi kama watu hawataheshimu separation ya jeshi na siasa.

na kama kawaida ya wakurupukaji kibao ndani ya jamhuri yetu inayoitwa Tanzania, wako walioimeza hook, line and sinker! Sasa wanajiumbua wenyewe kwa kutawaliwa na fikra za unafiki na undumilakuwili!

Mkurupukaji namba moja huyo Lema wenu asiyejua mwanasiasa nani na civil servant nani.

kazi ya jeshi ni kuilinda ama kuitii serikali iliyo madarakani? Serikali iliyoko madarakani inawajibika kwa wananchi walioiweka madarakani, sasa inakuwaje hiyo serikali inapoacha kuheshimu mkataba baina yake na wananchi kama katiba...hapo jeshi linatakiwa lisimame upande gani...wa wananchi au serikali? Binafsi naamini kazi ya jeshi si kuilinda serikali bali nchi na wananchi wake, jeshi linatakiwa liwe rafiki na si adui wa mwananchi na ikitokea wananchi wanaamua kukatisha mkataba waliowekeana na serikali yao, chombo kama jeshi kinatakiwa kukaa kando.

You are contradicting yourself. Unasimamia "jeshi kukaa kando" wakati unatetea Lema kuliingiza jeshi katika siasa? How do you reconcile the two irreconcilable positions? Hapa Lema hajaliacha jeshi kando, kaliingiza jeshi katika siasa. Mie ndo nataka jeshi liachwe kando, wewe unamtetea Lema, hutetei jeshi liachwe kando ya siasa, unatetea jeshi liingizwe katika siasa kama anavyofanya Lema.

Kuna namna nyingi ya kufikisha ujumbe

Lakini vile vile kuna ground rules, codes of conducts and first principles. Ndo maana yule kichaa mwingine Nassari alivyosema Kikwete atakanyaga huko kaskazini kwa visa na maneno ya kujitenga ilibidi mui address ile gaffe.

This is another gaffe, kubalini tu.

na hasa kwa serikali iliyoundwa na chama kinachoamini kina hati miliki ya kutawala na inayojifanyia mambo hovyo with impunity
Ukiviijibu chama/ serikali vinavyofanya mambo ovyo with impunity kwa kufanya mambo ovyo with impunity na wewe, sisi wananchi tuliotegemea tuone kitu tofauti kutoka kwako tunawaona wote wazugaji tu. Unapoteza hata moral high ground ya kukisema hicho chama tawala.
Wananchi tutaangalia na kusema "Hata kama ni kweli CCM inatumia jeshi isivyo sawa, hawa CHADEMA nao kwa kutoheshimu mtenganisho wa jeshi na siasa hawatuonyeshi chochote kipya"
kama tunavyoshuhudia. Jeshi limekimbilia kutoa tamko kwa sababu njia iliyotumika kutuma ujumbe is effective..

Effective to what end? Ku accelerate civil war?

ndio wanaoweza kuielewa kwa haraka hawa walevi wa madaraka.

Na huyo Lema kutoweza kuchekecha na kuona hizi habari za kuchanganya jeshi na siasa si ulevi wa madaraka? Mbona mnawasema CCM kwa mambo yale yale mnayoyafanya na nyie? Hivi huyu Lema anaweza kuwasema CCM kwa "ulevi wa madaraka" with any moral high ground?

Mwaka 2010 ilipoonekana kuna hatari ya wananchi kuikataa CCM, jeshi lilijisahau na haraka likatoa tamko kama kitengo cha CCM la kuwatisha na kuwaonya wananchi, jeuri ambayo inaonekana ni kawaida sana kwa nchi kama zetu.

So CCM ikijiharishia na kujionyesha inatumia jeshi bila kujali kanuni jibu lenu na nyie ni kujiharishia hivyo hivyo ili tujue hamna tofauti na CCM?

Nasema na ninarudia, hakuna kosa lolote kwa mwanajeshi kupiga picha ama na mbunge wake au mwanachi yoyote yule na kama kuna watu hawaafiki basi ujumbe umefika.

Umesoma sheria na kanuni za wanajeshi na siasa Tanzania au unabwabwaja tu?
 
Ni mtizamo kama huu wako ndio umelifikisha taifa letu la Tanzania hapa tulipo...watu kujidanganya kuwa kwa kutetea upuuzi kama unavyojaribu kufanya eti ndio to look at an issue with non partisan eyes, non partisan eyes my foot! Wahenga wana msemo kuwa ukitupa kombora halafu ukasikia kilio cha uchungu, ujue kombora limempata mtu! Lema katupa ndoana na kama kawaida ya wakurupukaji kibao ndani ya jamhuri yetu inayoitwa Tanzania, wako walioimeza hook, line and sinker! Sasa wanajiumbua wenyewe kwa kutawaliwa na fikra za unafiki na undumilakuwili!

Hivi kazi ya jeshi ni kuilinda ama kuitii serikali iliyo madarakani? Serikali iliyoko madarakani inawajibika kwa wananchi walioiweka madarakani, sasa inakuwaje hiyo serikali inapoacha kuheshimu mkataba baina yake na wananchi kama katiba...hapo jeshi linatakiwa lisimame upande gani...wa wananchi au serikali? Binafsi naamini kazi ya jeshi si kuilinda serikali bali nchi na wananchi wake, jeshi linatakiwa liwe rafiki na si adui wa mwananchi na ikitokea wananchi wanaamua kukatisha mkataba waliowekeana na serikali yao, chombo kama jeshi kinatakiwa kukaa kando.

Kuna namna nyingi ya kufikisha ujumbe na hasa kwa serikali iliyoundwa na chama kinachoamini kina hati miliki ya kutawala na inayojifanyia mambo hovyo with impunity kama tunavyoshuhudia. Jeshi limekimbilia kutoa tamko kwa sababu njia iliyotumika kutuma ujumbe is effective...ndio wanaoweza kuielewa kwa haraka hawa walevi wa madaraka. Mwaka 2010 ilipoonekana kuna hatari ya wananchi kuikataa CCM, jeshi lilijisahau na haraka likatoa tamko kama kitengo cha CCM la kuwatisha na kuwaonya wananchi, jeuri ambayo inaonekana ni kawaida sana kwa nchi kama zetu.

Nasema na ninarudia, hakuna kosa lolote kwa mwanajeshi kupiga picha ama na mbunge wake au mwanachi yoyote yule na kama kuna watu hawaafiki basi
ujumbe umefika.

Ur on point Mkuu!!
 
Mkuu bado hujaelewa kabisa.
Swali je ni kosa kwa Askari yule kupiga picha na wabunge wa Chadema?

Na kama kitendo kile kitaweza kutafisiriwa kuwa ni kujihusisha na siasa kwa askari basi hatua za kisheria zinapaswa kuchukuliwa lakini sio kwake tu na kwa Maafisa wa juu wa jeshi(akiwemo Kanali Ndomba ambaye kwa sasa ni mnadhimu mkuu wa JWTZ)
Vinginevyo itakuwa ni Double standard.

Kwa kuwa katazo la wanajeshi kujihusisha na siasa ni la kikatiba (Katiba ya nchi) hivi ni kwanini wanasheria wa Chadema na wengineo wasifungue kesi ya Kikatiba mahakamani kuhoji huu ujinga na hili la Lt. Gen. Ndomba likiwa kama vivid example?

Wadaiwa wakuu wawe CCM ambao katiba yao inatamka waziwazi wakuu wa mikoa na wilaya (baadhi yao ni wanajeshi kama ilivyokuwa kwa Ndomba) ni makada wao.

Hata kama nafasi ya ushindi itakuwa finyu itasaidia sana kwenye "public awareness" kuhakikisha upuuzi kama huu haujirudii tena. Hii ni muhimu sana kisiasa!
 
Back
Top Bottom