Kiranga, pamoja na yote uliyoandika, nakuomba unisome vizuri sana usikurupuke la sivyo nitakuweka kundi moja na wale wote wanaokaa na kuhoji maendeleo yaliyoletwa na wabunge wa upinzani majimboni kwao...eti waliwaahidi! Mimi si mwanachama wa Chadema na hata hao viongozi wake kama Lema nawasoma tu kwenye magazeti lakini naungana nao katika vita yao dhidi ya utawala dhaifu, mbovu, hovyo na ovu ambao haujawahi kutokea katika historia ya taifa hili linaloongozwa na mstaafu jeshini au?
Tatizo unachukulia criticism dhidi ya mediocrity kama kutounga mkono vita dhidi ya utawala dhalimu.
Mimi sipingi vita dhidi ya utawala dhalimu, sio tu naunga mkono vita dhidi ya utawala dhalimu, nataka vita hii ipigwe kwa akili zaidi, sio kwa kuwapa CCM msemo, sio kwa CHADEMA kurudia makosa ya CCM na kujikosesha moral high ground ya kuwasema CCM.
Nataka wapinzani wakisimama kuwasema CCM wanaleta siasa jeshini, wao wenyewe wapinzani wawe serious kuhusu kutochanganya siasa na jeshi. Sio CHADEMA wanawatuhumu CCM kwa kuingiza siasa jeshini huku wao wenyewe wanawa parade wanajeshi kwenye rallies zao. Tutaona hawa CHADEMA vipi? Hawa wanapenda kuchanganya siasa na jeshi, ila labda bado tu hawajapata nafasi, wakipata nafasi watakuwa CCM-B.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya yanayofanywa na chama tawala na yanayoweza kufanywa na chama pinzani
Mpaka hapo tayari ushatoa tofauti kubwa, "tawala" na "pinzani". Kama chama pinzani kinaendekeza kuchanganya siasa na jeshi kabla hakijapata madaraka ya kuwa chama tawala, kikiwa chama tawala na kupata nguvu zote za dola je? CHADEMA is shooting itself in the foot for gambling on an issue it has no advantage over, and even if it has the military's sympathy - hypothetically- that prospect is too combustive to be meaningful. You do not want a Sysiphean task of going the military way, even if you eventually win, you win over ruins. Why risk that especially if you have not reached a hopeless situation to say "this is my last resort option"? This is rather cavalier.
na hasa hapa nchini ambapo sera inatangulizwa mbele ya katiba, utii kwa chama unatangulizwa mbele ya taifa na hakuna kinachowezekana mpaka chama tawala iafiki au ibariki.
If that is the case, then give the people confidence that you are difference by doing something different, not by doing exactly what we hate in CCM. Unachukia utii wa chama kutangulizwa mbele ya utaifa? Fine and dandy, chukia hilo katika CCM, chukia wanajeshi wanaoendekeza utii kwa CCM over utaifa, lakini chukia hilohilo pia likijitokeza katika CHADEMA. Mwanajeshi yeyote akipanda mbegu ya kuligawanya jeshi letu kwa misingi ya siasa/ vyama, hilo lichukiwe, popote, CCM na CHADEMA. Sio Shimbo akitoa kauli controversial azomewe, lakini "mwanajeshi wa Lema" akitoa kauli zilizo equally controversial and divisive atetewe kwa spin zote. Dhambi ya kuligawa jeshi kisiasa ni ile ile, iwe CCM au CHADEMA. Sasa tutaichukia vipi dhambi hii CCM halafu tuipende CHADEMA? Hii si double standard pia?
Ndio maana hata kwenye utumishi serikalini sifa inachukua nafasi ya pili nyuma ya itikadi na hata katibu wa chama tawala anaweza kupata jeuri ya kutoa amri kwa kiongozi na mtumishi wa serikali na asikemewe na mamlaka husika. Ukweli ni kuwa mfumo wa Chama kimoja na chama kushika hatamu ulituathiri kiasi ambacho si rahisi kujikomboa hata baada ya miaka ishirini na ushee...inasikitisha, inaudhi na inatia hasira.
Mwanakijiji aliuliza swali hapa (I found it sarcastic) kwamba "Hivi kuna watu wanajali CCM wanafanya nini?)
Nyani Ngabu akacheka sana. Swali liko multi layered. On one level
Mwanakijiji kama ha make sense hivi. What do you mean kuna watu wanajali CCM wanafanya nini? CCM ni chama tawala of course tunatakiwa tujali wanafanya nini even if it's just so we can do better.
But on another layer, swali linabeza sana CCM kwamba kama wewe unaangalia CCM kama ndiyo standard, au hata base, basi una matatizo. Na kweli. Inaonekana kwa habari hii CHADEMA sio tu wanaangalia CCM kama base, bali wanataka ku emulate.
Mtu anaweza kusema CHADEMA wanataka kuwa kama CCM, wanataka kuwa na power na ku manipulate jeshi, sema hawana tu nguvu za dola. Why? Kwa sababu hawajapata serikali tu washaanza kujishaua na wanajeshi hivyo, tukiwapa uamiri jeshi mkuu je, na appointments zote? Watafanya nini?
Narudia tena, kama CHADEMA hawatuonyeshi anything better than CCM, wanarudia habari za kutumia jeshi katika siasa, kwa nini tufikiri kwamba watatupa kitu kipya ambacho CCM hawafanyi sasa hivi? Hatuipendi CCM, tunataka kuitoa, lakini tuitoe halafu tuweke nini? Tutoe CCM halafu tuweke CCM-B?
Hizo kanuni na sheria za wanajeshi na siasa ya Tanzania unazoziongelea ni ipi inamkataza mwanajeshi kupiga picha na mbunge wake lakini inamruhusu mwanajeshi tena mwandamizi kukitumikia chama?
Mwanajeshi hatakiwi kushiriki katika mkutano wa kisiasa katika capacity yake ya kijeshi au akiwa na magwanda, hatakiwi kupiga kampeni za kisiasa au ku express political affiliation yake publicly.
Hiyo habari ya mwanajeshi mwandamizi kukitumikia chama ni tofauti na haihusiani na hili, kwa sababu hata kama kuna mwanajeshi mwandamizi anakitumikia CCM, hilo halihalalishi hili la kumtumia mwanajeshi kisiasa. Two wrongs do not make a right. Hata kama CCM wamekosea, CHADEMA hawawezi kutumia kosa hilo la CCM ku justify makosa ya CHADEMA. CCM tunawajua ni utumbo, hapo ndo unakuta swali la Mwanakijiji kwamba hivi kuna watu wanajali CCM wanafanya nini? Mie nishawachoka CCM, nataka kuangalia kipya kutoka kwa CHADEMA, nakuta yale yale niliyoyakataa CCM ya kuchanganya siasa na jeshi, mwishowe naona CCM na CHADEMA wote sawa tu, hamna tofauti. Wote wanafanya siasa za longolongo, hamna mwenye principle.
Nitajie kiongozi yeyote awe wa umma au serikali (pamoja na jeshi) ambaye siyo kada wa chama tawala, je ndivyo katiba inavyosema?
I fail to understand the logic of this question, nikikutajia Mwananzoka Mulagimati katibu mkuu wa wizara fulani si kada wa chama, au nikikwambia viongozi wote wa jeshi na serikali ni makada wa CCM, then what? This has no bearing on CHADEMA. Kama CCM wamekosa kwa kulifanya jeshi lote liwe makada wa CCM, CHADEMA mnachotakiwa si kuiga hilo na kuingiza siasa katika jeshi ili na nyie muwe na wanajeshi wa CHADEMA. Hili litaleta Civil War. Nyie mnachotakiwa kufanya ni kuwaonyesha wananchi ubaya wa CCM, kwamba CCM inaleta siasa katika jeshi, inatuonea kwa nguvu za dola. Mnatakiwa kuwaonyesha wananchi kwamba sisi tuko tofauti, sis hatuendekezi kuligawa jeshi kisiasa, sisi tunaenda kileo zaidi, tunataka jeshi lenye utaifa zaidi. Hamjaonyesha hilo. Mmeonyesha mna uchu tu wa kuchukua nchi ili na nyie m-control jeshi na kupata kile muandishi mmoja wa alichokiita "It is our Turn To Eat Now"
je ndivyo kanuni na sheria za utumishi zinavyosema?
Kanuni na sheria za utumishi zinasema tusichanganye jeshi na siasa, period. Hazijasema kwamba kama CCM ikichanganya jeshi na siasa ni sawa kwa CHADEMA kufanya hivyo hivyo.
Ubovu wa comparison yako ya CHADEMA na CCM ni kwamba, while it may be effective to stop a CCM fanboy who is upholding CCM by eroding his moral high ground, it is not effective against me because I am not impressed by CCM in the first place. Hatuwezi kuwa caught up in the CHADEMA vs CCM duality as if there is no better. I demand better than both CHADEMA and CCM are giving Tanzanians right now. And I am more disappointed by CHADEMA than CCM simply because I did not expect much from CCM. CCM is the dinosauric behemoth, the steam engine. CHADEMA on the other hand, is the relatively new party, the hope of the hoi polloi, so why do we see CHADEMA acting like CCM? "The Young Turks" behaving like "The Old Turkeys"?
Ama na wewe unaamini kuwa wanajeshi wanaopewa ukuu wa Wilaya na Mikoa na hivyo moja kwa moja ni wajumbe (viongozi?) katika kamati za siasa wamestaafu jeshini? Okay, Samwel Ndomba alistaafu jeshini akawa Mkuu wa Wilaya/Mkoa na sasa ni Mnadhimu Mkuu jeshini! And you swallow this?
Una revolve huko huko kwenye makosa ya CCM. Mimi sitaki kusikia makosa ya CCM kutoka kwako, mimi naweza kuyaelezea makosa ya CCM vizuri zaidi ya wewe utakavyotaka kunieleza. Mimi nataka kuona CHADEMA ina ji conduct kama imejifunza kutokana na makosa ya CCM. Silioni hili.
Instead naona CHADEMA inayotaka kuwa kama CCM.
Je siku anagundulika afisa wa jeshi au polisi siyo kada wa CCM kutakalika? Huu ndio nauita utawala wa kinafiki na kiujanjaujanja na ningemtegema mtu anayedai
to look at issues with non partisan eyes, akae nao mbali kweli kweli! Kupiga picha iwe issue? Come on
Kiranga, you are better than this, hizo habari za civil war na upuuzi mwingine, tulizisahau zamani...unakumbuka kampeni dhidi ya vyama vingi mwaka 1991? Mifano tuliyokuwa tunapewa ni kama vile vita vya Rwanda na kwingineko kwamba hayo ndiyo matokeo ya demokrasia ya vyama vingi... you still go with that kind of propaganda? Interrobag!
CCM ni wanafiki na wajanja wajanja?
Let me get this now. Nyie CHADEMA mnaosema hampendi CCM kutumia jeshi katika siasa, halafu nyie wenyewe mnaenda kutumia jeshi katika siasa na kueneza kauli za kugawanya jeshi kwa misingi ya vyama vya siasa mbona mnataka kujichanganya kwa kufanya exactly kile kile mnachokikemea?
Huu si ujanjaujanja nao? Huu si unafiki huu?
Wewe umeona kupiga picha tu hapo? Hujaona kauli za huyo anayejisema kwamba ni mwanajeshi zilivyo combustive? Hujaona utetezi wa Lema? Yote hayo ni "kupiga picha tu"
Kubali tu CHADEMA wamechemka hapa, na kama wana ustaarabu waombe msamaha tu kurudisha moral high ground.
Vinginevyo watakuwa hawana tofauti na CCM.