Lema: Sikuogopa nilipoona mwanajeshi anapiga picha na mimi

Lema: Sikuogopa nilipoona mwanajeshi anapiga picha na mimi

Best na hadi hii leo hakuna aliyefukuzwa kazi kwa picha ile!!! lakini huyu aliyepiga na Lema wanataka kumshupalia wamfute kazi!!! Jeshi magamba na undumilakuwili wake!!!

Kuna haja ya kutoa definition ya kujihusisha na siasa (je ni kugombea au je kushiriki kwenye mikutano ya vyama na kama uvutiwa na maelezo usijioneshe hadharani kwa kuwa sheria inasema hivyo). In this case kwanini kwenye kambi za jeshi huwa vinawekwa vituo vya kupiga kura maana utapigaje kura bila kuwa mshabiki wa mgombea flani na sera za chama chake (ufafanunuzi hapa kwa wataalamu wa siasa maana ninatatizika kwenye tafsiri ya kujihusisha na siasa.
 
Kama kweli yule aliyepiga picha na kuhudhuria mkutano wa lema ni mwanajeshi.... Basi nadiriki kusema wazi chadema ni chama ambacho hakina jipya kabisa katika ukombozi wa nchii hii ni wanaiga na kuyatekeleza ya ccm... Nasema hivi kwa sababu chadema tunategemea wasiige ujinga au uozo wa ccm bali wenyewe wawe na vitu vipya ambavyo hata sisi wananchi tukiona na kusikia basi kweli tunaweza kusema hiki ndo chama kipya ambacho kitatuletea mambo mapya....
Chadema kila mara wamekuwa wanalalamika kuwa ccm inalifanya jeshi litumikie ccm kutokana na kuwatumia wanajeshi katika kufanya kazi za ccm ..imetolewa mifano mingi kuwa kuna wanajeshi ambao bado wako kazini wanateuliwa kuwa wakuu wa mikoa na wilaya ambao.... Kitendo cha chadema kupitia lema kumchukua na kumruhusu mwanajeshi kuhudhuria mkutano na kupiga nae picha ni wazi kabisa hata chadema nao wanatumia jeshi katika kutekeleza mikakati yao ya kisiasa jambo ambalo nibaya, na alikustahili kufanywa na chadema hata kidogo kama chama ambacho tunahitaji kupata kitu kizuri cha umoja wetu katika kutukomboa....kitendo hiki kinaendeleza fikra kama za ccm kutumia jeshi kufanikisha mambo yao ya kisiasa.... Ni hatari kwani jeshi halipaswa kutimika kama ngao ya kisiasa na kujiongezea umaarufu na kubadilishia watu fikra kuwa hata jeshi nalo linaunga mkono ...ukweli ni kitendo kibaya sana hakipaswa fanywa na chadema kabisa
shime chadema msiige ya ccm ikafika mahali tukaona nanyi ni wale wale kama ccm..


Ni mtazami wangu.... Unaweza endeleza mjadala
 
Njia utakayotumia kufikisha ujumbe inaweza kutuonyesha core principles zako ziko wapi.

Kwa mfano, mtu akim rape dada yako, na wewe ukachukizwa, ukaamua kumfikishia ujumbe kwamba unachukia rape, ukamkamata dada yake na kum rape, unaweza kufikisha ujumbe kwamba umechukia dada yako kuwa raped, lakini huwezi kusema kwamba umefikisha ujumbe kwamba unachukia rape.

Hili ndilo ilichokifanya CHADEMA.

Maoni ni kwamba CCM ime rape kanuni za kutochanganya siasa na jeshi, imetumia jeshi kisiasa na kuibana CHADEMA. Inawezekana hili lina ukweli.

CHADEMA wamefanya nini? Wametuma ujumbe kwamba hawapendi CCM kutumia jeshi kisiasa? Hasha.

Wangekuwa wanatuma ujumbe huo, wasingechanganya jeshi na siasa wao wenyewe.

Wametuma ujumbe tu kwamba hawajapenda kuonewa, na kama CCM wanatumia jeshi kisiasa, na sisi (CHADEMA) tunaweza kutumia jeshi kisiasa vile vile.

Kama wewe umem rape dada yangu, na mimi naweza kum rape dada yako vile vile.

This is despicable. Especially because CHADEMA was supposed to show us something new, give us hope after the wicked ways of CCM, and use the moral high ground they had to show us how different they are from CCM.

CHADEMA squandered this chance.

Mkizidi sana kutuambia habari za ubovu wa CCM mtaonekana kama mnataka ku set low bars for CHADEMA.

Kama kuchanganya jeshi na siasa ni kubaya CCM, basi kutabaki kuwa kubaya CHADEMA. Ukipinga hili utarudi kwenye double standards tu.

Wakifanya CM kibaya, wakifanya CHADEMA poa. Ndo nachokataa. Standard moja kwa wote.

Mkuu Kiranga uko sawa kabisa si vyema kulipiza kwa kutenda kile ambacho akistahili kutendwa!
Ila kwa CCM hii ndiyo njia sahihi kabisa! Kwani wao wakiambiwa huishia kusema ni upepo tu utapita, na kunyamaza kabisa as long as hilo jambo linawafaidisha wao kama vile tujuavyo polisi CCM n.k. Ila kwa njia hii ndogo tu ya kupiga picha na manneo yaliyo mtoka huyo askari imeleta mwangwi mkubwa ambao unawaamsha sasa, kwa kukurupuka walidhani wataibana CHADEMA, kumbe ndo nafasi nzuri ya CHADEMA kuwabana hivi.. kama ni vibaya mbona nyie hivi, mbona vile..nk. na kwahakika hapa jambo litatendeka hata kama si kwa ajili ya hili, lakini basi udhaifu uliopo katika sheria inayoambata na tukio hili utawekwa wazi, na pengine kupenyezwa ktk katiba mpya.

 
Mwanajeshi ndio ameomba kupiga picha na lema!! Soma maelezo ya lema kwanza!!
 
ndo nini hichi umeandika sasa??
povu linawatoka ccm kwa hii habari, Hakika chadema inawanyima usingizi.
 
mwanajeshi ndio ameomba kupiga picha na lema!! Soma maelezo ya lema kwanza!!

mkuu hapo ndo tatizo la uongozi ndo linajitokeza.... Nafikiri lema anafahamu kile kitendo kinaleta tafsiri gani katika jeshi..... Hapo mimi ndo ninaposema kuwa bado cdm wanaendeleza fikra za ccm kutumia jeshi kutekeleza mipango yao ya siasa kitu ambacho ni kibaya.... Na hoja yangu chadema awapaswi kuwa kama ccm....
 
ushamba unasumbua hata tundu lisu alipiga picha na tausi ikulu

dah... Ndege tausi vs jeshi jwtz???..... Kuna hoja ya msingi tukubali chadema kupitia lema wamechemka ni kama copy and pest ya ccm kitu ambacho kinafanya tuone hakuna utofauti wa kati ya cdm na ccm katika kufanya siasa....na cdm hawatakiwa kuwa hivyo kutumia jeshi kufanikisha dhima ya siasa... Hata ukimuuliza mbowe leo atakueleza kuwa kweli kijana wangu kachemka..
 
Kuna haja ya kutoa definition ya kujihusisha na siasa (je ni kugombea au je kushiriki kwenye mikutano ya vyama na kama uvutiwa na maelezo usijioneshe hadharani kwa kuwa sheria inasema hivyo). In this case kwanini kwenye kambi za jeshi huwa vinawekwa vituo vya kupiga kura maana utapigaje kura bila kuwa mshabiki wa mgombea flani na sera za chama chake (ufafanunuzi hapa kwa wataalamu wa siasa maana ninatatizika kwenye tafsiri ya kujihusisha na siasa.

EMT aliweka definition nddfu tu, ambayo ilijumuisha mwanajeshi kutoshiriki political rally akiwa na magwanda.

Kupiga kura anaenda kama raia. Kinachokatazwa si mapenzi kwa chama fulani, huwezi kuweka sheria dhidi ya mapenzi. Kinachokatazwa ni kuonyesha mapenzi yako ya kisiasa wazi ukiwa kama mwanajeshi.

Kura si issue kwa sababu kura ni siri ya mtu. Jeshi ni kama referee kwenye mpira, hata kama referee ana mapenzi na timu moja, hatutakiwi tujue anapenda timu gani, tunatakiwa tuone anachezesha kwa fair play.
 
Chadema hawajawahi kuwa na jipya lolote linaloweza kuleta maendeleo. Walijaribu kubuni sera ya majimbo kwa kuiga utaratibu uliokuwepo nchini enzi za Mwalimu, lakini wakashindwa hata kuitengeneza sera inayotekelezeka na mpaka sasa wameamua kuiacha na hawana jipya kiujumla.
 
Mkuu Kiranga uko sawa kabisa si vyema kulipiza kwa kutenda kile ambacho akistahili kutendwa!
Ila kwa CCM hii ndiyo njia sahihi kabisa! Kwani wao wakiambiwa huishia kusema ni upepo tu utapita, na kunyamaza kabisa as long as hilo jambo linawafaidisha wao kama vile tujuavyo polisi CCM n.k. Ila kwa njia hii ndogo tu ya kupiga picha na manneo yaliyo mtoka huyo askari imeleta mwangwi mkubwa ambao unawaamsha sasa, kwa kukurupuka walidhani wataibana CHADEMA, kumbe ndo nafasi nzuri ya CHADEMA kuwabana hivi.. kama ni vibaya mbona nyie hivi, mbona vile..nk. na kwahakika hapa jambo litatendeka hata kama si kwa ajili ya hili, lakini basi udhaifu uliopo katika sheria inayoambata na tukio hili utawekwa wazi, na pengine kupenyezwa ktk katiba mpya.


Basi kama hivyo mnacheza.

Maana mlitakiwa kuchukua askari wa kutosha na kuingia msituni kama Museveni.

Kwa watu serious kuuza sura na wanajeshi sio deal. Ni uvuguvugu usiotakiwa.

Mnakuwa hamtendei haki wale wasiotaka kabisa kuchanganya siasa na jeshi kama mimi, na wale wanaotaka kabisa kuanzisha jeshi la CHADEMA.

Ingieni msituni tujue mko serious mmechoshwa na shere za CCM.

Hizi habari za pichapicha nyiingi inakuwa mnajionyesha hamko serious kuingia msituni.
 
EMT aliweka definition nddfu tu, ambayo ilijumuisha mwanajeshi kutoshiriki political rally akiwa na magwanda.

Kupiga kura anaenda kama raia. Kinachokatazwa si mapenzi kwa chama fulani, huwezi kuweka sheria dhidi ya mapenzi. Kinachokatazwa ni kuonyesha mapenzi yako ya kisiasa wazi ukiwa kama mwanajeshi.

Kura si issue kwa sababu kura ni siri ya mtu. Jeshi ni kama referee kwenye mpira, hata kama referee ana mapenzi na timu moja, hatutakiwi tujue anapenda timu gani, tunatakiwa tuone anachezesha kwa fair play.

Ilikuwa ni tafakari mkuu angalau umeijibu kisayansi maana nikuwa najiuliza hili nadhani kama angeenda kama raia isingekuwa na shida sana
 
Tunashukuru kwa aliyemwandalia haya maelezo Lema!

Lema haandaliwi, ni kichwa eti unadhani kama wazee wetu wa CCM, nafurahi kwamba hata wewe yamekukuna ila tu umeshindwa kumpongeza ukaishia kusema unamshukuru aliyemwandalia
 
Uthibitisho ni kura za Jakaya pale LUGALO katika uchaguzi wa 2010. Huyu kaamua kujifunua lakini ukweli ni kuwa wengi wa wanajeshi na maaskari kwa ujumla wamechoka chama hiki na serikali yake.
 
Mkubwa naona bado un hangover ya xmas,
Hivi huyo dogo kama ni askari kweli ametekelezaje sera za cdm? . Ila kwa sababu umesema ni mtizamo wako na pengine unahitaji mjadala wa mtizamo wako utapata mengi. ila kwa kukumbusha linganisha matamshi ya Abrahaman Shimbo, na huyo dogo askari na ujue nani antumikiwa na jeshi.
 
Mkuu Kiranga uko sawa kabisa si vyema kulipiza kwa kutenda kile ambacho akistahili kutendwa!
Ila kwa CCM hii ndiyo njia sahihi kabisa! Kwani wao wakiambiwa huishia kusema ni upepo tu utapita, na kunyamaza kabisa as long as hilo jambo linawafaidisha wao kama vile tujuavyo polisi CCM n.k. Ila kwa njia hii ndogo tu ya kupiga picha na manneo yaliyo mtoka huyo askari imeleta mwangwi mkubwa ambao unawaamsha sasa, kwa kukurupuka walidhani wataibana CHADEMA, kumbe ndo nafasi nzuri ya CHADEMA kuwabana hivi.. kama ni vibaya mbona nyie hivi, mbona vile..nk. na kwahakika hapa jambo litatendeka hata kama si kwa ajili ya hili, lakini basi udhaifu uliopo katika sheria inayoambata na tukio hili utawekwa wazi, na pengine kupenyezwa ktk katiba mpya.


Tatizo ni kudhani kupiga picha ni njia ndogo na anaekomolewa ni CCM

Kupiga picha hakuishii na kupiga picha tu, kunakuna na matamko kama hili la Lema ambalo kimsingi anawasemea askari wetu (bila ya kutuambia takwimu amezipata wapi) kuwa robo tatu yao wamechoka na wanaweza kufanya kisichotarajiwa.

Huko ni kuzungumza irresponsibly kwa sababu kwanza hana takwimu hata ndogo inayomuonesha hilo, pia anapandikiza mbegu kwa askari wetu kuwa wajinasibu/washikamane kwa misingi ya vyama kwa sababu wao ni wengi

Athari ya jeshi kujigawa katika "Jeshi la CHADEMA" na "Jeshi la CCM" haitachagua CCM kama taasisi bali itaangukia kwa wananchi ambapo ni CCM, CHADEMA, CUF, NCCR na wengine wasio vyama wala wasiotaka hata kujihusisha na siasa

Kiongozi yoyote makini hawezi kuzungumza maneno ambayo yanapanda mbegu ya kuligawa jeshi au watu.

Hapa tunacheza na shilingi chooni
 
Thanx kamanda Lema kwa kuwaamsha wananchi. Hapo jirani yako Simanjiro, mkuu wa wilaya ni mjeshi (double salary). Wapo wengi tu wanachama wa CCM ndani ya jeshi. General Mboma aligombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Mbeya Vijijini. Tiba aligombea ubunge CCM, akabwagwa na Tiba. JWTZ (viongozi) wapo kwa ajili ya maslahi yao tu, ndio maana Shimbo ni Trilionea.
 
Lema ndiyo kaandika au kaandikiwa haya maelezo.

Keep going Kamanda Lema!!! Watakukoma hadi ifike 2015 hawana hamu!! Sasa ndugu yangu hata akiandaliwa au kuandikiwa kuna tabu? Mbona wa kwenu anaandikiwa na mwisho wa siku anasoma makosa na kuchomeka maneno ya uswazi!!! Hii ya Lema it is straight to the point!!! Na wote tumempata!!! Mwanasiasa mtu yeyote wa mapenzi mema ni rafiki!! Mh. Lema hawezi kukataa kupiga picha na mwanajeshi kisha eti kikatiba mwanajeshi si mwanasiasa!!! Katika kuwateua wakuu wa mikoa na wilaya-hawa si viongozi wa siasa? Msichanganye watanzania hapa!! Sasa na bado mapambano ndiyo yameanza mkuu wangu Ritz!!!! Siku mtaona jeshi limekaa wima--linasema halitaki tena!!! Si yanatokea haya lakini? tumeyasikia kwa wenzetu na kama hali itaendelea hivi tanzania hali itakuwa mbaya zaidi kwa kuwa tumeshaleta na uhasama wa udini na ukabila!! By the way, Padre Paroko amepigwa risasai Zenj!!! Sijasikia tamko!!! Eti ni majambazi walikuwa wananyemelea sadaka!! Ahhhh wapi? Nchi iko pabaya!!! Hata baadhi ya hao mnaosema wanajeshi, polisi etc are not happy!!
 
Nani asijejua askari wetu (JWTZ, Police na Mageleza) hawa wenye vyeo vidogo vidogo wana maisha magumu? - sasa wataficha mpaka lini? jamaa ame-represent kundi lao na kuomba CDM iwatetee wamechoka - mwakilishi wa kundi hili amesema "yupo tayari kwa lolote" na akaona kupiga picha na Lema itamuweka huru kifikra.
 
Back
Top Bottom