ndyoko
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,971
- 1,650
CCm na Twiga wetu.......tutakuja kuwamenya kama mayai ya kuchemshwa!!
Huyu Bibi wa kimakonde amtuaibisha sana wamakonde, looooh!
CCm na Twiga wetu.......tutakuja kuwamenya kama mayai ya kuchemshwa!!
"Nilipigiwa simu na mtu mmoja kutoka serikalini akaniambia kuna gari nyuma inanifuatilia, nilipogeuka niliona na kusimama kisha nikashuka na kubadili gari na lenyewe likaendelea kunifuatilia," Lema alidai kwamba hata juzi asubuhi alikutana nalo katika nyumba aliyofikia na alipolikaribia watu hao walishusha vioo na kumsalimu wakimwita ni MBUNGE WA ARUSHA ALIYEKO KWENYE LIKIZO.
Jinsi Mungu anavyozidi kufichua umafia wao TISS na Jk wao wanazidi kuchanganyikiwa
Unajua Ritz huwa analeta utani hadi kwenye masuala serious.
Utadhani hakumbuki kilichompata Imran Kombe mwaka 1995. Naye alikuwa akifuatiliwa hivihivi kama Lema kabla hajatandikwa risasi
Hii stori ya kitoto kabisa kwa hiyo ndio katishiwa kuuliwa kwa kusalimiawa?
Hii stori ya kitoto kabisa kwa hiyo ndio katishiwa kuuliwa kwa kusalimiawa?
"Nilipigiwa simu na mtu mmoja kutoka serikalini akaniambia kuna gari nyuma inanifuatilia, nilipogeuka niliona na kusimama kisha nikashuka na kubadili gari na lenyewe likaendelea kunifuatilia," Lema alidai kwamba hata juzi asubuhi alikutana nalo katika nyumba aliyofikia na alipolikaribia watu hao walishusha vioo na kumsalimu wakimwita ni MBUNGE WA ARUSHA ALIYEKO KWENYE LIKIZO.
Hiyo kitu Mkuu hata mimi naifahamu na kuna kipindi watu hawa wa TISS walikuwa kama 4 hivi na kwa bahati nzuri sana watatu kati yao nawafahamu fika na hata wao wananifahamu fika na hata kama wapo humu nadhani watakumbuka maneno niliyowaambia Jumamosi pale pale nje ya Southern Sun Hotel kwamba I know better the whole mission ya wao kuwepo pale.
I truly belive and in one of my contribution in the thread about Dr Ulimboka I had warned that the next victim of the Mafia style intimadation will be a Politician. The reason is simple they in power(TISS etc) intimidates those who "see things differently" from President and Prime Minister. This does not discriminate the political party but opinion. Having said that in addition to Chadema Leaders who have anounced in public that there are plans to take them to Madepwande, am worried about the safety of Filikunjombe and all those who dares to give out their opposing Opinions among CCM MPMimi nadhani umefika wakati sasa hata ukisimamishwa na Trafic barabarani kukiwa hamna wapita njia wengine usisimame maana huwezi jua wametumwa wakufanye nini.
SOMA NA HII!!
VIGOGO kadhaa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) wametajwa kuingilia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), MwanaHALISI limegundua.
Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya idara hiyo zinaeleza kuwa vigogo hao wana mahusiano ya karibu na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe.
Anayetajwa rasmi kuwa na mahusiano na Zitto ni Naibu Mkurugenzi wa TISS, Jack Zoka.
Kufichuka kwa taarifa za kuwapo uswahiba kati ya Zoka na Zitto kumekuja katika kipindi ambacho CHADEMA kimekuwa kikituhumu maofisa wa juu wa usalama wa taifa kuvuruga uchaguzi mkuu uliopita.
Aidha, kuibuka kwa tuhuma hizi kumekuja wiki moja baada ya gazeti hili kuchapisha taarifa mbalimbali za mawasiliano kati ya Zitto na Rais Jakaya Kikwete.
Baadhi ya mawasiliano hayo, ambayo Zitto ameyapeleka kwa rais, aliyapeleka pia kwa baadhi ya watuhumiwa ufisadi nchini.
Kwa mujibu wa mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa ambaye alitangazwa kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Kikwete; viongozi wa TISS walihusika, kwa kiasi kikubwa, katika kile alichoita, Kuchakachua matokeo ya uchaguzi.
MwanaHALISI limefanikiwa kupata rekodi ya mshororo wa mawasiliano kati ya Zitto na Zoka.
Kuna mwingiliano wa simu za mdomo na maandishi (sms) kutoka kwa Zitto kwenda kwa baadhi ya vigogo wa ngazi ya juu serikalini na TISS, hasa Zoka.
Nyaraka za mawasiliano zinaonyesha kuwa Zitto amekuwa akiwasiliana na naibu mtendaji mkuu wa TISS huyo zaidi ya mara tatu kwa siku.
Kwa mfano, Zitto na Zoka walifanya mawasiliano ya simu mara tisa hapo tarehe 8 Agosti. Simu iliyotumika katika mawasilino hayo, ni Na. +255756809535 ambayo hutumiwa na Zitto na +255754787550 ambayo hutumiwa na Zoka.
Wakati mawasiliano hayo yanafanyika, Zitto alikuwa katika maeneo tofauti.
Mawasiliano ya kwanza kati ya Zitto na Zoka yalipokuwa yanafanyika, simu ya Zitto ilisomeka kuwa alikuwa katika maeneo mbalimbali.
Mathalani, wakati mwingine simu ilikuwa ikisomeka kuwa yuko Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam, Kigoma Urban (Mjini), Kigoma Rural (Vijijini), Mtwara, Uwanja wa ndege-Ilala, Oyster Bay, Ukonga, Upanga na katikati ya mji.
Gazeti hili halikuweza kugundua mara moja undani wa mawasiliano ya Zitto na Zoka.
Kinachofanya baadhi ya wachunguzi wa mambo kujenga shaka ni kwamba mmoja ni mwanasiasa, tena kutoka chama kilichopo nje ya utawala; na mwingine ni mtumishi wa idara ya usalama inayolalamikiwa kukandamiza upinzani nchini.
Hata hivyo, taarifa zinaonyesha kuwa mawasiliano kati ya Zitto na Zoka yalianza kupamba moto kuanzia tarehe 6 Agosti 2010, siku moja baada ya CHADEMA kuzindua kampeni zake za urais.
Kulingana na uchunguzi, siku hiyo, tarehe 6 Agosti, simu ya Zitto ilisomeka kuwa yuko Kigoma Urban.
Katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni, CHADEMA kupitia kada wake mashuhuri, Mabere Marando, iliibuka na lundo la tuhuma dhidi ya vigogo kadhaa wa serikali, CCM na idara ya usalama wa taifa.
Mawasiliano mengine ya mara kwa mara yalifanyika tarehe 7 Agosti 2010, siku mbili tangu hotuba kali ya Jangwani. Yalianza saa 10:17 na kuendelea tena saa 10:50, saa 10:51:31, saa 11:46:13, saa 12: 14:46, saa 12:26:48 na saa 13:50: 21.
Lakini Zitto alipoulizwa kuhusu sababu ya yeye kufanya mawasiliano ya mara kwa mara na vigogo wa TISS, alisema hajui na hakumbuki lolote kuhusu kuwapo mawasiliano hayo na Zoka au mkuu yeyote wa idara hiyo.
Zitto amesema yeye, akiwa mwanasiasa na kiongozi, anazungumza na watu wengi kutoka katika taasisi na mashirika mbalimbali ndani na nje ya nchi, lakini hajui kitu kuhusu usalama wa taifa.
Alipobanwa kuhusu mazungumzo yake na Zoka, hasa yale ya 3 Novemba 2010, saa nne na dakika 56 asubuhi, siku mbili baada ya uchaguzi kumalizika, Zitto alisema, Siku hiyo nilizungumza na watu wengi sana. Siwakumbuki ni akina nani hasa.
Alisema, Hicho ndicho kipindi ambacho matokeo ya uchaguzi nchini kote yalikuwa yakizuiwa ikiwamo kwetu Kigoma. Na ukumbuke mimi nilipigwa mabomu na polisi na usalama wa taifa. Nakumbuka viongozi wengi wa vyombo vya ulinzi na usalama walinipigia simu kunijulia hali na kupata taarifa ya kilichotokea, anaeleza.
Sasa kama Zoka naye alinipigia siku hiyo sikumbuki; lakini nilipigiwa na wengiNaomba uniambie kitu, hivi mnachokitafuta hasa ni nini? aliuliza.
Katika njia ya kujitetea, Zitto aliuliza, Mwanasiasa kuongea na wakuu wa vyombo vya usalama ni kosa? Maana, hata kama ningekuwa nimezungumza naye, kosa langu liko wapi? alieleza mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini.
Alipoelezwa kuwa haoni hiyo ni hujuma dhidi ya chama chake kwa kuzungumza na viongozi wa TISS na kile ambacho amekuwa akikizungumza kikiwa hakifahamiki kwa viongozi wake, Zitto alisema, Sijawahi kukihujumu chama changu mahali popote, siku yoyote.
Jitihada za gazeti hili kuzungumza na Zoka hazikufanikiwa katika kipindi chote
cha mwishoni mwa wiki, kwa vile kila alipopigiwa, simu yake ya mkononi ilikuwa haipokelewi.
Hata ujumbe mfupi wa maneno uliotumwa kwenye simu yake saa 2:53 asubuhi ya Jumapili; ukieleza sababu za gazeti kuzungumza naye, haukujibiwa.
Aidha, tarehe 2 Novemba, siku moja baada ya kuzungumza na Zitto, Zoka alinukuliwa akikana madai ya Dk. Slaa, kuwa TISS imesaidia kuvuruga uchaguzi.
Katika taarifa yake aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari, ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Zoka alisema, Dk. Slaa amekuwa akidanganywa na watu wanaojiita maofisa wa usalama wa taifa.
Hata hivyo, kuna meseji mbalimbali kuhusu udini na uamuzi wa CHADEMA kususia hotuba ya rais Kikwete ambazo zilitumwa na Zitto kwa baadhi ya wabunge wa CHADEMA ambazo zinadaiwa kuandaliwa na idara ya usalama wataifa.
Ujumbe huo unadaiwa kuandaliwa kwa ustadi mkubwa katika kukuza suala la udini na kuleta mtafaruki katika chama.[/COLOR]
"Nilipigiwa simu na mtu mmoja kutoka serikalini akaniambia kuna gari nyuma inanifuatilia.
Nilipogeuka niliona na kusimama kisha nikashuka na kubadili gari na lenyewe likaendelea kunifuatilia," Lema alidai kwamba hata juzi asubuhi alikutana nalo katika nyumba aliyofikia.
Na alipolikaribia watu hao walishusha vioo na kumsalimu wakimwita ni MBUNGE WA ARUSHA ALIYEKO KWENYE LIKIZO.
Kwani Ritz utakubali sasa si mpaka uone ulimboka tuu, lakini mwisho wenu ni karibu ngojea tu!!!!!Hii stori ya kitoto kabisa kwa hiyo ndio katishiwa kuuliwa kwa kusalimiawa?
Ritz yuko sawa,hiyo stori ni ya kuwaambia mazuzu sio watu wenye akili....eti nimepigiwa simu..... ku si bullshiiiiiiit!!!!
Wakina Jack Nzoka wanatumia mtindo wa kizamani kuwafuatilia viongozi wa CDM ambao ni wajanja mara elfu moja kuliko wao ambao wamesoma Urusi na Al-haramain