Lema: Nilipigiwa Simu na mtu kutoka serikalini

Lema: Nilipigiwa Simu na mtu kutoka serikalini

Akina ritz and the like ni kitengo cha propaganda cha chama cha mabwepande aka sisiemu.
 
ulisWewe hawahi kusema Lema ni jambazi, nani anajuwa wewe ni nani?Kombe bosi wao waliyekuwa wakimfahamu pale Moshi walimwita jambazi...

Kutokana na michango yako humu ndani, wewe ni fisadi kubwa.

Hapo kwenye red nadhani mie utanionea bure

Bwana ZOMBE alizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania hapo jana. Aidha zombe amedai kuwa wakati alipokuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa DSM alipata taarifa kuwa Bwana LEMA ana mtandao wa wizi wa magari kutoka Tanzania na kuyapeleka Kenya.
 
Kajipanga kupoteza mada hawezi kuamini hata kama anafuatiliwa hasa Bwn Lema anaona ni sawa tuu, au analipwa kupotezea mada watu wasishtuke waone ni normal, kazi nzuri Ritz hadi uone Dr Uli !!!!

Mkuu JF sio mali ya Chadema wewe unataka kila mtu humu Jamvini asifie Chadema hilo aliwezekani.
 
Hofstede na Wana JF,
Umeelezea vizuri sana, nakupongeza kwa hili, sijui hizi Tamaa za kujilimbikizia Mali za ubadhilifu tunatoa wapi.Tu
natakiwa kujifunza kutoka kwa wenzetu.
My Take: Ukimwacha Mungu naye anakuacha, Malipo ni hapa hapa Duniani
Nawakilisha







Nafikiri CCM wanajaribu kupima kina cha maji. Historia inaonesha kuwa uongozi wowote unaposhindwa hoja huanza vitisho na ukandamizaji ambao polepole huongeza ujasiri miongoni mwa wananchi na kujikuta ukigeukwa na kuangushwa. Sasa CCM wasitumie vibaya advantage ya kuwa na serikali inayowapatia authority ya kutoa amri kwa vyombo vya dola. Na vyombo vya dola pia ambao ninaamini kuna wataalam wazuri na wazalendo wanatakiwa kujua kuwa unapokubali kutekeleza amri haramu ya mtawala basi na wewe unakuwa ni sehemu ya wahalifu hao. Siku mtawala akianguka na wewe pia unaanguka na taaluma yako.

Haihitaji kutekeleza amri haramu ili kulinda kazi yako ni bora ujiuzulu na kukaa pembeni kuliko kuwa sehemu ya uhalifu. Unaweza ua mtu lakini huwezi ua mawazo. Na kitu cha kujifunza ni kuwa vitisho havikufanyi upendwe au uonekane uendelee kutawala, bali vitisho vinakufanya uongeze chuki kati ya wananchi na serikali yako. Walikuwepo kina Sadam Hussein, Gaddafi, Mobutu, Idi Amini Dada et al na wote hao leo hii wamepita na tawala zao zimekuwa historia.

Tanzania ni yetu sote hivyo tuifanye nchi salama ya wote kuishi kwa amani bila woga, Ukimu-eliminate mtu anayepingana na wewe basi ujue unaandaa watu laki wanaopingana na wewe na hivyo kujikuta unaweka maisha ya watu wanakuzunguuka na wanaohusiana na wewe katika hali ya wasiwasi wa avenge. Hakuna mtu wala chama chenye haki miliki ya uongozi wa nchi hivyo tukubali kuwa kama wananchi wakisema sasa basi iwe basi, wewe na wanaokuzunguuka chukueni majembe mkalime msubiri next time mje kuwashawishi wananchi tena.

Hizi operation za giza zinzoandaliwa hazitafanikiwa kamwe, zinaweza fanikiwa kuzima wahusika lakini hazitafanikiwa kuzima fikra za mabadiliko, kwani hata kama watu watakuwa wanaishi kwa woga bado hawakuoni wewe kuwa ni kiongozi wao. Kuna maana gani ya kuwa kiongozi bila ya kupata ushirikiano toka kwa unaowaongoza?. kama lengo ni kuongoza si kutunisha tumbo lako?.

I hate haya mawazo ya targeted killing kwa kuwa tu watu fulani wanatishia ulaji wetu. Cha kujiuliza na kufikiri ni kuwa ni rahisi sana kuanzisha uvunjifu wa amani ila ni vigumu sana kuirudisha amani hiyo, kwani amani hulka na tabia inayojijenga kwenye akili isiyokuwa na wazo la kulipa kisasi kwa sababu imeonewa. Vyombo vya dola vitumike kulinda wananchi na mali zao na kulinda nchi na si rungu la kujiimarishia madaraka ambayo by nature hutolewa na wananchi. Unapowaingiza wanausalama wengi katika criminal activities maana yake ni kwamba wanausalama hawa wanajiona kuwa guilty unless someone anayewalinda aendelee kutawala. Tunataka Tanzania ambayo CCM ikiondoka madarakani basi wakuu wa usalama kama public servants waendelee kuwa salama katika nafasi zao, kwani chaguzi hubadili viongozi wa siasa tu na si watekelezaji ambao wamekuwa trained kwa pesa nyingi za walipa kodi.

Tabia ya wanasiasa kuwapaka uchafu wao wataalam kwa sababu tu wanadhani kwa kufanya hivyo kutalinda nafasi zao ni mbaya na haifai. Tunataka Tanzania yenye uwezo wa kutransion power toka chama kimoja kwenda kingine kwa amani na utulivu kwani lengo la siasa si kuvunja amani bali ni kugonganisha mawazo positive yenye nia moja ya kuendeleza nchi.

Shame on those who are abusing their political authorities!, hata kama mna pesa uswisi za kukimbilia baada ya kutuunguzia nchi yetu kwa tamaa zenu binafsi, ila mjue kuwa popte mtakapokuwa popote pale duniani mtapatikana tu.

Mungu Ibariki Tanzania!
 
Ritz yuko sawa,hiyo stori ni ya kuwaambia mazuzu sio watu wenye akili....eti nimepigiwa simu..... ku si bullshiiiiiiit!!!!

Hacha kutafuta cheap popularity mtoto wa kiume kwa kumkandia Lema umaaru jamii forums hauji kwa style hiyo
 
Hii inanikumbusha ile ajari iliyomkosa Mh. Zitto Zuberi Kabwe ikampata masikini Mh. mmoja wa CCM.
Mungu amlaze pema Peponi AMINA.
 
Hapo kwenye red nadhani mie utanionea bure

Bwana ZOMBE alizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania hapo jana. Aidha zombe amedai kuwa wakati alipokuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa DSM alipata taarifa kuwa Bwana LEMA ana mtandao wa wizi wa magari kutoka Tanzania na kuyapeleka Kenya.
Umeuona udhaifu wa serikali wanawajua majambazi alafu wanawaacha hadi wanakuwa waheshimiwa. UPUUUUUZi!.
 
Tatizo la kwanza... kuuwa unaweza lakini huwezi kufufua mtu
Tatizo la pili ........ kuuwa unaweza lakini hata wewe utakufa pia
Tatizo la tatu ....... kuuwa waweza, lakini unapingana na Mungu anayeruzuku uhai. Hivyo unakuwa aduwi wa Mungu moja kwa moja
Tatizo la nne ........ Kuuwa si njia ya kuleta majibu ya masuali magumu..bali ni kusababisha hali na matokeo usiyoyafahamu

Mifano ya zamani:
Daudi aliua askari wake Uriah ...Mungu alimwambia na yeye atakufa !!
Sauli alitaka kumwua Daud, kwa sababu hizi hizi za kushindwa kutawala vizuri taifa na kumwona Daudi kama threat.. hatimae Mungu alimwangamiza Sauli

Mifano ya siku hizi:
Gadaf alinuwia kuangamiza wapinzani wake, badala yake yeye alipoteza roho yake
Samuel Doe aliuwa ili kutawala nchi yake ... yeye pia aliuawa kinyama pia
Karume alizowea kuuwa wapinzani wake, yeye naye aliuawa kinyama

ONYO
Kila auwaye kwa upanga, atakufa kwa upanga. Njia nzuri ya kuwashinda wapinzani wako ni kutoa uongozi mzuri na watu wako wakakupenda. Njia ya kuua mara nyingi ina matokeo mabaya sana kwa kila taifa ..

Mwenye sikio asikie.
 
Na mimi juzi nilikuwa na drive kugeuka nyuma nakata kona naona gari nyeusi tinted Fortuner nayo imekata kona dah lazima itakuwa usalama wa Taifa.

ulipigiwa simu na mtu wa kwenye system?
 
Hapo kwenye red nadhani mie utanionea bure

Bwana ZOMBE alizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania hapo jana. Aidha zombe amedai kuwa wakati alipokuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa DSM alipata taarifa kuwa Bwana LEMA ana mtandao wa wizi wa magari kutoka Tanzania na kuyapeleka Kenya.
Since unatumia jina bandia, sikujui wewe ni nani, sasa tofauti ikwapi ukisema si wewe umesema ni Zombe?Useme wewe, aseme Zombe,mi sioni tofauti.

Ninachojuwa ni kwamba hata Kombe alipigwa risasi wakisema ni jambazi, kwahiyo kuwaita watu majambazi si dalili nzuri kwa anayeitwa.
 
Unaweza ukamuua mwanamageuzi lakini huwezi kuua ideas za mageuzi
 
Hii stori ya kitoto kabisa kwa hiyo ndio katishiwa kuuliwa kwa kusalimiawa?
Inawezekana ulikuwa mtego ili Lema awajibu hao jamaa kwa risasi(assuming Lema is always armed) so a shoot out would ensue. Lema might be armed but would be no match for the instigators who definitely were wearing bullet proof vests
 
Haya ndio matatizo ya ushamba.hapa dar ajue kuna msongamano wa magari sio km arusha unaweza kutembea km nzima peke ako afu hoja kuwa alipigiwa simu na mtu wa serikali sisi tutamwaminije.hatudanganyiki
 
Usikurupuke ka gurue pori, shirikisha ubongo japo kwa 1.5%.....

kwa kuongeza mambo mapya ambayo hujawahi kukutana nayo lazima yatiliwe shaka. kumfuatilia mtu nyuma kwa gari ni aina ya ujasusi uliokomaa
 
hata kudanganya huwezi. serikali.hiyohiyo ikuwinde halafu serikali hiyohiyo ukutaarifu kuwa kuna gari inakufatilia kwa nyuma..hujapona lema rudi hospital
 
Yaani wewe ulivyokuwa na upeo mdogo unadhani wote tupo hivyo siwezi kuamini stori ya kitoto kama hii...

Watu wanakufa wewe unaita stori ya kitoto!! Ulitaka akuambie kesho unatahiriwa ndiyo ujue ni stori ya watu wazima?
 
Back
Top Bottom