chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 12,569
- 21,683
Lissu mroho wa madarakaGodbless Lema ameandika ukurasani X
Halafu wakitoka hapo wanasema CCM inatoa Fomu Moja
Siasa za Tanzania pasua kichwa sana aiseee
====
Nimeona andiko la BOB Wangwe na maandiko mengine ya watu wengi pamoja na ushauri wake.
Jibu langu kwenu ni hili ,tukiwa Arusha mahali fulani kwenye mazungumzo yetu ambapo nilikuwepo pamoja na Kamanda Wenje, Heche,Msigwa na Mkti F.Mbowe, Mh Lissu aliongea maneno haya “ Nanukuu “ Kaka , Mwenyekiti , ulibeba chupa ya damu nisife wkt nimeshambuliwa kutoka Dodoma ukiwa umesimama kwenye ndege mpaka Nairobi, na ulikaa Nairobi na wenzako hawa muda wote wa matibabu yangu , siwezi kuchukua fomu utakayogusa kwenye Chama hiki,tusiruhusu wapambe watuharibie CHAMA “.
Maneno haya niliyasikia Mimi, Heche, Msigwa, Wenje na Mwenyekiti Mbowe.Hakuna vita kwenye nafasi ya Urais CHADEMA isipokuwa kuna wapambe wajinga na CCM haswa ktk muelekeo wa siasa 2024/2025.
View attachment 2981595