Lema: Nikimuona mtoto wa Waziri Mkuu Majaliwa au wa Rais Mwinyi anaendesha Bodaboda ndipo nitaomba radhi

Lema kaongea kitu cha kweli.

Invasione ya Bodaboda Africa imeua sanaaa.
Imejeruhi mnoo.
Na mpaka sasa nafikiri ndo inaongoza kwa vifo na ulemavu Barani Africa.

Ispokuwa ni jinsi anavyo pitisha hoja yake.
 
Ndo maana nikakwambia ni utofauti hata wewe unaweza kuingia kweny system au kuwa na kipato kikubwa na wanao wakafika mbali...Hata marekani sio wote wanaokula keki ya taifa kuwa na akili.

Hao chadema na CCM ndo walewale hawana jipya pambania familia yako
 
Mkuu nchi ina wajinga sana, wao watotobwao wako hadi Umoja wa Matifa huko New York, tena wameajiriwa kwa Vimemo, huku watoto wa Choka mbaya wakiambiwa waende Ualimu na TOYO
Zile scholarship za kwenda kusoma like USA ,Canada France,Sweden , Amsterdam yaani zile nchi nzurinzuri Ni watt wao ndio wanaoenda
 
Kama nchi unadhani kuwaingiza vijana hawa wa miaka 15 hadi 30 kwenye kazi ya uboda boda itaisaidia nchi kupiga hatua
 
Sorry bro mimi nimeajiriwa nafanya kampuni ya kilimo, ni vile tu tumezoea shida na kuona ni kawaida. Ila hiyo kazi ya boda boda hapana kwakweli watu tubadili mitazamo pengine.
Kuna kuna ku adapt habits and neuropathway za umasikini unaona uko sahihi. Jamani boda risk Ni kubwa kwa maisha yake yaani Sana mno. Safety Ni ndogo.


Kuna kuzoea kupanda daladala unaona uko sahihi ama kula ugali wali viazi mahindi choma chemshwa makande uji wa mahindi ugali wa mahindi wewe unajipa comfortableness kuwa uko sawa. Ila siku ukionja utamu wa dunia utaona Kama ulikuwa gerezani.


Hivi hamjui Kuna watu wanazoea gerezani hata wakitoka wanaomba Tena kurudi.


Yaani Kuna kitu kinaitwa subconscious mind is very powerful than you combined millions times.
 
Za undergraduate degree Ila Masters nadhani inakuwa Cha wote.
Nina ndugu zangu wawili mmoja algeria na mwingine anasoma USA na sio watoto wa vigogo wameenda kusoma degree baada ya kufaulu vizuri kwa kuwa gpa kubwa
 
Sasa wewe unataka wafanye kazi gani?
Hapo sasa ndio tunaletwa pamoja dhidi ya ujumbe anao tupa Lema, kwamba serikali imeshindwa kurahisisha fursa zilizopo ili watu wake wafanye kazi zenye kuwahakikishia usalama wao na zenye tija.. Badala yake wao wanajinufaisha na vizazi vyao halafu nyinyi wanawaaambia eti boda boda ni maisha.
 
Lema yuko sahihi by the way, vijana wetu tunaumizwa sana na bodaboda lakini kwa nchi kama hizo za africa hasa huko Tanzania ni shida vile vile vijana wetu kutafuta kazi mbadala ambayo haijuulikani iko wapi wala utaipatje
 
Haya alitakiwa sasa akawaeleze Mh Majaliwa na Mh Mwinyi. Kuwaeleza bodaboda wenyewe ni kuwakashifu.
 
Unamwambia yeye apambanie maisha ila wakati anapambania anatozwa kodi halafu hiyo kodi inawanemeesha watoto wa wengine aisee hii haiko Sawa unaonaje
 
Wapo bodaboda wametoboa na wengine wanalisha familia zao hivi nikuulize Kati ya bodaboda na yule cashier wa Mlimani city s yupi anaingiza hela zaidi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…