Lema: Nikimuona mtoto wa Waziri Mkuu Majaliwa au wa Rais Mwinyi anaendesha Bodaboda ndipo nitaomba radhi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,904
141,855
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Lema amesema endapo atamuona mtoto wa Waziri mkuu mh Majaliwa au mtoto wa Rais Mwinyi anaendesha Bodaboda ndipo ataomba radhi.

Lema amesisitiza Kuwa Bodaboda ni Kazi isiyofaa inayouwa na kuwapa ulemavu Vijana Wengi.

Lema amenena haya kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Mlale Unono!

======

"Nikimuona mtoto wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa au Mtoto wa Rais Mwinyi anaendesha bodaboda na kudai ni kazi ya heri nitaomba radhi. Bodaboda ni kazi ya mateso,imeumiza watu na kujeruhi watu wengi.Acheni kudanganywa na Serikali iliyo kosa mbinu za kuokoa maisha yenu. Umasikini sio sifa."

Screenshot 2023-03-07 at 04-01-38 Godbless E.J. Lema on Twitter.png
 
Huku ndiko kunaitwa kujazana ujinga, haiwezekani watoto wote wazazi wao wakawa na Uwezo wa shule za medium!, ACHA KUJAZA WATU UPUMBAVU!,

Wameshaitana kama mchwa waje watafune ruzuku yao taratibu, pia mkikosa la kuongea si lazima uongee!
Jifunzeni hekima kutoka CCM.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Lema amesema endapo atamuona mtoto wa Waziri mkuu mh Majaliwa au mtoto wa Rais Mwinyi anaendesha Bodaboda ndipo ataomba radhi...
Hiyo hoja kama kweli ameitoa basi amedhihirisha yeye Lema ana upeo mdogo sana wa kufikiri. Lakini sishangai maana hata mwenzake John Heche niliyesoma nae Shahada ya Elimu na mkewe ambaye ni Mwalimu pale Nyabulogoya Sekondari Kata ya Nyegezi Jijini Mwanza eti nae anauponda Ualimu kisa tu aliwahi kuwa Mbunge! Watu Hawa ni washamba kweri kweri!!
 
Hiyo hoja kama kweli ameitoa basi amedhihirisha yeye Lema ana upeo mdogo sana wa kufikiri. Lakini sishangai maana hata mwezake John Heche niliyesoma nae Shahada ya Elimu na mkewe ambaye ni Mwalimu pale Nyabulogoya Sekondari Kata ya Nyegezi Jijini Mwanza eti nae anauponda Ualimu kisa tu aliwahi kuwa Mbunge! Watu Hawa ni washamba kweri kweri!!
Ualimu huu uticha?
 
Wakuu achana na Lema nafikiri point yake angeiweka kwa namna ambayo isingeleta sintofahamu.
 
Back
Top Bottom