Lema asitisha wanafunzi kuendelea kusoma Korona Sec

Lema asitisha wanafunzi kuendelea kusoma Korona Sec

Je, Lema ana mamlaka ya kisheria ya kuamuru shule ifungwe? je, jambo hili limejadiliwa kwenye council?

Je, wazazi wa watoto hawa wametimiza vipi jukumu la kuhakikisha watoto wao wanapata elimu? Mimi nilidhani Lema ataamrisha halmashauri ianzishe utaratibu wa kuwacharge wazazi wa watoto hawa nauli ya kifordi ili kiwe kinacommute kuwapeleka shule.

Ukijengewa shule halafu bado tena unalalamika kuwa huwezi kufika huko shuleni kwa sababu ni mbali, inakuwa too much complain!

Sio kila mtu anakaa katikati ya mji, hata shule ikiwa katikati ya jiji, kuna wanafunzi wanaotoka pembezoni wanakuja, of course if they see the importance of going to school...
1. Watoto walikuwa hawasomi japo wanaenda shule.

2. Lema hakufanya aliyoyafanya peke yake, alikuwa na Mkuu wa shule, Afisa Elimu, Diwani na Mwakilishi wa Mkurugenzi.

3. Hatua aliyochukua Lema, inasaidia watoto wasomee katika shule nyingine wakati matatizo ya shule hiyo yanatafutiwa ufumbuzi.

4. Kumbuka hii ni shule ya serikali na Halmashauri ilikuwa haijali, na ilikuwa inaona bora muda upite japo watoto hawasomi, Lema anataka kuhakikisha wanapata elimu bora.

Hapo chini ni jopo lililomsaidia Lema kuamua

View attachment 80592
Afisa elimu, Diwani, Mbunge, kaimu mkurugenzi na mwalimu mkuu wa shule ya Korona.
Kuna mambo yanahitaji maamuzi ya haraka, na mojawapo ndio hili. Hivi kama unaona jengo linashika moto katika hatua za kwanza, unaamua kuitisha kikao ili kujadili tuushughulikieje moto, badala ya kuuzima?

Hongera Lema, umeonesha mfano wa kufanya maamuzi magumu.
 
Cha msingi asimamie hilo zoezi la kuwapatia shule kwa muda huu ili wasome, pia waziri wa elimu aje atuambie hiyo shule ilisajiliwaje?
 
I think this is the right decision whatsoever.
Mbunge wa Arusha mjini Mh. Godbless Lema leo amesitisha wanafunzi wa shule ya Korona Secondari iliyoko kata Ongutoto wilaya ya Arusha. Korona inayopaswa kuwa na wanafunzi 1,200 lakini kwa sasa ni wanafunzi 139 tu wanaofika shuleni hapo na tuliowakuta ni 118 tu, huku kidato cha kwanza wakiwa 19 badala ya 400.

Lema alifikia maamzi hayo kwa kile alicho kiita ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kutembea km 13 huku wakikosa masomo, wanafunzi hao wakitoa ushuuda walisema wamekuwa wakija shuleni na kurudi bila kusoma,Walimu hufika saa sita na kuondoka saa saba na nusu.

Wanafunzi hufika saa tano na kuondoka saa nane,Wanafunzi hawafundishwi na wakifundishwa hufundishwa kipindi kimoja cha dakika 30.

Wazazi wanatoa michango kiasi cha TZS 72,000/= ya chakula kwa watoto wao lakini hawajawahi kupata chakula chochote kwenye shule hiyo, 32,000/= ya sare lakini hawajawahi kupewa sare, 5,000/= ya vitambulisho lakini hawajawahi kupewa vitambulisho.

Watoto wanakunywa maji ya mto Kijenge ambao kwa wanyeji wa kijenge/Arusha wana jua namna ulivyo mchafu.

Hali hiyo imepelekea watoto 98 kuhamishwa na kupelekwa kwenye shule zilizoko manispaa ya jiji la Arusha wakati wizara walishasema shule hizo zimejaa lakini baadhi ya wazazi walitoa ushuuda kuwa kuna rushwa kubwa inayofanyika katika kuhamisha watoto kwani kama huna TZS 200.000/= huwezi kumhamisha mtoto ndiyo maana waliobaki ni watoto yatima ambao wazazi wao ama hawana uwezo huo wa kutoa kiasi hicho cha pesa au hawa thamini elimu ya watoto wao.

Baada ya Lema kusitisha mwanafunzi hao kwenda kusoma Korona alimkabidhi Diwani wa kata hiyo kwenda na watoto kwenye ofisi yake na atakuwa anakaa nao hapo mpaka siku watakapo patiwa shule za kuhamia ambapo Lema alishauri kuwa kila shule iliyoko kwenye jimbo hilo ichukue wanafunzi angalau watano tu, kwa muda ambao shule hiyo itakuwa ikifanyiwa marekebisho na kubadilishwa iwe boarding kitu ambacho ilionekana ndiyo suruhu ya kudumu, mbunge huyo aliahidi kutoa tofari 3000, solar panel, na pampu ya kuvutia maji na atatoa iwapo wanao husika wataonyesha nia...
View attachment 80588
View attachment 80592
Afisa elimu, Diwani, Mbunge, kaimu mkurugenzi na mwalimu mkuu wa shule ya Korona.
View attachment 80594
Wanafunzi wa Korona Secondari wakishangilia maamzi ya mbunge wa Arusha mjini ya kusitisha masomo kwenye shule hiyo..
 
Nadhani kwa kuanzia hiyo ni hatua nzuri lakini next; watoro waende wapi wakati muda wa shule unaendelea. Je fedha zao walizolipa ambazo hazijatumika watazipataje ili wakaanze upya mahali pengine?? Je waliosababisha haya wawajibishwe vipi (au hawalipwi mshahara?. Please find out) ???? Zaidi ya initiatives za mbunge bila kujali itikadi, Mamlaka husika kwa ajili ya final solution and right action ni ipi??? Kuna maswali mengi kuliko majibu
 
Hii ni shule ya serikali au ya mtu binafsi? Kama Lema amesitisha wanafunzi, solution yake nini? Anawahamisha kwenda shule nyingine au ndo imetoka hiyo? Mleta mada fafanua hapa!!!

Tiba

Soma mada nzima! Acha uvivu
 
Hii ni shule ya serikali au ya mtu binafsi? Kama Lema amesitisha wanafunzi, solution yake nini? Anawahamisha kwenda shule nyingine au ndo imetoka hiyo? Mleta mada fafanua hapa!!!

Tiba

Soma mada vizuri. keshasema kila shule kwenye jimbo lake ichukue angalau wanafunzi 5.
 
Hilo mtoa mada kaliweka vizuri kabisa, wataendelea kukaa ofcn kwake mpaka watakapopata shue za kuhamia "Baada ya Lema kusitisha mwanafunzi hao kwenda kusoma Korona alimkabidhi Diwani wa kata hiyo kwenda na watoto kwenye ofisi yake na atakuwa anakaa nao hapo mpaka siku watakapo patiwa shule za kuhamia ambapo Lema alishauri kuwa kila shule iliyoko kwenye jimbo hilo ichukue wanafunzi angalau watano tu"

jamani jifunzeni kusoma na kuelewa.

Mkuu, nimekwisha toa maelezo juu ya hii kwa mtu mwingine aliyenishambulia. Ukweli ni kwamba mleta mada hapo awali hakueleza kwamba watoto watakwenda wapi na wala picha hazikuwepo ndio maana nilihoji hivyo. Aliongezea hayo maelezo baadae sana labda leo kwa kuwa hii post ilitoka jana jioni.

Ni matumaini yangu umenielewa!!!

Tiba
 
Soma mada vizuri. keshasema kila shule kwenye jimbo lake ichukue angalau wanafunzi 5.

jamani jifunzeni kusoma na kuelewa.

Mkuu, nimekwisha toa maelezo juu ya hii kwa mtu mwingine aliyenishambulia. Ukweli ni kwamba mleta mada hapo awali hakueleza kwamba watoto watakwenda wapi na wala picha hazikuwepo ndio maana nilihoji hivyo. Aliongezea hayo maelezo baadae sana labda leo kwa kuwa hii post ilitoka jana jioni.

Ni matumaini yangu umenielewa!!!

Tiba
 
Lema na siasa zake za Arusha ni vichekesho tu.

Kinachokuchekesha ni nini hapo? badala ya kujihisi maumivu juu ya hali hiyo inayotokea wewe unasema ni kichekesho.
 
Hili lijamaa kweli linajua kufanya maamuzi magumu. Big up kamanda!!!
 
jamani jifunzeni kusoma na kuelewa.

Mkuu, nimekwisha toa maelezo juu ya hii kwa mtu mwingine aliyenishambulia. Ukweli ni kwamba mleta mada hapo awali hakueleza kwamba watoto watakwenda wapi na wala picha hazikuwepo ndio maana nilihoji hivyo. Aliongezea hayo maelezo baadae sana labda leo kwa kuwa hii post ilitoka jana jioni.

Ni matumaini yangu umenielewa!!!

Tiba

Nimekuelewa Mkuu!!!!!....Nafuta kauli.
 
hee naangalia mkuu wa wilaya kupitaa tbc anasema lema hana mamlaka ya kuzuia watoto wasiende shule
 
Nilikuwepo kwenye ziara hiyo ya mbunge alipotembelea sekondari ya korona hapa mjini arusha.
Afisa elimu alikuwepo, mkuu wa shule, diwani, kaimu mkurugenzi wa jiji. Akaamuliza mkurugenzi kama baraza la madiwani lilishaamua ijengwe bweni kabla ya wanafunzi hawajafungua shule mwaka wa masomo 2013 ina maana mmedharau baraza na mmewapuuza watoto hawa ambao wanateseka kwa kutembea umbali mrefu wa namna hii.
Wazazi walikuwepo ambao walitaja matatizo mengi ambao yalipafanya hapo pasiitwe shule, mzazi mmoja akasema shule ilifunguliwa na makamu wa rais mhe mohamed bilal na kwenye hotuba waliahidi kuijenga ndani ya miezi sita kuimaliza na kuwa na mabweni, kitu ambacho hakikufanywa.

Lema akaamuru shule ifungwe kwa miezi mitatu, watoto wapelekwe kwa muda kwenye shule zilizopo jijini, nyumba za walimu zijengwe ili wawepo shuleni, mabweni yajengwe na walimu waajiriwe waletwe shuleni, kisima cha maji kichimbwe na yeye akawa ametoa mtambo wa solar kwa ajili ya umeme.

Nilifurahi afisa elimu alipomwambia, asifunge shule mpaka aandike barua kwa afisa wa elimu wa mkoa na baraza la madiwani liamue, akamjibu, "Endelea na taratibu zote za kufunga lakini watoto hawa watafutiwe mahali pa kusoma maana hapa wanakuja kukua na wanacheza tu kwa hiyo hatuwezi kuwatesa watoto kwa taratibu ambazo zinaweza kuwa na majibu mbadala".

Haya ndio maamuzi magumu.
 
Huyo Ndiye Lema, taratibu zipi, mambo yako wazi sasa taratibu za nini? Heko Mh G. Lema chapa kazi mkuu.
 
shule za namna hiyo ziko nyingi nchini tena nyingi zazo ziko na hali mbaya, lakini wahusika wala hawataki kuona matatizo yaliyopo.
Nampongeza sana mh Lema, kwa uamuzi aliouchukua......HII NDO AINA YA VIONGOZI TUNAOWATAKA AMBAO WANAGUSWA NA MATATIZO YA WANANCHI WAO KWA DHATI NA WASIOSITA KUCHUKUA HATUA KWA MASLAHI YAO!
 
mbunge hana mamlaka ya kufunga shule wala hao maofisa ulio wataja nadhan tatizo la mleta mada analeta ushabiki wa kisiasa .wakati anajua ukweli wa jambo lenyewe ila sababu alizo toa za kufunga shule ni vivid lazima ingekuwa hivyo tu
 
Back
Top Bottom