Mkuu
Ritz, bila kujali ikadi za kisiasa, Lema hakuwa na mamlaka ya kuifungia shule ile. Hili lazima lieleweke. Pia, Mkuu wa Wilaya kuifungua shule ilikuwa lazima, kulingana na ile concept ya "Who does What".
Lakini, kimantiki, Lema na Mkuu wa Wilaya, na Afisa elimu, wanapaswa kuangalia namna bora ya kuwasaida wanafunzi wale. Walai nakwambia
Ritz, ukiona wanafunzi wa shule za kata wanavyosoma, haki utalia!. Kuna shule moja niliienda kuitembelea, ipo Sengerema, mita chache baada ya kuvuka kivuko cha Kamanga Mwanza, Walimu walikuwa Wawili, Mwanafunzi lazima atembee karibia saa nzima kufika shuleni, maji maeneo hayo hakuna, umeme ndo usisema, vyoo vilikuwa hata havijajengwa, kiufupi,
Ritz wewe ungesoma shule kama hizo, tusingekuwa wote katika jukwaa hili (nina imani umenielewa!). Hata mtoto wako sidhani kama utamruhusu asome shule kama hizo!.
Hii lazimisha lazimisha ya kufungua hule za kata, bila kaundaa miundombinu na walimu wa kufundisha katika shule hizi, hakika Lowassa na Serikali yetu walichemka mbaya, ndo maana hivi sasa Vijana wengi wanapata
''bora elimu na sii elimu bora''!