Lema asitisha wanafunzi kuendelea kusoma Korona Sec

Lema asitisha wanafunzi kuendelea kusoma Korona Sec

Lema tupia jicho Shule ya Sekondari Oloirien, kwa nini watoto huzuiwa getini wakati agizo la Serikali ni mwanafunzi
asinyimwe haki ya kusoma.
 
Ritz; Unajua wewe mwisho wako wa kuona na kufikiri inafika mwisho wewe umeona vichekesho gani? Ama ya wazazi kulipa fedha na kuliwa na wenye matumbo tumia kichwa kufikiri na kuleta post! Ritz; Kwa mtazamo wako ina maana tunavyosemaga uongozi uliopo madarakani ni janga hauamini?


Lema na siasa zake za Arusha ni vichekesho tu.
 
Last edited by a moderator:
Mbunge wa Arusha mjini Mh. Godbless Lema leo amesitisha wanafunzi wa shule ya Korona Secondari iliyoko kata Ongutoto wilaya ya Arusha. Korona inayopaswa kuwa na wanafunzi 1,200 lakini kwa sasa ni wanafunzi 139 tu wanaofika shuleni hapo na tuliowakuta ni 118 tu, huku kidato cha kwanza wakiwa 19 badala ya 400.

Lema alifikia maamzi hayo kwa kile alicho kiita ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kutembea km 13 huku wakikosa masomo, wanafunzi hao wakitoa ushuuda walisema wamekuwa wakija shuleni na kurudi bila kusoma,Walimu hufika saa sita na kuondoka saa saba na nusu.

Wanafunzi hufika saa tano na kuondoka saa nane,Wanafunzi hawafundishwi na wakifundishwa hufundishwa kipindi kimoja cha dakika 30.

Wazazi wanatoa michango kiasi cha TZS 72,000/= ya chakula kwa watoto wao lakini hawajawahi kupata chakula chochote kwenye shule hiyo, 32,000/= ya sare lakini hawajawahi kupewa sare, 5,000/= ya vitambulisho lakini hawajawahi kupewa vitambulisho.

Watoto wanakunywa maji ya mto Kijenge ambao kwa wanyeji wa kijenge/Arusha wana jua namna ulivyo mchafu.

Hali hiyo imepelekea watoto 98 kuhamishwa na kupelekwa kwenye shule zilizoko manispaa ya jiji la Arusha wakati wizara walishasema shule hizo zimejaa lakini baadhi ya wazazi walitoa ushuuda kuwa kuna rushwa kubwa inayofanyika katika kuhamisha watoto kwani kama huna TZS 200.000/= huwezi kumhamisha mtoto ndiyo maana waliobaki ni watoto yatima ambao wazazi wao ama hawana uwezo huo wa kutoa kiasi hicho cha pesa au hawa thamini elimu ya watoto wao.

Baada ya Lema kusitisha mwanafunzi hao kwenda kusoma Korona alimkabidhi Diwani wa kata hiyo kwenda na watoto kwenye ofisi yake na atakuwa anakaa nao hapo mpaka siku watakapo patiwa shule za kuhamia ambapo Lema alishauri kuwa kila shule iliyoko kwenye jimbo hilo ichukue wanafunzi angalau watano tu, kwa muda ambao shule hiyo itakuwa ikifanyiwa marekebisho na kubadilishwa iwe boarding kitu ambacho ilionekana ndiyo suruhu ya kudumu, mbunge huyo aliahidi kutoa tofari 3000, solar panel, na pampu ya kuvutia maji na atatoa iwapo wanao husika wataonyesha nia...
View attachment 80588
View attachment 80592
Afisa elimu, Diwani, Mbunge, kaimu mkurugenzi na mwalimu mkuu wa shule ya Korona.
View attachment 80594
Wanafunzi wa Korona Secondari wakishangilia maamzi ya mbunge wa Arusha mjini ya kusitisha masomo kwenye shule hiyo..


siungi mkono kusitisha masomo kwa sababu hizo, nakubali kuna tataizo kubwa la msingi shuleni hapo ambalo linahitaji ufumbuzi haraka. ambacho ninaona kungefaaa ni kulishughulikia wakati shule iko on sio kusitisha masomo! na kufunga shule
 
korona4.gif
Wanafunzi wa Korona Sekondari
 
siungi mkono kusitisha masomo kwa sababu hizo, nakubali kuna tataizo kubwa la msingi shuleni hapo ambalo linahitaji ufumbuzi haraka. ambacho ninaona kungefaaa ni kulishughulikia wakati shule iko on sio kusitisha masomo! na kufunga shule
Imesoma vizuri matatizo ya shule hiyo unajua serikali yakikwete inavyofanyakazi?..ulitaka waachwe iliwafanye nini hapo shuleni maana kama ni kusoma walikuwa hawasomi...acheni kupepesa macho...
 
Lema tupia jicho Shule ya Sekondari Oloirien, kwa nini watoto huzuiwa getini wakati agizo la Serikali ni mwanafunzi asinyimwe haki ya kusoma.
Unajua kuna vitu vingine ifike wakati wananchi tusisubiri mbunge yaani mtoto wangu anasoma serikali akarudishwe kisa hajatoa pesa ya mlinzi halafu ni subiri mbunge atupie jicho...NO
 
Hapo kuna mtoto wa kigogo anasoma? Kama yupo masomo yanaweza kuendelea
 
Mkuu unategemea jibu la maana hapo? Hao wakuhurumia tuu,wako kazini hao!

waache kuweka siasa kila sehemu wafikilie maisha ya hawa watoto wanaotembea km 13 kuanzia huku wakiwa wameshatumia nauri 1000 halafu huwafundishi..
View attachment 80670
Wanafunzi wa Korona Sekondari
 
Hapo kuna mtoto wa kigogo anasoma? Kama yupo masomo yanaweza kuendelea

Hata wa balozi wa nyumba kumi hakuna yaani kifupi kama mzazi una akili timamu huwezi kumwacha mtoto wako kwenye shele kama hiyo..ndiyo maana kati ya wanafunzi 1,200 tulio wakuta ni 118 tu...
 
Halafu mtu anakuja humu na kuuliza maswali kama hana kichwa, Lema piga kazi, wacha wapayukaji wapayuke.


......................................
Histiria haiishiwi wino.
 
Hii ni shule ya serikali au ya mtu binafsi? Kama Lema amesitisha wanafunzi, solution yake nini? Anawahamisha kwenda shule nyingine au ndo imetoka hiyo? Mleta mada fafanua hapa!!!

Tiba

Hilo mtoa mada kaliweka vizuri kabisa, wataendelea kukaa ofcn kwake mpaka watakapopata shue za kuhamia "Baada ya Lema kusitisha mwanafunzi hao kwenda kusoma Korona alimkabidhi Diwani wa kata hiyo kwenda na watoto kwenye ofisi yake na atakuwa anakaa nao hapo mpaka siku watakapo patiwa shule za kuhamia ambapo Lema alishauri kuwa kila shule iliyoko kwenye jimbo hilo ichukue wanafunzi angalau watano tu"
 
Wazo la msingi, maana ilikuwa mateso siyo masomo tena
 
namuunga mkono mbunge lema godbless 100% kwa uamuzi wa busara lakini mgumu alioufanya kama kiongozi, tena mbele ya afisa elimu, mwakilishi wa mkurugenzi, mkuu wa shule na diwani. Hapa nalichukulia kama ni suala la kizalendo zaidi ya itikadi za ki vyama na najua ni viongozi wachache wenye uthubutu kama huu. Swali lingine, ilikuwaje makamu wa rais kufungua shule isiyokidhi viwango? Naamini gharama alizotumia mh. Makamu wa rais na ujumbe wake kufika hapo kufungua shule zilikuwa zinatosha kufanya shule kuwa na viwango stahiki. Tusichukulie ushabiki masuala kama haya kwa sababu tu watoto wetu na wadogo zetu wao hawaathiriki na uzembe kama huu. Nakuunga mkono lema, na hata ahadi ulizotoa. Serikali ya tanzania sio masikini lakini imejaa viongozi wabinafsi kiasi cha kutisha! Mh lema viongozi wenzio kama wewe sasa hivi wako mikoani wakipita na kupata per-diem kutangaza mafanikio ya serikali! Aibu kubwa, tubadilike kabla ya kulaaniwa na watoto wasiokuwa na hatia.
 
Je, Lema ana mamlaka ya kisheria ya kuamuru shule ifungwe? je, jambo hili limejadiliwa kwenye council?

Je, wazazi wa watoto hawa wametimiza vipi jukumu la kuhakikisha watoto wao wanapata elimu? Mimi nilidhani Lema ataamrisha halmashauri ianzishe utaratibu wa kuwacharge wazazi wa watoto hawa nauli ya kifordi ili kiwe kinacommute kuwapeleka shule.

Ukijengewa shule halafu bado tena unalalamika kuwa huwezi kufika huko shuleni kwa sababu ni mbali, inakuwa too much complain!

Sio kila mtu anakaa katikati ya mji, hata shule ikiwa katikati ya jiji, kuna wanafunzi wanaotoka pembezoni wanakuja, of course if they see the importance of going to school...
 
jamani jifunzeni kusoma na kuelewa.

Mkuu, nimekwisha toa maelezo juu ya hii kwa mtu mwingine aliyenishambulia. Ukweli ni kwamba mleta mada hapo awali hakueleza kwamba watoto watakwenda wapi na wala picha hazikuwepo ndio maana nilihoji hivyo. Aliongezea hayo maelezo baadae sana labda leo kwa kuwa hii post ilitoka jana jioni.

Ni matumaini yangu umenielewa!!!

Tiba
 
Soma post nzima mbona imeeleweka suluhu itakuwa vipi juu ya watoto hawa.
 
Sasa kuna sababu gani ya kutembea maurefu yote hayo na kusoma kwa dk 30 siku nzima na njaa?
 
Back
Top Bottom