Lema asitisha wanafunzi kuendelea kusoma Korona Sec

Lema asitisha wanafunzi kuendelea kusoma Korona Sec

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
22,227
Reaction score
8,760
Mbunge wa Arusha mjini Mh. Godbless Lema leo amesitisha wanafunzi wa shule ya Korona Secondari iliyoko kata Ongutoto wilaya ya Arusha. Korona inayopaswa kuwa na wanafunzi 1,200 lakini kwa sasa ni wanafunzi 139 tu wanaofika shuleni hapo na tuliowakuta ni 118 tu, huku kidato cha kwanza wakiwa 19 badala ya 400.

Lema alifikia maamzi hayo kwa kile alicho kiita ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kutembea km 13 huku wakikosa masomo, wanafunzi hao wakitoa ushuuda walisema wamekuwa wakija shuleni na kurudi bila kusoma,Walimu hufika saa sita na kuondoka saa saba na nusu.

Wanafunzi hufika saa tano na kuondoka saa nane,Wanafunzi hawafundishwi na wakifundishwa hufundishwa kipindi kimoja cha dakika 30.

Wazazi wanatoa michango kiasi cha TZS 72,000/= ya chakula kwa watoto wao lakini hawajawahi kupata chakula chochote kwenye shule hiyo, 32,000/= ya sare lakini hawajawahi kupewa sare, 5,000/= ya vitambulisho lakini hawajawahi kupewa vitambulisho.

Watoto wanakunywa maji ya mto Kijenge ambao kwa wanyeji wa kijenge/Arusha wana jua namna ulivyo mchafu.

Hali hiyo imepelekea watoto 98 kuhamishwa na kupelekwa kwenye shule zilizoko manispaa ya jiji la Arusha wakati wizara walishasema shule hizo zimejaa lakini baadhi ya wazazi walitoa ushuuda kuwa kuna rushwa kubwa inayofanyika katika kuhamisha watoto kwani kama huna TZS 200.000/= huwezi kumhamisha mtoto ndiyo maana waliobaki ni watoto yatima ambao wazazi wao ama hawana uwezo huo wa kutoa kiasi hicho cha pesa au hawa thamini elimu ya watoto wao.

Baada ya Lema kusitisha mwanafunzi hao kwenda kusoma Korona alimkabidhi Diwani wa kata hiyo kwenda na watoto kwenye ofisi yake na atakuwa anakaa nao hapo mpaka siku watakapo patiwa shule za kuhamia ambapo Lema alishauri kuwa kila shule iliyoko kwenye jimbo hilo ichukue wanafunzi angalau watano tu, kwa muda ambao shule hiyo itakuwa ikifanyiwa marekebisho na kubadilishwa iwe boarding kitu ambacho ilionekana ndiyo suruhu ya kudumu, mbunge huyo aliahidi kutoa tofari 3000, solar panel, na pampu ya kuvutia maji na atatoa iwapo wanao husika wataonyesha nia...
korona.gif
korona2.gif
Afisa elimu, Diwani, Mbunge, kaimu mkurugenzi na mwalimu mkuu wa shule ya Korona.
korona3.gif
Wanafunzi wa Korona Secondari wakishangilia maamzi ya mbunge wa Arusha mjini ya kusitisha masomo kwenye shule hiyo..
MBUNGE wa Arusha Mjini,-Godbless Lema, ameifunga Shule ya Sekondari-Korona iliyopo Kata ya Engutoto jijini hapa, ambayo ilizinduliwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, mwaka 2011.

Lema alifikia uamuzi huo katika kikao cha pamoja cha mashauriano shuleni hapo na Kaimu Mkuu wa Shule hiyo, Eusebi Maeda, kilichohudhuriwa pia na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji ambaye ni Ofisa Utumishi, Eliphas Mollel na Ofisa Elimu Sekondari, Violet Muwowoza.

Alisema kuwa aliifunga shule hiyo kutokana na kukabiliwa na matatizo mengi yaliyosababisha wanafunzi kushindwa kusoma tangu ifunguliwe Januari 14, mwaka huu.

Matatizo hayo ni pamoja na umbali unaosababisha wanafunzi na walimu kutembea kilometa 6.5 hadi kufika shuleni hapo, hivyo kuwa na muda mfupi wa masomo.

Shule hiyo pia haina huduma ya maji safi baada ya bomba lililokuwepo kukatwa na mamlaka ya maji kutokana na deni la sh 340,000. Pia, pamoja na walimu watano waliopo, mkuu wa shule na msaidizi wake hawaonekani.

Kati ya wanafunzi 1,200 wa kidato cha kwanza hadi cha tatu wa shule hiyo ni wanafunzi 118 pekee ndio wanaohudhuria masomo.

Lema aliwaagiza wanafunzi hao wafike ofisini kwake na wazazi wao kesho, huku akimtaka Diwani wa kata hiyo, Anthony Male, kwa kushirikiana na ofisa Elimu kuwahamishia kwa mafungu wanafunzi hao katika shule nyingine zilizomo ndani ya Jiji la Arusha.

Mbunge huyo aliahidi kutoa pampu ya kuvutia maji, vifaa vya kuzalisha umeme wa jua pamoja na matofali 3,000 na kwamba atashirikiana na mkuu wa wilaya na mkoa kuhakikisha shule hiyo inaboreshwa ndani ya miezi mitatu ili kutoa fursa ya kuchukua wanafunzi wa bweni.

Naye Ofisa Elimu Sekondari, Violet Muwowoza, alijitetea kuwa yeye angeomba kwanza afuate- taratibu za kuandika barua kwa Ofisa Elimu Kiongozi ambaye ana mamlaka ya kufunga shule, jambo ambalo Lema alisema aendelee na taratibu zake wakati wanafunzi hao wakiendelea na masomo katika shule nyingine.

Aidha katika utetezi wake juu ya changamoto za shule hiyo, Ofisa Elimu huyo alisema alikwisha kuwahi kupeleka mapendekezo katika vikao vya baraza la jiji vya kununua magari ya wanafunzi lakini yakapingwa na kusema hata hivyo wengi wa wanafunzi waliopelekwa katika shule hiyo wanatoka shule za mchepuo wa Kiingereza, ndiyo maana hawaripoti shuleni hapo.

Kaimu Mkurugenzi alimuomba-Lema asubiri kiitishwe kikao cha dharura cha baraza la madiwani wa jiji, alichodai huenda kitatoka na suluhisho zuri zaidi-kuhusiana na shule hiyo.
 
Mkuu nini kinafuata/kunamkakati gani kuhakikisha mambo yawekwa sawa na watoto wanaendelea na masom? maana kusoma

bado ni haki kwao. Habari hii inaumiza sana, maana majivuno ya ccm majukwaani yanatia kichefuchefu.
 
duh!
hii kali, sasa kamanda atawapeleka wapi?
CCM hawana ubinadam kabisa aisee..
 
Hii ni shule ya serikali au ya mtu binafsi? Kama Lema amesitisha wanafunzi, solution yake nini? Anawahamisha kwenda shule nyingine au ndo imetoka hiyo? Mleta mada fafanua hapa!!!

Tiba
 
Lema na siasa zake za Arusha ni vichekesho tu.
 
Nashauri Lema aonyeshe mfano kutafuta eneo la karibu waanze ujenzi wa shule wananchi wa arusha wakitoa 1000 kwa wananchi 70000 mh atakua na milioni 70 zinatosha kabisa kuanza ujenzi + yeye akiongezea na kupata na wadau wengine shule itajengwa kwa haraka sana.
 
Kinachopaswa hapa kufanywa na Lema ni kulivalia njuga hili suala na kuhakikisha kila mwanafunzi anapata shule atakayoamia ili asiendelee kuathirika kwa kukosa masomo.
 
Sidhani Kama anawasaidia wanafunzi wake na mda ndo unayoyoma........acha azalishe mambumbumbu......huyu jamaa sijuwi Kama anatafakari Kabla hajatenda.....ohh alisoma Kile chuo
 
Mkuu nini kinafuata/kunamkakati gani kuhakikisha mambo yawekwa sawa na watoto wanaendelea na masom? maana kusoma

bado ni haki kwao. Habari hii inaumiza sana, maana majivuno ya ccm majukwaani yanatia kichefuchefu.
wanafunzi watasambazwa kwenye shule zilizoko wilaya ya Arusha mjini kwa muda, pia shule hiyo kubadilishwa na kuwa boarding na katika mabadiliko hayo yeye ametoa solar panel, Mota, na tofari 3000 za ukuta kwani shule hiyo iko karibu na kolongo na ilionekana kwa usalama wa wanafunzi ukuta na walinzi ni mhimu sana...

net na umeme itatizo kwangu leo...
 
Sijaelewa bado au ndiyo shule ya kata. Sera ya elimu ikoje? Wakaguzi wa elimu kuanzia kata wako wapi?
 
duh!
hii kali, sasa kamanda atawapeleka wapi?
CCM hawana ubinadam kabisa aisee..
Nilikuwa nakimbiza na umeme na net ya leo...wata hamishiwa kwenye shule zilizoko wilaya ya Arusha angala kila shule ichukue watoto hata watano watano
 
Kama mbunge ulikuwa wapi ck zote badala ya kuhamasisha wananchi wako wakaboresha mazingira ya shule kuliko kuwahamisha.....am not sure Kama unajua impact yake baadaye.......ahhhhhh kumbe alisoma Kile chuo
 
Sijaelewa bado au ndiyo shule ya kata. Sera ya elimu ikoje? Wakaguzi wa elimu kuanzia kata wako wapi?

Ni moja ya shule za kata...lakini imeone kana ni shule ambayo ni nzuri pale tu matati hayo yakitatuliwa na kubadilishwa kuwa boarding kwani iko nje ya mji na hali ya hewa ni nzuri sana...
 
Kama mbunge ulikuwa wapi ck zote badala ya kuhamasisha wananchi wako wakaboresha mazingira ya shule kuliko kuwahamisha.....am not sure Kama unajua impact yake baadaye.......ahhhhhh kumbe alisoma Kile chuo
Alikuwa mahakamani na kisha akawa honeymoon kwa takribani mwaka mzima...
 
Basi wapeleke nyumbani kwako uwalee Kama unawaonea huruma.....hizi ndizo impact za maandamano hakuna mda wa kufanya kazi wabunge wenzake ahhh swafiiiiiiiiiiiiii
 
maccm kila siku yanajitapa yamepiga hatua kwa miaka 50.... yananikera sana haya mamtu sio siri... nahisi akili zao haziko sawa
 
Sidhani Kama anawasaidia wanafunzi wake na mda ndo unayoyoma........acha azalishe mambumbumbu......huyu jamaa sijuwi Kama anatafakari Kabla hajatenda.....ohh alisoma Kile chuo

Watoto watasoma kwenye shule zingine kwa muda wakati wahusika wakifanyia kazi mapungufuya shule hiyo kwani hata hivyo walikuwa hawasomi kwa maana hiyo hata kama ange waacha bado walikuwa hawasomi...
 
maccm kila siku yanajitapa yamepiga hatua kwa miaka 50.... yananikera sana haya mamtu sio siri... nahisi akili zao haziko sawa
Hata hiyo shule ilifunguliwa na makamu wa raisi tena kwa mbwembwe nyingi sana...
 
Back
Top Bottom