Lema asitisha wanafunzi kuendelea kusoma Korona Sec

Lema asitisha wanafunzi kuendelea kusoma Korona Sec

Tukiwambia lema jembe hua hamtuelewi na 2015 atakua waziri wa mambo ya ndani.watu watafagiaje barabara!kamanda lema anatisha
 
Sijui kama kiprotoko mbunge anayo amri ya kufunga shule. Lets see what will happen, lakini sidhani kama mbunge ana mamlaka ya kufunga shule. Itachekesha pale mkuu wa wilaya atakapokuja kuamrisha watoto waendelee na masomo hapohapo.
 
Soma kilichoandikwa sio unasoma heading tu na kuanza kuchangia! ......kaagiza wapelekwe shule nyingine mpaka shule yao itakapowekwa mambo sawa...............

Hii ni shule ya serikali au ya mtu binafsi? Kama Lema amesitisha wanafunzi, solution yake nini? Anawahamisha kwenda shule nyingine au ndo imetoka hiyo? Mleta mada fafanua hapa!!!

Tiba
 
Imesoma vizuri matatizo ya shule hiyo unajua serikali yakikwete inavyofanyakazi?..ulitaka waachwe iliwafanye nini hapo shuleni maana kama ni kusoma walikuwa hawasomi...acheni kupepesa macho...

Mkuu, nimekusoma, ila nataka kujia mamlaka ya Mbunge ktk kuruhusu au kukataza shughuli za maendeleo katika jimbo lake, ninachojua ingawa ni mwakilishi wa wananchi, yeye ni kama msimamizi wa shughuli za maendeleo ktk jimbo lake, kusimamisha/ kufunga shule mamlaka haya ni ya waziri mwenye dhamana, na hapa ndipo tunachanganya siasa na utaalam, utao awabunge wanakuwa ndo mainjinia wa umeme, maji na barabara nk. bado nasisitiza mbunge hana mamlaka haya kisheria... corect me if i'm wrong! he could have been smarter than this!
 
This is a joke. Where are the education officers? How can an MP close down a school? Kweli siasa za tanzania ni joke
 
Hatari! Hizi shule za kata zimekuwa duni kitaaluma, kimiundo-mbinu, kimkakati nk nk Mbaya zaidi watawala wa awamu ya nne wanaamini na kujisifu kuwa shule ni majengo na sio taaluma (ubora wa elimu ya walimu na wanafunzi).

Kuna shule nimeziona watoto wa kidato cha kwanza wanakula ugoro, bangi, gongo kisa hawana kuwekwa kwenye majengo (eti shule) ambazo hazina hata chembe ya huduma za kishule na malezi.

Tunaelekea kubaya, na kizazi kijacho tujiangalie sana Watanzania wenzangu. Hatua ya Mh. Lema ni ya dharura na ikitekelezwa kikamilifu basi huenda nusu ya shule za serikali zitafungwa.
 
Mkuu, nimekusoma, ila nataka kujia mamlaka ya Mbunge ktk kuruhusu au kukataza shughuli za maendeleo katika jimbo lake, ninachojua ingawa ni mwakilishi wa wananchi, yeye ni kama msimamizi wa shughuli za maendeleo ktk jimbo lake, kusimamisha/ kufunga shule mamlaka haya ni ya waziri mwenye dhamana, na hapa ndipo tunachanganya siasa na utaalam, utao awabunge wanakuwa ndo mainjinia wa umeme, maji na barabara nk. bado nasisitiza mbunge hana mamlaka haya kisheria... corect me if i'm wrong! he could have been smarter than this!
Yeye kasha sitisha wanafunzi kwenda kukua kwenye shule hiyo na kwakuwa hana mamlaka ya kufunga shule na kwa kuwa afisa elimu na kaimu mkurugenzi walikuwepo wao watafata utaratibu unao takiwa na serikali lakini kwa kibunge au yeye kama mwakilishi wa wananchi kashasitisha mpaka hapo matatizo husika yata boreshwa...
 
MBUNGE wa Arusha Mjini,-Godbless Lema, ameifunga Shule ya Sekondari-Korona iliyopo Kata ya Engutoto jijini hapa, ambayo ilizinduliwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, mwaka 2011.

Lema alifikia uamuzi huo katika kikao cha pamoja cha mashauriano shuleni hapo na Kaimu Mkuu wa Shule hiyo, Eusebi Maeda, kilichohudhuriwa pia na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji ambaye ni Ofisa Utumishi, Eliphas Mollel na Ofisa Elimu Sekondari, Violet Muwowoza.

Alisema kuwa aliifunga shule hiyo kutokana na kukabiliwa na matatizo mengi yaliyosababisha wanafunzi kushindwa kusoma tangu ifunguliwe Januari 14, mwaka huu.

Matatizo hayo ni pamoja na umbali unaosababisha wanafunzi na walimu kutembea kilometa 6.5 hadi kufika shuleni hapo, hivyo kuwa na muda mfupi wa masomo.

Shule hiyo pia haina huduma ya maji safi baada ya bomba lililokuwepo kukatwa na mamlaka ya maji kutokana na deni la sh 340,000. Pia, pamoja na walimu watano waliopo, mkuu wa shule na msaidizi wake hawaonekani.

Kati ya wanafunzi 1,200 wa kidato cha kwanza hadi cha tatu wa shule hiyo ni wanafunzi 118 pekee ndio wanaohudhuria masomo.

Lema aliwaagiza wanafunzi hao wafike ofisini kwake na wazazi wao kesho, huku akimtaka Diwani wa kata hiyo, Anthony Male, kwa kushirikiana na ofisa Elimu kuwahamishia kwa mafungu wanafunzi hao katika shule nyingine zilizomo ndani ya Jiji la Arusha.

Mbunge huyo aliahidi kutoa pampu ya kuvutia maji, vifaa vya kuzalisha umeme wa jua pamoja na matofali 3,000 na kwamba atashirikiana na mkuu wa wilaya na mkoa kuhakikisha shule hiyo inaboreshwa ndani ya miezi mitatu ili kutoa fursa ya kuchukua wanafunzi wa bweni.

Naye Ofisa Elimu Sekondari, Violet Muwowoza, alijitetea kuwa yeye angeomba kwanza afuate- taratibu za kuandika barua kwa Ofisa Elimu Kiongozi ambaye ana mamlaka ya kufunga shule, jambo ambalo Lema alisema aendelee na taratibu zake wakati wanafunzi hao wakiendelea na masomo katika shule nyingine.

Aidha katika utetezi wake juu ya changamoto za shule hiyo, Ofisa Elimu huyo alisema alikwisha kuwahi kupeleka mapendekezo katika vikao vya baraza la jiji vya kununua magari ya wanafunzi lakini yakapingwa na kusema hata hivyo wengi wa wanafunzi waliopelekwa katika shule hiyo wanatoka shule za mchepuo wa Kiingereza, ndiyo maana hawaripoti shuleni hapo.

Kaimu Mkurugenzi alimuomba-Lema asubiri kiitishwe kikao cha dharura cha baraza la madiwani wa jiji, alichodai huenda kitatoka na suluhisho zuri zaidi-kuhusiana na shule hiyo.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Ni kweli shule nyingi zilifunguliwa kisiasa pasipo kubaini uhalisia wake. Watoto wetu wemefilishwa hapa. Na matokeo ya kidato cha pili ni wanafunzi sita tu ndio wamefaulu. Ni kweli ifungwe ili wapate fursa ya kutathimini vizuri.
 
lemajukwaani_300_259.jpg


Kitendo cha Mbunge Lema wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kufunga shule ni dalili kwamba hakutumia busara na amechukua jukumu kinyume cha sheria. Mbunge hana mamlaka ya kufunga au kuamrisha jambo, bali ni mshauri serikalini. Alitakiwa kuwasiliana na wahusika baada ya kuona tatizo na kusingetokea migongano. Kwa vyo vyote katika hili amekosa busara, amejichukuklia madara yasiyo yake, amejiweka juu ya serikali. Anatakiwa kuheshimu mamlaka za serikali kwa sababu ndio wenye mamlaka hayo si yeye Lema.

Mkuu wa Wilaya Amefungua chule hiyo dalili ya wazi ya mgongano kati yake na mbunge Lema. Lema angetumia busara asingegona na angebaki na heshima yake.
 
Nasikia mkuu wa wilaya kaifufungua tena. Hii inaweza kumaanisha nini? mfyetele na jonahex
 
Last edited by a moderator:
Hapo Lema alikurupuka, afisa elimu alishauri vizuri hakumsikia. Hii ndio weakness kubwa ya wanasiasa wetu.
 
Nani kakwimbia heshima yake imepotea? Hishima imepotea kwa Bilal ambaye toka aingie madarakani yeye anatembea na mkasi mfukoni kufungua hata mmajengo ambayo hayajaisha
 
John Mongela nae amechemka sana alipomvua madaraka Mwl Mkuu,alimtaka afike kwenye kikao (Mwl yuko nje Mkoa kwa dharula) yeye anamvua bila hata ya kujitetea kwa nini hakufuka!uongozi wa kiimla huo!wewe jaji,wewe mwendesha mashitaka na wewe ndio shahidi!mtuhumiwa hajajieleza hata ukajua yaliyomsibu!sio hivyo!uongozi wa jazba
 
Nani kakwimbia heshima yake imepotea? Hishima imepotea kwa Bilal ambaye toka aingie madarakani yeye anatembea na mkasi mfukoni kufungua hata mmajengo ambayo hayajaisha

Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

Kwa hili Lema amekoroga, na kwanza hana mamlaka ya kufanya hivyo. Anachotakiwa kukfanya ni kuishauri serikali ifanye hivo si yeye. Nashangaa amevimbishwa kichwa kiasi cha kumfikisha kutojua hata mipaka yake ya utendaji kama mbunge.
 
Tatizo la Lema kukurupuka hata kama jambo linaitaji maongezi siasa za makengeza ndizo zinaizamisha Chadema.
 
Mabadiliko ni wewe, ukisema kila kitu usubiri hao viongozi walio jaa ubinafsi, hakuna kitu kitacho fanyika.
 
Back
Top Bottom