Lema ashinda rufaa dhidi ya ubunge wake!

january makamba aliandika kwenye fb yake kuwa lema anavuliwa ubunge kabla hata ya hukumu .... alifurahi sana ... sijui leo yu wapi
 
Kwa kuanzia tu maandamano na vurugu zisizo na tija yanaanza lema atakapowasili arusha. Shuguli za maendeleo zitasimama kwa muda. Tourism industry itapata shida barabarani kwa kufungwa njia na wazee wa viroba ambao ni jeshi la lema. Watalii hawatakuwa na amani. Mungu amesaidia barabara nyingi zimejengwa wakati hayupo maana fedha za un zingewezatokomea kusiko julikana angekuwepo kwenye vikao.(arusha bila mbunge lema inawezekana)
Pole sana maana ndiyo kazi imeanza na hao mgambo wenu mnaowatumia kunyanyasa mama zetu pale NMC ni mwisho mwambie kabisa na huyo mmeo mkurugenzi na meya wa kuchonga bila kuwasahau machizi wa magogoni kuwa Lema karudi huo uhuni wao tutautokomeza...
 
Yaani tokea saa tatu na nusu hivi nilipoyapokea haya matokeo nimefurahi mpaka machozi ya furaha yamenitoka. Nilikuwa najiandaa kunywa breakfast lakini kwa furaha niliyokuwa nayo njaa sina tena na sijui kama njaa ya kula lunch nitaipata.

Tokea tulipokuwa tunaenda Mahakama Kuu ya Arusha kusikiliza kesi hii tuliona haikuwa na sababu yoyote ya kumvua LEMA Ubunge. Cha kushangaza Jaji alimvua. Lakini haki ya mtu haipotei, hatimae ameipata. Hongera LEMA na CHADEMA kwa ujumla.

Tunasubiri kukupokea kwa hamu hapa Arusha.
 
Credits to the appeal judges kwa kweli....wameonyesha mahakama ya rufaa kuna umakini mkubwa kwenye kutoa haki kwa kweli....Once again...hukumu hii inathibitisha ukweli wa uwepo wa mediocre judges kwenye mahakama kuu....hili limejionyesha tena kenye kesi hii.....yule jaji aliyehukumu arusha sijui anajionaje sasa??what a mediocre judge!!!....
 
Usijifanye wewe mjuaji kuliko wananchi wa Arusha waliopiga zaidi ya kura 50,000 kumchagua Lema. Katika hao wako watu wa rika mbalimbali, taaluma mbalimbali, usiwafanye wajinga kuwa wakati wanamchagua walikuwa hawajui wanalolifanya...

Usilete masihala kwa mbunge aliyechaguliwa na kura za wananchi, mchezo wako na wivu peleka kwa akina Vicky Kamata na Sophia Simba. Waulize wana Arusha kwa nini walimchagua na kwa nini saizi wako full shangwe baada ya kurejeshewa ubunge wake???
 
Salamu hizi zimfikie moja kwa moja Regia Mtema(RIP).
Naamini huko aliko ameweka usoni lile tabasamu lake linalotibu ugonjwa wa Presha!


cc. Remmy
 
Last edited by a moderator:
Kama kuna makosa ya kisiasa ambayo CCM walifanya na watayajutia sana, ni siasa za Arusha.

Arusha ndio pameonesha wazi jinsi ambavyo watawala wanataka kupindisha sheria kwa maslahi yao ya kisiasa.

Hii imefanya hata waliokuwa wakereketwa wa CCM, lakini ni wapenda haki, wakichukie chama.

Hii pia imekuwa reference ya wazi hata sehemu nyingine za mbali na Arusha.

CCM itafakari vema maneno ya Injili:

Kwa maana, ni nani miongoni mwenu ambaye akitaka kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama zake ili ajue kama ana kiasi chakutosha cha kumalizia? La sivyo, baada ya kuweka msingi na kushindwa kumaliza, watu watamcheka wakisema: `Mtu huyu alianza kujenga, lakini hakumalizia.`"Au, ni mfalme gani ambaye, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, hataketi kwanza chini na kufikiri kama ataweza, kwa askariwake elfu ishirini? Kama anaona hataweza, atawatuma wajumbe kutaka masharti ya amani wakati mfalme huyo mwingine angali mbali.
Lk. 14:28-32
 
Bwana Lema hongera kwa kushinda kesi yako ua Ubunge na karibu sana tufanye kazi.
Sasa bwana Lema tunaomba utulie ufanye kazi na uwache mambo yako ya kitoto na fujo zisizo na msingi.

Utakumbuka ulivyokuwa Mbunge maandamano yalikuwa hayaishi ila ulivyosimamishwa mji ulitulia na watu tukafanya kazi vizuri sana. Tunakupenda sana kama Mbunge wetu ila hatutavumilia kama uta anza tena fujo zako.

Asaante sana na sisi wafanyabishara wa Arusha tuko tayari kushirikiana na wewe katika kazi

Wasalaam
 
january makamba aliandika kwenye fb yake kuwa lema anavuliwa ubunge kabla hata ya hukumu .... alifurahi sana ... sijui leo yu wapi
Mkuu, nawe...!
Bado unaongelea hawahawa kundi la wanaojiita 'vijana' akina prezoo?....tuache tupumuweee leooo!
 
Back
Top Bottom