Lema amjibu DPP Mganga Biswalo, amtaka aache kutisha watu

Hii ndiyo awamu ya kwanza kumuona DPP akiongea na vyombo vya habari kama mwanasiasa. Watanzania hatukuzoea. Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ametusemea watu wengi tulioumizwa na DPP Biswalo Mganga. Hakika Mungu atamlinda Godbless Lema dhidi ya hila zote za kishetani. Hapa nawakumbusha tu baadhi ya uovu ambao DPP Biswalo Mganga ameufanya kwa makusudi au kwa kutumika na anayemtuma;

1. Kwenye Plea bargaining wanafanya dhuluma ya wazi wazi kwa kuchukua fedha kwa watu ambao wamewakamata bila ushahidi. Watu wanasota miaka mitatu rumande kwa kisingizio upelelezi haujakamilika, then wanaambiwa waombe msamaha ili waingie plea bargain. Kimsingi Plea bargain inapaswa ifanyike na kusimamiwa na Mahakama, lakini hapa Tanzania inasimamiwa na DPP. Plea bargain ni mradi wa kujipatia fedha binafsi kati ya Jiwe na Biswalo Mganga. Kuna fedha ambayo wanaingiza Serikalini kwenye akaunti ya Plea bargain lakini kuna fedha zingine wanachukua wao binafsi ambazo hazina rekodi lakini mtuhumiwa anaambiwa atoe ili aaweze kuwa eligible.

2. Aliwaachia askari waliomuua Akwilina wa DIT na akawafungulia Mashtaka viongozi 9 wa CHADEMA ambao last week walichangiwa hela na wananchi ili wasifungwe miezi 5 jela.

3. Amewabambikia kesi akina Eric Kabendera, Tito Magoti na wenzie kwa kuwapa kesi ya kutakatisha hela ingawa kwa sabau tu ya kuikosoa Serikali

Tuombe Mungu atupe uhai, awamu inayokuja namuona Biswalo Mganga naye akipelekwa Mahakamani kama anavyopeleka wenzie pamoja na Kamanda Lazaro Mambosasa.
DPP kabla ya kuwa DPP hakuwa na kitu alikuwa masikini mtu wa kawaida tu, lakini mpaka sasa kawa Tajiri mkubwa kama Naibu Rais Daud Bashite. Achunguzwe mali zake wananchi ingieni kazi mtoe taarifa za mali zake hata kama kaandika majina ya ndugu jamaa marafiki.
 
Cha msingi ushahidi wa mauji hayo ya kuchinjwa awe nao tu,
Combination ya ofisi hizi mbili kwa maana ya polisi na DPP usipime
Ushahidi siyo shida bali jiulize, Je DPP alipaswa kumtishia Godbless Lema kama ameongea habari ambayo siyo ya ukweli? Kwani Job despription ya DPP inasemaje? Ukiweza kujibu maswali hayo utagundua kuwa DPP alikuwa anajihami kwa ukweli anaoufahamu kuhusu mauaji ya Singida.
 
Ushahidi siyo shida bali jiulize, Je DPP alipaswa kumtishia Godbless Lema kama ameongea habari ambayo siyo ya ukweli? Kwani Job despription ya DPP inasemaje? Ukiweza kujibu maswali hayo utagundua kuwa DPP alikuwa anajihami kwa ukweli anaoufahamu kuhusu mauaji ya Singida.
DPP wa Tanzania ni mwanasiasa ni tofauti na DPP wengine wote Duniani
 
Wasukuma wote mlaani DPP kwani ndiye kawaletea yote haya kama siyo DPP kumfanyia Lema ushetani leo hii wasukuma msingekuwa mnalaumiwa humu, wasukuma wote popote mlipo mmulaaani DPP kwa kuwadhalilisha wote
 
DPP ni Msukuma mwenzako acha kuwatetea wasiojali haki za binadamu, jitetee wewe na ukoo wako ambao nyie wachache pengine ni wasitaarabu hamna Tatizo na watu
Unajua mi nimesoma na shule imeijenga akili yangu. Nikiona mtu anahusisha kabila na majukumu ya kiserikali, napata hisia kwamba huyo shule yake ndogo. Akili haijanufaika na elimu.
 
Hapa kabila linakuja kwa sababu ipi? Hiyo ndo dalili ya poor brain. Mtu ambaye hajaweza kuinua akili yake, anahangaika kuwaweka wengine chini ili aonekane yuko juu. That is rubbish and stupid.
Vp kuhusu kauli ya jiwe juzi darajan moro kumuhusu mama mchaga aliyekula kona na pesa za kikoba 😆😆
 
Nadhani wapinzani muanzishe kikundi cha taarabu mkate na viuno kuukatikia mti. Yaani Mh. Lema unakosa kabisa hoja unabaki kutoa allegations za uongo uongo. Hivi ni nani ambaye aliwahi kusema ofisi ya DPP ni legelege? Yaani hujui hata DG wa TPDC ilikuja kubainika alisingiziwa? Hivi hujui msamaha kwa wahujumu uchumi umetoa nafasi kwa wahusika kujutia makosa??? Hivi Mh. Lema kwa nini hamkumlipia Kabendara? Yaani mmeishiwa kabisa.
ungemuuliza Magu je kwa akina Kabendera hawana undugu kama kwa akina Msigwa
 
Mamlaka yanaweza mpumbaza mtu akaona yeye ni Yesu wa duniani.

Lakini ukweli ni kwamba huu ulimwengu unatawaliwa kwa misingi ya HAKI.

Huwa ni suala la muda tu, lakini kila nafsi lazima ipate mshahara wa matendo yake!!

Lema upo sahihi...Bravo!!
DPP kama ana Akili timamu ataitumia fursa hii kujitafakari vizuri na kuachana na ushetani wake
 
Back
Top Bottom