Lema amjibu DPP Mganga Biswalo, amtaka aache kutisha watu

Kuingilia uhuru wa Mahakama ni kosa kisheria na kikatiba. Mhe. Lema kama Mbunge ni mtunga sheria na anajua hivyo. Angekwenda mahakamani kumshitaki DPP badala ya kumtolea vitisho ambavyo, kisheria, vinazidi kumtia hatiani yeye mwenyewe. Pili, hili suala la kufuata fuata ni tuhuma ya ajabu kusemwa na Mhe. Lema. Yaani kwa vile ni Mbunge na Waziri Kivuli basi anafikiri anaweza kuvunja sheria na kubaki juu ya sheria?
Kumtishia mtu ni nini?
 
Kila MTU na mtazamo wake kulingana na chama chake
 
Kuingilia uhuru wa Mahakama ni kosa kisheria na kikatiba. Mhe. Lema kama Mbunge ni mtunga sheria na anajua hivyo. Angekwenda mahakamani kumshitaki DPP badala ya kumtolea vitisho ambavyo, kisheria, vinazidi kumtia hatiani yeye mwenyewe. Pili, hili suala la kufuata fuata ni tuhuma ya ajabu kusemwa na Mhe. Lema. Yaani kwa vile ni Mbunge na Waziri Kivuli basi anafikiri anaweza kuvunja sheria na kubaki juu ya sheria?
Hakuvunja sheria, yeye kama waziri kivuli au Shadow minister hiyo ipo kwenye moja ya kazi zake....ameona kuna kesi ambazo zimechukua muda mrefu na huko kwenye hiyo wilaya watu wanauawa ovyo, hivyo ni jukumu la serikali au polisi kusema upelelezi huo umefikia wapi lakini serikali hizi za kijinga jinga za kijamaa zinaficha...Wewe unategemea Godbless Lema apate wapi information? Polisi hawataki na authority hawataki kutoa information, Lema ametoa kile alichoambiwa na ikatokea watu 14 kweli wameuawa...Hivyo ni jukumu la serikali au polisi kukanusha siyo DPP kwenda kwenye press conference na kuropoka aliyo yaropoka.
 
Pascal say something my friend on this! Hii kusema ''Duh....! " haisaidii lolote....!
Alichoongea Mhe. Lema Ni UKWELI mtupu....MGANGA Biswalo amekuwa anaingulia Uhuru na maamuzi ya Mahakama....!
Hata juzi amekurupuka kuhusu Hukumu ya Viongozi wa CHADEMA....!
Mkuu Mzalendo,
1. Jee ulimsikia Mhe. Lema mwanzo aliongea nini?.
2. Jee ulimsikia DPP alimjibu nini?.
3. Sasa umemsikia Mhe. Lema anacho zungumza, amejibu hoja za DPP?.

DPP ana mamlaka ya kuingilia kesi yoyote ya jinai ikiwa katika stage yoyote only kabla ya hukumu. Na baada ya hukumu, DPP anao uhuru wa kukata rufaa kupinga hukumu yoyote kama ilivyo haki ya mshtakiwa kukata rufaa baada ya kuhukumiwa.
Kuhusu powers za DPP tumezijadili sana humu. Kwa vile jf ni kisima cha maarifa, karibu mitaa hii ujielimishe kuhusu DPP.

Nani Zaidi Kati ya Bunge na Mahakama?!. The Doctrine of "Separation of Powers" Nothing, Just a Myth!
Pia kasome
‪DPP atumie madaraka yake kisheria ipasavyo, asisubiri maelekezo ya wanasiasa ili afanye kazi‬

P
 
Acha ujinga wako DPP hana madaraka hayo uliyomsimika kienyeji na wala hasubiri maelekezo ya wanasiasa kwani tayari anayo maelekezo ya wanasiasa wa CCM maelekezo ya kuwaonea kuwabambikia kuchelewesha kesi, na kama DPP anayo mamlaka ya kuingilia kesi yeyote katika stage yeyote hayo ni mamlaka haramu ndiyo yanayolalamikiwa kutumika vibaya kuwabambikia watu kesi za uhujumu uchumi kuchelewesha kesi makusudi na usumbufu mwingine mwingi sana, hapa hujaelimisha chochote juu ya DPP zaidi ya kujimwambafy tu kumtetea kwa mambo yake ya uonevu
 
DPP anasubiri maelekezo ya CCM hafanyi kazi kwa mujibu wa Sheria anafanya kazi kwa mujibu wa zidumu fikra za CCM tu si zaidi ya hapo.
 
Kuingilia uhuru wa Mahakama ni kosa kisheria na kikatiba. Mhe. Lema kama Mbunge ni mtunga sheria na anajua hivyo. Angekwenda mahakamani kumshitaki DPP badala ya kumtolea vitisho ambavyo, kisheria, vinazidi kumtia hatiani yeye mwenyewe. Pili, hili suala la kufuata fuata ni tuhuma ya ajabu kusemwa na Mhe. Lema. Yaani kwa vile ni Mbunge na Waziri Kivuli basi anafikiri anaweza kuvunja sheria na kubaki juu ya sheria?
DPP ashitakiwe mahakamaccm? au ashitakiwe The Hague? Kumbuka mahakamaccm ni mali binafsi ya DPP ni vigumu Lema kupata haki labda kwa nguvu za mwenyezi mungu, lema hukumtolea vitisho bali kamshitaki DPP kwa wananchi wa Tanzania wajue mapungufu yake mapema.
 
Akiongea kupitia youtube chanel yake ya GLema Tv amemuonya DPP kuacha kutisha watu.

”…Mimi nimwambie DPP kwamba taifa hili linaanza kushuhudia kuwa yeye ni DPP wa kwanza anayeweza kutoka hdharani n akum-comvict mtuhumiwa. DPP siyo mahakama, wala DPP siyo Polisi…”

“…Katika shauri hili lililopo mkoani Singida nilipewa dhamana na polisi, baada ya kukaa lockup kwa takribani siku tatu. Na tulikubaliana nirudi polisi tarehe 24 mwezi huu, baadaye nikapigiwa simu kuwa natakiwa Polisi tarehe 19 jambo ambalo nilikuwa najiandaa nalo…”

“…Katika jambo hili nilipata fursa ya kuongea na IGP, na nilimpelekea meseji hata IGP ya majina haya ya watu ambao wameuawa kule Manyoni. Na nilimuomba IGP tuongee hata kabla sijaitaja ile list hadharani, nikifanya huvyo kama Mbunge, Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani na mtu ambaye nachukia kuona watu wanauawa hovyo…”

“…DPP katika mazungumzo yake, kitu ambacho kimenifanya nimjibu, kwanza hana mamlaka kisheria ya kuita vyombo vya habari kunihukumu kabla ya mahakama haijanihukumu. Hana hayo mamlaka kisheria; anakwenda kinyume kabisa na utaratibu wa kazi yake…”

“…Ile aliyofanya ni kudhihaki Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Setrikali katika taifa hili.

Swali ambalo watu wanatakiwa wajiulize ni kwanini DPP amekuwa na mamlaka makubwa sana katika Taifa hili, huyu tuliye naye. Ni kwanini DPP anaweza aka pre-empt maamuzi ya court? Ni kwanini DPP anatoka hadharani, anajaribu kumkemea Mbunge, kuchafua Mbunge na kumdhalilisha Mbunge wakati Mahakama bado haijafanya maamuzi wala kesi bado haijasikilizwa?...”

"...Maganga, Biswalo; Kama kuna mtu ameumiza watu wengi nchi hii, wewe ni aidha namba moja ama namba mbili..."

“…Mioyo ya watu wengi imepondeka. Hawakwambii pengine hawana guts niliyo nayo mimi; hawakwambii pengine wanaogopa wanasubiri hii regime ipite. Na itapita hii regime. Kwasababu hii regime haiongozwi na Mwenyezi Mungu wala Yesu….umetumia ofisi yako vibaya sana, na hata leo unatumia ofisi yako vibaya…”

…”Nakuhakikishia kama Mungu aishivyo, kwanza sikuogopi na siogopi unaweza ukaamua kitu gani juu ya maisha yangu kwasababu anayeweza kuamua maisha yangu ni Mwenyezi Mungu peke yake. Kwahiyo elewa kwamba sikuogopi na hakuna namna yoyote unaweza kunitisha nikakuogopa. Na nitaendelea kufanya kazi yangu. Fanya chochote…”

DPP: Mbunge Lema kuchukuliwa hatua kwa kupotosha vifo vya watu 14 Manyoni, Hatuwezi kuwa na Taifa la watu wazushi na wazua taharuki
Safi sana Muheshimiwa Godbless Lema,
Jina lako tu ni kinga tosha dhidi ya hii mijitu inayojifanya miungu watu! Kwanza imepewa vyeo kikabila! Kichwani ni zero kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DPP ashitakiwe mahakamaccm? au ashitakiwe The Hague? Kumbuka mahakamaccm ni mali binafsi ya DPP ni vigumu Lema kupata haki labda kwa nguvu za mwenyezi mungu, lema hukumtolea vitisho bali kamshitaki DPP kwa wananchi wa Tanzania wajue mapungufu yake mapema.

Kama kuna ushahidi wa kutosha, Mhe. Lema anashindwa nini sasa kwenda haraka kushitaki The Hague?
 
Acha ujinga wako DPP hana madaraka hayo uliyomsimika kienyeji na wala hasubiri maelekezo ya wanasiasa kwani tayari anayo maelekezo ya wanasiasa wa CCM maelekezo ya kuwaonea kuwabambikia kuchelewesha kesi, na kama DPP anayo mamlaka ya kuingilia kesi yeyote katika stage yeyote hayo ni mamlaka haramu ndiyo yanayolalamikiwa kutumika vibaya kuwabambikia watu kesi za uhujumu uchumi kuchelewesha kesi makusudi na usumbufu mwingine mwingi sana, hapa hujaelimisha chochote juu ya DPP zaidi ya kujimwambafy tu kumtetea kwa mambo yake ya uonevu
Kama una uwezo wa kusoma na kuelewa, nakuomba kamsome DPP wetu hapa
DPP wa Tanzania: Ni Kihiyo wa Sheria, Msanii au Mbabaishaji?
P
 
Kama kuna ushahidi wa kutosha, Mhe. Lema anashindwa nini sasa kwenda haraka kushitaki The Hague?
Mahakama ya uhalifu wa kimataifa The Hague wametuma wapelelezi wao hapo Nchini wapo wanakusanya ushahidi wote wa unyanyasaji wenu wa CCM ikiwemo magerezaccm kuwapiga wabunge mdee na Bulaya kisha mfunguliwe kesi mkiwemo nyie watetezi wa udhalimu wote
 
Kama una uwezo wa kusoma na kuelewa, nakuomba kamsome DPP wetu hapa
DPP wa Tanzania: Ni Kihiyo wa Sheria, Msanii au Mbabaishaji?
P
Nimesoma vizuri naelewa jinsi DPP anatumia mamlaka yake vibaya kuwanyanyasa wapinzani, hayo mamlaka anapaswa ayatumie kutenda haki kupunguza mrundikano wa kesi kupunguza wafungwa magerezani siyo kutumia mamlaka yake kufanya kazi kinyume cha Sheria kwa mujibu wa fikra za CCM, moja ya kitu muhimu kinapaswa kufanywa na Bunge ni kurekebisha Sheria mbovu Sheria kandamizi, Sheria zinazompa mamlaka DPP kuingilia kesi yeyote kienyeji baada ya kutumwa na CCM, DPP apunguziwe mamlaka na Bunge kwani anayatumia kinyume badala ya kutenda haki.
 
Hakuvunja sheria, yeye kama waziri kivuli au Shadow minister hiyo ipo kwenye moja ya kazi zake....ameona kuna kesi ambazo zimechukua muda mrefu na huko kwenye hiyo wilaya watu wanauawa ovyo, hivyo ni jukumu la serikali au polisi kusema upelelezi huo umefikia wapi lakini serikali hizi za kijinga jinga za kijamaa zinaficha...Wewe unategemea Godbless Lema apate wapi information? Polisi hawataki na authority hawataki kutoa information, Lema ametoa kile alichoambiwa na ikatokea watu 14 kweli wameuawa...Hivyo ni jukumu la serikali au polisi kukanusha siyo DPP kwenda kwenye press conference na kuropoka aliyo yaropoka.

Sitaki kuingia kwenye malumbano ambayo naona hayatafika mwisho kwa sababu hakuna ambaye yuko tayari kubadili uelekeo wa mtazamo wake katika suala hili. Nilipoanza kuchangia hoja hii nilishauri kwamba wanasiasa wetu (pamoja na Mhe. Lema) wawe wanapata ushauri wa kisheria kabla ya kutoa matamko ya hadhara ili kuepuka matatizo ya kisheria yanayoweza kujitokeza. Ni vyema pia tunapotoa hoja kuhusu masuala ya sheria, tufanye utafiti kidogo kuhusu sheria zetu kwenye suala lililopo mezani. Mfano, ninaamini kama wewe Field Marshall 1 ungefanya utafiti kidogo kisheria kuhusu matamshi ya Mhe. Lema kwa upande mmoja, na tuhuma alizoleta DPP kwa upande mwingine, usingekuja kusema kwa kujiamini kwamba Mhe. Lema hajavunja sheria. Hata kama umejiamini kisheria kwamba hakuna kosa alilofanya Mhe. Lema, basi usingetaharuki na kudai kwamba DPP alikuja kuropoka kwenye vyombo vya habari wakati alichokifanya ni kuorodhesha mapungufu ya hoja za Mhe. Lema kuhusu vifo 14 vya wananchi wa Singida na uwezekano wa uvunjifu wa sheria ambao alisema ataupeleka Mahakamani ili Mhe. Lema apate nafasi ya kujitetea huko. Na kama Mhe. Lema ataona kwamba hakuvunja sheria, basi asiwe na wasiwasi kwenda kujitetea huko au kwenda kufungua kesi yake (kwa DPP) huko The Hague.
 
DPP kaongea kwenye vyombo vya habari kinyume cha Sheria kwanza anapaswa ajiuzulu kwa mapungufu hayo tu, Lema kujibu vya DPP kupitia vyombo vya habari hakuna kosa kisheria ingawa wewe umetumwa na DPP utengeneze mazingira ya kumbambikia Kesi ingine zaidi kama kawaida yenu, muogopeni mungu na mtambueni kuwa kuna maisha baada ya utawala huu wa Naibu Rais Daud Bashite na mtukufu magufuli kupita, kumbuka mtukufu magufuli mwenyewe alishasema watanzania siyo wajinga anajua na kuamini kuwa licha ya kuwanyanyasa wapinzani watanzania wameamua kuwa wavumilivu licha ya kwamba wanaumia sana mioyoni.
 
Watetezi wa CCM muogopeni mungu badala ya kutumia nguvu kubwa kumtetea DPP ni vyema mtumie nguvu hiyo kumkataza aache roho mbaya aache kuwabambikia kesi kuwanyanyasa wapinzani aache Tabia zote mbaya hapo mtakuwa mmesaidia kuliko kulazimisha watanzania wamwamini DPP wakati waneshuhudia akifanya vingi kinyume cha haki za binadamu na Sheria.
 
Back
Top Bottom