Lema amjibu DPP Mganga Biswalo, amtaka aache kutisha watu

Sizuii mtu kuona kwamba hoja yangu ina unafiki maana kila mtu ana haki ya kuwa na mtazamo wake. Lakini, mada inasema “Lema amjibu DPP...”. Hata hivyo, ukisikiliza vizuri “majibu” ya Mhe. Lema hayagusii kabisa hoja na tuhuma zinazomkabili kama alivyozitaja DPP kuhusu vifo 12 vya Singida. Badala yake, Mhe. Lema kazungumza mambo tofauti kabisa ikiwa ni pamoja na vitisho na kujisifu kwamba hamuogopi DPP nk. Kwa mantiki hiyo, Mhe. Lema ‘hakumjibu’ DPP bali kamtumia ujumbe.
Wasiwasi wangu ni kwamba je, vitisho alivyotoa Mhe. Lema vimo kwenye mipaka ya sheria? Pili, niligusia hili la wanasiasa kusema mara kwa mara, mmoja baada ya mwingine kwamba hawamuogopi mtu...mbona sasa linakuwa kama la ugomvi wa watoto kwenye mchezo wa chandimu?
Pointi ya Lema ni kuwa " DPP aache kuingilia uhuru wa mahakama" Hapo si mahali pa kujibizana ila ilikuwa mahali pa kumweleza DPP asimfuate fuate kwa sababu kesi ipo mahakamani.
 
The Hague wapo kweli wanakusanya ushahidi ili magerezaccm washitakiwe kwa kuwapiga wanawake na kuwadhalilisha kinyume cha haki za binadamu
Upuuzi gani huu? Unategemea wazungu wakusaidie maisha?
 
Ktk kipindi ambacho hutakiwi MTU kuogopa lolote nikipindi hiki...nafurahi kuona ofisi ya DPP haimuogopi MTU na nafurahia zaidi kuona MTU binafsi nambunge hamuogopi MTU/au taasisi ikienda hovyoohovyoo kuisema ijirekebishe.....nadhani muda wakuelewana ufike

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akiongea kupitia youtube chanel yake ya GLema Tv amemuonya DPP kuacha kutisha watu.





”…Mimi nimwambie DPP kwamba taifa hili linaanza kushuhudia kuwa yeye ni DPP wa kwanza anayeweza kutoka hdharani n akum-comvict mtuhumiwa. DPP siyo mahakama, wala DPP siyo Polisi…”

“…Katika shauri hili lililopo mkoani Singida nilipewa dhamana na polisi, baada ya kukaa lockup kwa takribani siku tatu. Na tulikubaliana nirudi polisi tarehe 24 mwezi huu, baadaye nikapigiwa simu kuwa natakiwa Polisi tarehe 19 jambo ambalo nilikuwa najiandaa nalo…”

“…Katika jambo hili nilipata fursa ya kuongea na IGP, na nilimpelekea meseji hata IGP ya majina haya ya watu ambao wameuawa kule Manyoni. Na nilimuomba IGP tuongee hata kabla sijaitaja ile list hadharani, nikifanya huvyo kama Mbunge, Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani na mtu ambaye nachukia kuona watu wanauawa hovyo…”

“…DPP katika mazungumzo yake, kitu ambacho kimenifanya nimjibu, kwanza hana mamlaka kisheria ya kuita vyombo vya habari kunihukumu kabla ya mahakama haijanihukumu. Hana hayo mamlaka kisheria; anakwenda kinyume kabisa na utaratibu wa kazi yake…”

“…Ile aliyofanya ni kudhihaki Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Setrikali katika taifa hili.

Swali ambalo watu wanatakiwa wajiulize ni kwanini DPP amekuwa na mamlaka makubwa sana katika Taifa hili, huyu tuliye naye. Ni kwanini DPP anaweza aka pre-empt maamuzi ya court? Ni kwanini DPP anatoka hadharani, anajaribu kumkemea Mbunge, kuchafua Mbunge na kumdhalilisha Mbunge wakati Mahakama bado haijafanya maamuzi wala kesi bado haijasikilizwa?...”

"...Maganga, Biswalo; Kama kuna mtu ameumiza watu wengi nchi hii, wewe ni aidha namba moja ama namba mbili..."

“…Mioyo ya watu wengi imepondeka. Hawakwambii pengine hawana guts niliyo nayo mimi; hawakwambii pengine wanaogopa wanasubiri hii regime ipite. Na itapita hii regime. Kwasababu hii regime haiongozwi na Mwenyezi Mungu wala Yesu….umetumia ofisi yako vibaya sana, na hata leo unatumia ofisi yako vibaya…”

…”Nakuhakikishia kama Mungu aishivyo, kwanza sikuogopi na siogopi unaweza ukaamua kitu gani juu ya maisha yangu kwasababu anayeweza kuamua maisha yangu ni Mwenyezi Mungu peke yake. Kwahiyo elewa kwamba sikuogopi na hakuna namna yoyote unaweza kunitisha nikakuogopa. Na nitaendelea kufanya kazi yangu. Fanya chochote…”

Safi sana. Mawe matupu.
 
Huu ndio uanaume bhana! Biswalo uwe makini kweli awamu hii itapita, huwezi jua itakayokuja na namna utakavyotendwa! maneno ya kamanda Lema usiyapuuze, huwezi kuwa na cheo hicho daima kuna kesho, na uwe unaweka akiba ya maneno.
 
Ila Dpp alikosea yeye siyo polisi inatakiwa asubiri polisi wamletee case aandae mashtaka kama alivyosema Lema
Nilimshangaa sana hadi nilijiuliza madaraka yake yameongezwa au! anyway, yana mwisho na mwisho wa ubaya huwa ni mbaya siku zote, muda ni mwalimu mzuri sana.
 
Pointi ya Lema ni kuwa " DPP aache kuingilia uhuru wa mahakama" Hapo si mahali pa kujibizana ila ilikuwa mahali pa kumweleza DPP asimfuate fuate kwa sababu kesi ipo mahakamani.
DPP wa Tanzania ni mkuu wa MaDPP wote Duniani anajua atakuwa DPP milele na milele hajui kuwa kuna leo na kesho kaamua kujitoa fahamu kuwaonea kuwabambikia kesi kuwanyanyasa watu kasahau kuwa malipo ni hapa hapa Duniani
 
Dah ingekuwa boxing ndio tungejua nani mbabe, bahati mbaya ni maneno maneno tu. 😅
 
Upuuzi gani huu? Unategemea wazungu wakusaidie maisha?
Mbona CCM kutwa wanaenda kuwaomba misaada mikopo? CCM mnaomba omba mpaka mfalume wa Morocco awajengee uwanja wa soka Dodoma kwani CCM ni wapuuzi kutegemea Wachina na wazungu? Wajibie CCM tuone jibu lako
 
CCM wakienda kuomba omba misaada mikopo kwa wazungu huwaita ni wafadhili Nchi rafiki, lakini hao hao wazungu wakianza kukemea uovu uonevu mabaya ya CCM huanza kuwaita ni mabeberu, CCM wakiwa na shida hunyenyekea lakini wakipewa hujimwambafy sana.
 
Ni wakati DPP aache ushetani wake ajitafakari amludie mungu asipange visasi vya kumkosoa Lema zaidi kwani sasa Duniani kote wamemjua ni mtu hafai kwenye jamii ya utu na kistaraabu
Ndo kanaongoza genge la kubambikia watu kesi,watu wako ndani mwaka wa saba sasa eti ushahidi aujakamilika sijui ushahidi ukamilika Kwa miaka mingapi.
 
Pili, niligusia hili la wanasiasa kusema mara kwa mara, mmoja baada ya mwingine kwamba hawamuogopi mtu...mbona sasa linakuwa kama la ugomvi wa watoto kwenye mchezo wa chandimu?
Na bado huoni sababu yake?

Hapo ndipo na wewe unapojiunga katika kundi maalum hata kama hujistukii!
 
Ktk kipindi ambacho hutakiwi MTU kuogopa lolote nikipindi hiki...nafurahi kuona ofisi ya DPP haimuogopi MTU na nafurahia zaidi kuona MTU binafsi nambunge hamuogopi MTU/au taasisi ikienda hovyoohovyoo kuisema ijirekebishe.....nadhani muda wakuelewana ufike

Sent using Jamii Forums mobile app
Upo sahihi kwenye mtu binafsi mbunge hamuogopi DPP lakini kwa upande wa DPP ni muoga anamuogopa Mbunge Lema ndiyo maana kaamua kutumia njia haramu kinyume cha Sheria kumhukumu Lema, muda wa DPP kujitambua kujitafakari kuacha uonevu ndiyo ufike sasa.
 
Ndo kanaongoza genge la kubambikia watu kesi,watu wako ndani mwaka wa saba sasa eti ushahidi aujakamilika sijui ushahidi ukamilika Kwa miaka mingapi.
Amerajirika sana kupitia hizo kesi za kuwabambikia watu kwa uonevu mkubwa, achunguzwe mali zake
 
Nchi ipo katika Ombwe la uongozi,alichokifanya Biswaro ni matumizi mabaya ya ofisi za Umma.
 
Kuna baadhi ya jamii huwa ni makosa makubwa sana kuwapa udereva yafaa waishie kwenye Kazi za utingo
 
Back
Top Bottom