Tetesi: Hawa ndio wanamkingia kifua singasinga wa IPTL

Tryagain

Member
Nov 23, 2021
66
436
Baada ya Ufisadi wa IPTL, PAP na Escrow kurejeshwa Bungeni, inatajwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Jaji Eliezer Mbuki Feleshi na Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) Sylvester Mwakitalu wako nyuma ya Singa Singa na kwamba ndio wanaopaswa kulaumiwa na kuchukuliwa hatua kwa kile kinachoelezwa kuwa ni muendelezo wa njama za wazi za kuihujumu serikali ya Awamu ya Sita.

Wachambuzi na Vyanzo mbalimbali ndani ya Serikali na watu wenye ufahamu wa muda mrefu wa Wizi huu wanaeleza kwamba kama si Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Mashtaka DPP walioko hivi sasa kuwa ndio walinzi namba moja wa Singa, basi huenda Sakata hili lenye muda mrefu pengine kuliko mengine yeyote katika historia ya nchi hii lisingefika hata Bungeni na kuzua taharuki kubwa yenye kugubikwa na mijadala mizito na ya kusikitisha kiasi cha kuleta taharuki na fadhaa kwa wananchi wa kawaida.

Cha kustaajabisha, licha ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kuweka wazi ufisadi wa karne na kutoa ushauri wa nini kifanyike, Pamoja na michango yenye tija na iliyojaa uzalendo wa Wabunge, inaonekana wawili hawa wana dhamira ya dhati na mipango kabambe zaidi kuhakikisha Nchi inaibiwa tena. Hii inatokana na Mwanasheria Mkuu na Mkurugenzi wa Mashtaka kukataa kusimamia Maamuzi halali ya Mahakama zote za hapa nchini ikiwemo Mahakama ya Rufaa ya Tanzania.

Hukumu ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ikiketi na Majaji watatu Chini ya Uenyekiti wa Jaji wa Rufani Ndika, katika Kesi ya Rufani Namba 190 ya Mwaka 2013 iliyotolewa tarehe 29 julai 2021 inatamka wazi kuwa Singa Singa hapaswi kuwa Mmiliki wa IPTL kwa kubatilisha uamuzi uliohamisha IPTL kwake. Uamuzi huo haukupingwa hata na Singa mwenyewe, lakini bado Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameshindwa kuishauri serikali kufanya maamuzi sahihi. Waswahili wanasema kikulacho ki nguoni mwako.

Maswali ya msingi kwa Mwanasheria Mkuu Feleshi na DPP Mwakitalu ni, licha ya hukumu zote za ICSID kuwepo dhidi ya Singa na Serikali, wawili hawa hawaoni hatari iliyopo kwa serikali endapo Benki ya Standard Chartered Hong Kong itaamua leo kuchukua hatua dhidi yake ? licha ya Singa kukiri na kusaini kuifidia Serikali kupitia Hati ya Maridhiano ( Consent Decree ) katika kesi ya Madai namba 90 ya Mwaka 2018 na ambayo mpaka sasa hajafanya chochote, licha ya Singa kukiri makosa katika Mahakama ya Kisutu na kuahidi kulipa katika kesi ya jinai iliyokuwa ikimkabili katika Mahakama ya Kisutu na ambayo amegoma kuitekeleza, Licha ya Kampuni ya Mechmar kuweka wazi kuwa haijawahi kuuza hisa zake kwa Singa na hivyo kuwepo kwa hukumu ya Mahakama ya rufaa dhidi ya Singa, Mwanasheria Mkuu Feleshi na DPP Mwakitalu wameendelea kumlinda Singa na hivyo kudharau mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Pamoja na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Singa singa aliingia pia katika makubaliano ya kukiri kosa na kuahidi kuilipa serikali. Mpaka sasa Mabilioni hayo hayajalipwa licha ya ahadi ya Mkurugenzi wa Mashtaka alipohojiwa na vyombo mbalimbali vya Habari nchini alieleza kwamba Singa akishindwa kulipa/kutekeleza makubaliano hayo basi hatua za kisheria zitafuatwa ikiwemo kurudishwa magereza na kujibu tuhuma zilizokua zikimkabili. Singa Singa hajalipa na kuna taarifa kuwa amekuwa hapa nchini wakati wote akiingia na kutoka bila wasiwasi wowote. Tunajiuliza tu, kiburi hiki anakitoa wapi ? Mkurugenzi wa Mashtaka aliwahi wakati Fulani kujipambanua kama mtu wa misingi na mwenye kufuata sheria, lakini sio kwa Singa. Kuna kila viashiria kuwa ulinzi wanaoutoa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Feleshi na Mkurugenzi Mwakitalu ndio hasa kinachompa Jeuri Singa kiasi cha kutamba kwa watu wake wa karibu kuwa hakuna la kumfanya na kwamba serikali itamlipa, iwe jua iwe mvua.

Nchi yetu imefikia mahali ambapo wenye Mamlaka ya kushauri na kusimamia Maamuzi ya Mahakama zetu ndio walanguzi namba moja wa maslahi ya nchi yetu. Cha kusikitisha zaidi ni kwamba Mamlaka za uteuzi ni kama zimepata ganzi dhidi yao.

Leo Bibi wa Kitanzania anaesadikiwa kukutwa na vipande kumi na mbili vya nyama ya swala amehukumiwa miaka 20 lakini Singa Singa mgeni mwenye kulitia hasara taifa hili miaka nenda miaka rudi yuko mtaani licha ya hukumu nyingi dhidi yake. Singa singa huyu ataendelea kuwa ni hatari kwa usalama wa taifa letu mpaka pale Mwanasheria Mkuu Feleshi na Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Mwakitalu watakapoamua kuwa Wazalendo na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria na kusimamia maamuzi halali ya Mahakama zetu na kwa Maslahi mapana ya nchi yetu.

Feleshi na Mwakitalu wanapaswa kujua kuwa dhamana walizopewa ni kwa niaba ya Watanzania na wanapaswa kusimamia hayo. Kuendelea kutoa ulinzi kwa Singa Singa kwa sasa ni kuiweka nchi rehani na historia itawahukumu.
 
Huyu Feleshi hakustahili kuwa hapo alipo kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
 
Shida sio Feleshi wala Mwakitalu shida iko kwa mamlaka ya uteuzi ya wawili hao. Unataka kusema haya unayayosema kiongozi wao hayajui? Kama hayajui huyo anafaa nini? Huenda washindwa kuchukua maamuzi sababu mkuu wa mhimili uliojichimbia zaidi amewapiga pin
 
hili suala lilikuwa mikononi mwa DPP na Mwanasheria Mkuu simuoni uhusika wa yoyote ukimya wake hauna uhusiano na lolote tusishangae siku akiwatolea uvivu huyo DPP na Mwenzie
 
Back
Top Bottom