Sasa kwenda Bukoba ni TZS 100K kutoka TZS 65K, LATRA mnafahamu hali halisi ya maisha ya Watanzania wenzenu?

Investigation Unit

Senior Member
Nov 26, 2023
164
220
Haraka haraka twendeni kwenye hoja,

LATRA wamepandisha bei za mabasi kwa wastani wa TZS 15 kwa Kila kilometa hasa kwa safari za Mikoani,

Mfano kutoka Dar es Salaam mpaka Bukoba ni sawa na 1,380 kilometa na kilometa moja kwa mabasi mazuri kidogo itakuwa TZS 67.84

Fanya hivi,
1,380km X TZS 67.84 = TZS 95,000 bado TZS 5,000 ya Agent.

Pia soma > LATRA yatangaza ongezeko la nauli za Safari za Masafa Marefu na Mafupi kuanzia Desemba 8, 2023

=====

Habari zaidi kutoka Gazeti la Mwananchi

Latra yatangaza nauli mpya za daladala, mabasi​


Dar es Salaam. Vicheko kwa wamiliki wa mabasi ya masafa marefu na daladala huku vIlio vikiwa kwa upande wa wananchi wa kawaida kutokana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra) kutangaza ongezeko jipya la nauli ambazo zitaanza kutumika Desemba 8, 2023 kama hakutakuwa na pingamizi lolote.
Latra kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wake, Habibu Suluo leo Jumatatu Novemba 27, 2023 jijini Arusha imetangaza nauli hizo mpya ambazo zimepanda kwa viwango tofauti kulingana na umbali na aina ya barabara.

Sababu kuu ya kupanda kwa bei hizo za nauli imetajwa kuwa ni ongezeko la gharama za uendeshaji ikiwamo kupaa kwa bei za mafuta (petroli na dizeli).

Nauli mpya
Suluo amesema daladala zenye ruti isiyozidi kilomita 10 itapanda kutoka Sh500 hadi Sh600, ruti ya kilomita 11 hadi 15 nauli itaongezeka kutoka Sh550 hadi Sh700 na ruti ya kilomita 16 hadi 20 nauli itaongezeka kutoka Sh600 hadi Sh800.

“Daladala zilizokuwa na ruti ya umbali wa kilomita 21 ha 25 nauli itapanda kutoka Sh700 hadi Sh900, zile zenye ruti ya kilomita 26 hadi 30 nauli itapaa kutoka Sh850 hadi Sh1,100,”amesema Suluo.

Taarifa iliyotolewa na Latra pia imesema, kwa daladala ambazo zilikuwa zinatoza Sh1,000 (umbali wa kilomita 31 hadi 35) bei itapanda hadi Sh1,300 na zile zenye ruti ambazo umbali wake ni kati ya kilomita 36 hadi 40, bei ya nauli itapanda kutoka Sh1,100 hadi Sh1,400.

Wakati nauli zikipaa kwa upande wa daladala kwa wastani wa asilimia 10, pia mabasi ya masafa marefu nauli itapaa kulingana na daraja la basi na aina ya barabara inayotumika.

“Mabasi ya daraja la kawaida katika barabara ya lami kila kilomita moja itatoza Sh48.47 kutoka Sh41.29 kama ilivyokuwa awali na kwa barabara ya vumbi daraja hilo litatoza nauli ya Sh53.32 kwa kilomita kutoka Sh51.61,”imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Pia, nauli itapanda kwa mabasi ya daraja la kati (luxury na semi-luxury) kwa barabara ya lami nauli itapanda kutoka Sh56.88 kwa kilomita hadi Sh67.84.

Aidha, Latra imesema kuwa viwango hivyo vipya vya nauli vinajumuisha tozo ya asilimia 0.5 inayotozwa na mamlaka hiyo.

Mchakato wa kupandisha nauli
Latra imesema ilipokea maombi kutoka kwa makampuni ya utoaji huduma ya usafiri wa abiria ya Super Feo Enterprises, ABC Classic na Happy Nation wakiiomba mamlaka ya kufanya marejeo ya nauli za mabasi kufuatia ongezeko la gharama za uendeshaji, ikiwemo kupanda kwa bei ya mafuta (petroli na diseli).
Aidha, katika taarifa yao Latra iliyosomwa na Suluo, imesema iliitisha mkutano na wadau wa sekta hiyo kwa ajili ya maoni kuhusu viwango vya nauli.

“Mamlaka iliitisha mkutano wa wadau uliofanyika Dar es Salaam, Jumatano, tarehe Oktoba 18, 2023, katika ukumbi wa Arnaoutouglou, ili kutoa fursa kwa makampuni haya kuwasilisha mapendekezo yao kwa wadau na kisha kukusanya maoni ya wadau,”imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Wananchi walia na bei
Kutokana na upandaji wa nauli hizo, maoni tofauti yameibuka kutoka kwa wananchi huku wakilalamikia bei hiyo kuathiri mnyororo wa uchumi.

“Sikubaliani na bei hizo kwasababu vigezo walivyotumia kupandisha bei hizo bado sijaviona kwasababu hali ya uchumi mtaani ni ngumu, wakipandisha nauli pia bidhaa zitapanda na bodaboda nao watapandisha tu,” amesema Godson Joram mkazi wa Mbagala Chamazi.

Naye Eva Luka mkazi wa Kimara amesema kwa mara ya kwanza kuzizoea nauli hizo itakuwa ngumu ila hakuna namna.

“Kwa mara ya kwanza itakuwa ngumu kwa sababu nitakuwa sijajipanga lakini baadaye tutazoea tu, ila ni maumivu jamani maana kila kitu kitapanda bei, wasafirishaji wa bidhaa kupitia mabasi nao wataongeza bei,”amesema.
 
Ni ngumu kumpangia mtu binafsi bei za kupangia wateja wakati gharama ya vipuri wala kwenda Benki kwenye kukopa haukumsaidia....

Ndio hapo linakuja suala haya mambo ya transport ni mambo ya jamii wala haikuwa busara kuua Kampuni kubwa za UMMA; ingawa bora zaidi ni kuwakeza kwenye mass transportation vitu kama train n.k. viwe na bei rafiki, na efficient; ama sivyo tutaendelea kuonana wabaya (kupigana wenyewe kwa wenyewe kumbe adui yetu wala sio necessarily mtu anayebangaiza aweke gari lake barabarani)
 
Ni ngumu kumpangia mtu binafsi bei za kupangia wateja wakati gharama ya vipuri wala kwenda Benki kwenye kukopa haukumsaidia....

Ndio hapo linakusa suala haya mambo ya transport ni mambo ya jamii wala haikuwa busara kuua Kampuni kubwa za UMMA; ingawa bora zaidi ni kuwakeza kwenye mass transportation vitu kama train n.k. viwe na bei rafiki, na efficient; ama sivyo tutaendelea kuonana wabaya (kupigana wenyewe kwa wenyewe kumbe adui yetu wala sio necessarily mtu anayebangaiza aweke gari lake barabarani)
Hapana faida wanapata kubwa sana hata sasa,

Basi inachukua abira 60


Fanya 60X 95,000
Ni ngumu kumpangia mtu binafsi bei za kupangia wateja wakati gharama ya vipuri wala kwenda Benki kwenye kukopa haukumsaidia....

Ndio hapo linakusa suala haya mambo ya transport ni mambo ya jamii wala haikuwa busara kuua Kampuni kubwa za UMMA; ingawa bora zaidi ni kuwakeza kwenye mass transportation vitu kama train n.k. viwe na bei rafiki, na efficient; ama sivyo tutaendelea kuonana wabaya (kupigana wenyewe kwa wenyewe kumbe adui yetu wala sio necessarily mtu anayebangaiza aweke gari lake barabarani)
Faida ni kubwa sana ,
Fanya

95,000X 60 = 5,700,000
Mafuta ni 700,0000

Faida ya 5M ni supper profit,
Waziri Mkuu angalia hii,
 
Amfungua nchi!

Mahela yamemwagwa mtaani wananchi wanajikotea tu baada ya kubanwa na bwana yule!

Ameongeza ajira kila kona!

Amepandisha mishahara na madaraja ya watumishi.

Anaupiga mwingi!


Na bado mpaka akili ziwakae sawa.
Ndani ya miaka 2 ya utawala wa mama nauli ya daladala imeshapandishwa mara mbili..mpaka anatoka madarakani nauli za daladala zitakuwa 3000 na nauli za mikoani zitafikia Hadi 200,000
 
Haraka haraka twendeni kwenye hoja,

LATRA wamepandisha bei za mabasi kwa wastani wa TZS 15 kwa Kila kilometa hasa kwa safari za Mikoani,

Mfano kutoka Dar es salaam mpaka Bukoba ni sawa na 1,380 kilometa na kilometa moja kwa mabasi mazuri kidogo itakuwa TZS 67.84

Fanya hivi,
1,380km X TZS 67.84 = TZS 95,000 bado TZS 5,000 ya Agent,


Kigoma Kasulu 101000 hii sio haki kabisa kutoka kwenye 60000
 
Back
Top Bottom