LATRA yawaonya wanaopandisha Nauli za Mabasi kiholela

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1697556662192.png

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetoa onyo hili baada ya kuwepo kwa malalamiko ya Wananchi kuhusu baadhi ya Wamiliki na Kampuni za Usafirishaji Abiria kuamua kufanya mabadiliko ya Nauli kinyume na masharti ya Leseni zao.

Taarifa ya Mkurugenzi wa LATRA, CPA Habibu J.S. Suluo imeeleza kuwa pamoja na Mamlaka hiyo kukutana na kujadiliana na watoa huduma hao, baadhi wameonesha nia ya wazi ya kupinga na kupandisha Nauli, kitendo kinachochukuliwa kama nia ovu dhidi ya umma.

Awali, Mdau wa JamiiForums.com alilalamikia upandishwaji holela wa nauli ambapo Mamlaka imetoa tahadhari kwa watoa huduma wanaokusudia kujipangia au kutangaza nauli kinyume na Sheria na Kanuni za Usafirishaji wasitishe haraka azma hiyo na kusubiri mchakato unaoendelea kuhusu kufanya marekejo ya nauli.
 
Back
Top Bottom