Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Baadhi ya wahusika wa mabasi ya abiria wanaochezea mifumo ya usalama na mwendo katika mabasi wamenaswa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Mkoa wa Arusha.
Afisa Mfawidhi wa LATRA Mkoa wa Arusha, Joseph Michael ameongoza zoezi la ukaguzi katika maeneo tofauti katika maegesho ya magari Jijini hapo ambapo amesema madereva wanaofanya hivyo wanahatarisha maisha ya abiria ambao wamekuwa na imani kwa vyombo hivyo.
Ameongeza kuwa mamlaka hiyo haitamuonea muhali mtu yeyote ambaye atakiuka taratibu zinazosimamiwa na mamlaka hiyo.