BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,119
Mwezi mmoja tangu Serikali iruhusu safari za mabasi kwa saa 24, tathimini ya mamlaka za usimamizi imeonyesha kuwepo ukiukwaji mkubwa wa sheria na kanuni za usalama barabarani, hali inayohatarisha usalama kwa abiria na mali zao.
Kutokana na ukiukwaji huo, ndani ya muda huo mabasi 759 yamekamatwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) kwa kushirikiana na Kikosi cha Usalama Barabarani kwa kuzidisha mwendo na kuchezea mfumo wa VTS unaodhibiti na kutoa taarifa za kasi ya gari.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Habibu Suluo na Kamanda wa Trafiki, Ramadhan Ng’anzi ilieleza kati ya mabasi hayo, 723 yalipewa onyo na mengine kusitishiwa leseni.
“Mabasi yaliyositishiwa leseni mpaka mamlaka itakapojiridhisha kwamba wamebadilika ni 36.
“Kati ya mabasi 246, asilimia 80 (mabasi 197) yamebainika yanaendeshwa kwa mwendo kasi kati ya kilomita 86 hadi 89 kwa saa, huku asilimia tisa yakiendeshwa kwa kilomita 90 hadi 103 kwa saa,” ilisema.
Madereva waliofungiwa
Orodha ya Mabasi yaliyofungiwa