Ndahani
Platinum Member
- Jun 3, 2008
- 18,119
- 9,049
Nimejiuliza sana, kwanini lamination ya mizigo inayodhaniwa inaweza kuchafua ndege mfano ndoo ya samaki iwe lazima kufanyiwa lamination tena kwa gharama kubwa vile?
Abiria umefunga vizuri samaki zako kwenye ndoo safi lakini unalazimishwa kufanya lamination.
Kama wenye ndege hawataki kuchafua ndege yao basi wao ndo wawajibike kutengeneza sehemu ya kuhifadhia mizigo michafu.
Siku moja nimeunganisha kibox na kindoo kidogo nikaambiwa lamination ni 15,000 ilihali mzigo mmoja ni 5,000.
Halafu mbona Mwanza tu ndo wenye hizi lamination?? Au hii ni biashara ya nani??.
Pale Mwanza mpaka samaki wanakagua ndoo nzimaa. Nasikia huko nyuma kuna nyara zilipita kwa njia hiyo ya kubeba ndoo ya samaki. As a precaution, wanakagua kama hawana akili nzuri.
Viwanja vya ndege mara nyingine vinakuwa kero sana kwa sababu ya ukaguzi. Ila ndio salama ya wasafiri. Kuna wapumbavu wakiachiwa hata kila siku kujilipua hewani hawaoni shida.