Jinsi biashara ya uchuuzi wa samaki ilivyonipa msoto wa hasara

Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,563
3,708
Wakuu salaam,

Hakika hii itabakia katika kumbukumbu zangu,nimejalibu kufupisha tiririka nayo.

Katika harakati zangu za kazi nilifanikiwa kupata dili flani niliingiza pesa yakutosha nilimtembelea ndugu yangu 1 alinipa wazo.

Biashara ya uchuuzi wa samaki,kiukweli hii biashara inafaida ukibahatika maana inachangamoto nyingi sana yataka moyo, alinielekeza vizuri sana jinsi ya kuifanya niliona ni wazo zuri.

Kwakuwa sikuwa mzoefu wabiashara husika nilimtafuta mtu mzoefu nilimwambia twende tufanye hii biashara faida ikipatikana nitakupa pesa ya mtaji maana yeye akiitaji pesa ya mtaji alafu hajui anaipataje, tukakubaliana vizuri.

Tuliangalia soko la samaki Songea linaendaje samaki gani wanaweza kuuzika,tukapata jibu aina ya samaki wanaitwa samunge wanapatikana ziwa Eyasi Arusha hao pekee hawapo kabisa sokoni hii ni kutokana ni ziwa ambalo linafungwa maji yakipungua linafunguliwa maji yakiongezeka kwaiyo kama tukileta samaki wake watauzika.

Maandalizi yalianza ili twende na mda tuliwapata wadau walio kuwepo kwenye ziwa wakatuambia bado wiki mbili ziwa lifunguliwe.

Nilikuwa nina cash. Tsh. Mil.1,500,000/=

Gharama zikaanza kutumika:

Usafiri wote wawili Tsh.laki 154,000/=,

Waya wa kuanikia samaki,

Kutengeneza jiko lakubanikia samaki pamoja na chanja yakuanikia

Kuni za kubanikia samaki tulinunua kwa uwingi ili tusiangaike

Turubai 3

Miti yakujengea hema wenyeji wanaita (bajaji)

Tulikaa siku 40,kila siku tulitumia Tsh.elfu 5,000/= kwa ajili ya chakula cha siku 1

Matumizi mengine ya kambini Tsh.30,000/=

Jumla ilitugharimu kama Tsh.laki 599,000/= kila kitu kukamilika.

Cash balance iliyokabakia Tsh. Laki 901,000/=

Hapo ndipo kazi ilianza tulifanya kazi kwa bidii sana jamaa alinipa ushirikiano mzuri alikuwa mwaminifu alinishauri na kunifunza vitu vingi sana.

Ugumu wa samaki za ziwa wa kubanika kama njia tuliyotumia sisi ni kazi inatuma sana usiku na mchana unatakiwa uwe makini ucheze na moto wakuni na makaa unaungua sura lazima ukunje kama umekula pilipili kichaa.

Changamoto ni kupata samaki kwa haraka wavuvi kuuza kwa mgeni ni ngumu kila mvuvi ana bosi wake anaye muuzia ila kwakuwa sisi tulifika mapema ilkuwa ni rahisi angalau.

Changamoto ya pili ni ndege wakubwa wanaitwa "ndege joni"(si rasmi) hatari hao aisee wanakula samaki wakivamia kwenye eneo la samaki dk 30 tu kama hayupo wanamaliza.

Tulizilinda wakati wote usiku na mchana. Usiku ndio mbaya sana tulikuwa tunafanya kazi mpaka saa 5 usiku tukijalibu kulala tu,ndege wanakuja kula samaki hawalali usiku kucha tukiangaika nao mpaka asubuh ikifika kazi zinaendelea.

Tulifanya uku tunauchovu wa usingizi tukipata mda mchana tunalala kidogo
Tulijitaidi tumalize pesa tuondoke tukaliwai soko.

Tulinunua samaki za Tsh.Laki 881,000/= jumla ya samaki elfu 29,366 kwa bei samaki Tsh.30/= kutoka kwa wavuvi moja kwa moja.

Makadirio ya mauzo samaki 1 sokoni anauzwa Tsh.100/= adi Tsh. 150/=

Tulinunua samaki 29,366 tufanye 366 zililiwa na ndege joni,kualibika na kutafuna wenyewe maana ni tamu.
Tulipomaliza kukusanya mzigo maandalizi ya safari yalianza.

Gharama za usafiri tulikopa ilikuwa Tsh. Laki 350,000/= tulisafirisha kwenye fuso kwenda songea mjini.

Tulipanda kwenye ilo gali tulikuwa hatuna nauli pesa yote iliisha tulibakisha elfu 20,000/= kwa ajili yakula njiani,tulikuwa kama watu 18 tuliopanda ilo gari nyuma na maboksi ya samaki.

Tulianza safari saa 3 usiku,tulitembea kitambo kidogo kwenye majira ya saa 10 usiku gali iliaribika tulilala pale.

Asubuhi tunapewa taarifa kuwa kuna kifaa kimearibika kinapatikana Arusha mjini wakati sisi tupo eneo moja linaitwa kidongo chekundu mbali kidogo kufika karatu.

Hapo ndipo hasara ilipoanzia,

Tulilala siku mbili tulipata wenyeji kibishi warembo wakimbulu hapo ndio kwao tuliwanyoosha,hiyo spear hakikupatikana Arusha ilibidi waagizie Dar-es-Salaam.

Siku ya 3 usiku saa 4 safari ilianza tena,tulitembea usiku na mchana njiani ni changamoto nyingi sana matukio mbalimbali pamoja na kukamatwa na polisi.

Siku yapili tulifika Makambako saa 10 usiku mwenye gali alituambia amehairisha safafi ya kwenda Songea anaenda mbeya kwa hiyo wenye mizigo ya Songea tuliteremshiwa na tulirudishiwa Tsh. Elfu 50,000/=

Kwakweli iyo elfu 50 ilitusaidia tulikuwa hatuna kitu kabisa kwakuwa ilikuwa usiku tulitafuta geust tulilala asubuhi tulikula breakfast kubwaa kabisa tulituliza akili tukajadiliana tunafikaje songea na tulibakiwa naTsh elfu 15,000.

Tulipata wazo tumpigie dalali wa soko la Songea atutumie nauli ili tukifika atauza mzigo wote alafu atakata baada ya mauzo yote kukamilika.

Alitutumia Tsh. Elfu 50,000/= tukapata gari ya makaa ya mawe zinatoka Zambia dereva kwake ni dili hawezi kukataa tukapakiza samaki zetu lilikuwa ni box two in one ni kubwa sana kulipandisha si chini ya 5 walioshiba.

Saa 8 mchana tulianza safari,saa 2 usiku gali iliaribika filter ilikuwa inavujisha,tulisaidiana na dereva kulitengeneza japo hatukuwa mafundi ila kumsaidia angalau kukaza nati ilikuwa ni polini kilimani yani hatari tupu na kuna matukio ya ajabu ajabu lakini wanaume tukasema lolote na liwe.

Tulifika Songea saa 11 alfajiri.

Asubuhi tulifungua mzigo ili tuangalie samaki maana zimesafiri takribani wiki 1 njiani
"Ng'ombe wa maskini hazai" samaki zilivunjika yani ni ungaunga tupu kwasababu zimekauka sana siku 7 njiani ni nyingi na zile habari za shusha pandisha mara 3 basi ikazidi kukata samaki.

Wastani asilimia 50% ya samaki zote zilikatika ziliuzwa kwa kupima kwenye kindoo kikubwa kwa bei ya hasara jumla ilipatikana Tsh.Laki 300,000/=

Jumla ya Samaki wazima ambazo 50% ni elfu 14,000 waliuzwa kwa bei ya Tsh.100/= ilipatikana Tsh.Mil.1,450,000/=
Jumla ya mauzo yote ni Tsh.Mil.1,750,000/=

Gharama za usafiri kwa ujumla Tsh.Laki 400,000/=
Faini za njiani Tsh. Laki 100,000/=
Dalari yake ni 10% ya mauzo yote alichukua Tsh. Laki 175,000/=

Pesa niliyokapata baada ya kutoa kila kitu nilibakiwa na Tsh. Mil.1,025,000/=
Jamaa yangu nilimpatia Tsh. Laki 200'000/= maana hasara tu kwaiyo kifutia josho.

Nilibakiwa na Tsh.Laki 825,000/= sikukata tamaa nikaona ni moja ya changamoto ya biashara ilivyo.

Nikajipanga nikaondoka tena hii ilikuwa Iringa uko nako kizaa kizaa kingine zaidi kilinikuta..

Awamu nyingine nikipata wasaa nitawaletea yaliyojili

Mwendelezo...

Jamaa yangu yeye alijichanganya ziwa Rukwa uko kwenda kujalibu bahati yake.

Mimi niliamua kwenda bwawa la Mtera eneo moja linaitwa Migori mkoani Iringa.

Kwakuwa nilikuwa tayari nina uzoefu sikuwa na hofu japo sijawai kufika iyo sehemu nikathubutu kwenda kupambana kivyangu vyangu nikavaa sura ya kazi kidume.

Nilifika migori hayupo ninaemfahamu ata mmoja ata ndugu wakikabila sikumuona maana sikuwa mtu wa jamii yao.

Lakini uzoefu wa maeneo kama yale ulinifanya nimpate mwenyeji siku ileile kwa hiyo.

Katika Tsh. Laki 825,000/=
Nilifanya matumizi yafuatayo:

Nauli kutoka songea mpaka site

Nilinunua unga kiloba 1 cha kg 50

Turubai 1 na viazi vitamu (makaba)ndoo 1

Mpaka ninafika Migori nina Tsh. Laki 650,000/=

Tanzania watu wake ni wakarimu sana,

Mwenyeji wangu niliyempata ni mvuvi kwaiyo hapa nafuu ya maisha ilikuwa chini kidogo kwa sababu nililala kwenye kibanda chake,jiko la kubanikia samaki lilikuwepo.

Usiku jamaa akienda kuvua akirudi asubuhi ananiuzia samaki, tena anakuta na viazi vimeiva freshi anakunywa chai tunatia story uku tunasaidiana kazi mchana ukifika tunaliumua dongo la kiume mboga samaki siku zikisonga.

Akiniuzia samaki 1 Tsh.35 katika pesa niliyokabakia nayo nilitenga Tsh. Laki 600,000/= inunue samaki na Tsh. Elfu 50,000/= iwe ni akiba lolote linaweza kutokea.

Matumizi yakawa kama ifuatavyo

Kuni za elfu Tsh. 50,000/=

Nauli usafirishali Tsh.elfu 50,000/=

Nilinunua samaki wa Tsh. Laki 500,000/=
Jumla ya samaki kwa bei sh. 35 ni samaki elfu 14,285.

Awamu hii kidume nilichakaa kazi nilifanya mda mrefu kwa sababu mwenyeji sio kila wakati alikuwa ananisaidia nilipambana nilinuka jasho mpaka nikalizoea nywele timtim sitamani kitu sina habari na mtu nina uchungu na pesa yangu.

Nilikaa takribani siku 30 sijaoga yani nilivurugwa nguo nilikuwa sibadili nipo kama sipo,niliongeza umakini wautendaji kazi kuhakikisha hasara hairudii tena.

Migori ni kwenye kambi ya wavuvi ni porini lakini pana starehe kila aina wanawake,pombe,ukitaka kuoga maji ya ziwa ni wewe vijana hapo wapo wengi sana pana fursa ya biashara sana hasa ya chakula.

Starehe yangu mimi ilikuwa kwenda kuangalia mpira mwaka ule France ilichukua kombe la dunia Final dhidi ya Cratia,akina Modric, rakitic,mandukic n.k

Jumla ya samaki elfu 14,285
Nilizisafilisha moja kwa moja mpaka Songea mimi mwenyewe nilibakia.

Samaki elfu 13,000/= zilifika salama zikauzwa kwa bei ya Tsh. 160.

Ziliuzwa kwa bei nzuri kwa sababu ya ubora na ukubwa na samaki ngumu kuliko zile za awali.

Jumla ya Pesa iliyopatikana ni Tsh.Mil. 2,080,000/=

Dalari alichukua 10% yake ambayo ni laki 208,000/=

Nilibakiwa na Tsh. Mil. 1,872,000/=

Hapo niliacha hii biashara baada kurudisha pesa yangu ikiyoniumiza kichwa usiku na mchana nikaenda kufanya shughuli zangu za kila siku zilizniingizia pesa kama ile.

Usikate tamaa maisha ni kupambana thubutu unaweza ukianguka inuka anza upya.

FB_IMG_15894551700614157.jpg

Samaki wameanikwa baada kutolewa utumbo badae wabanikwe

FB_IMG_15894551004447099.jpg


Samaki wametoka kuvuliwa

images-9.jpeg


Vitendea kazi vya wavuvi
 
Kwanini ulikuwa unakamatwa na Polisi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tulikamatwa na polisi mara 2, mara yakwanza Iringa kwa ajili ya kupakiza abiria kwenye gali ya mizigo na walidai samaki hawajakidhi ukubwa wakuvuliwa.

Mara ya pili Wakati tunaenda songea kuna check-point moja ivi tulikamatwa kwa ajili yakupakiza chakula kwenye gari ya makaa ya mawe wakati tunajua makaa ya mawe ni sumu.
 
Tulikamatwa na polisi mara 2,mara yakwanza Iringa kwa ajili ya kupakiza abiria kwenye gali ya mizigo na walidai samaki hawajakidhi ukubwa wakuvuliwa.
Mara ya pili Wakati tunaenda songea kuna check-point moja ivi tulikamatwa kwa ajili yakupakiza chakula kwenye gari ya makaa ya mawe wakati tunajua makaa ya mawe ni sumu.
Duh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Polisi wa Tanzania wanataka sababu ya kukumata? Hata kama huna kesi watakupa kesi
Sio kweli.

Fuata taratibu za kufanya hiyo biashara uone kama utakamatwa.

Next time tafuta vibali kutoka fisheries alafu safirisha mzigo wako, cha kwanza uhakikishe hao samaki ni size inayokubalika, hakikisha umepata kibali cha kusafirisha, hakikisha umelipa ushuru au tozo eneo lile ulilokusanyia.

Ukikamilisha hilo polisi akikukamata usimpe hela mwambie akupeleke kokote anakotaka. Kwa taarifa yako polisi hawana uelewa na mambo ya sheria za uvuvi kikubwa wanakudandi wakiona una samaki wadogo na wakiuliza kibali cha kusafirisha huna ndo ushaingia hasara.

Watu wengi mnatoa hela kwa polisi kwa sababu huwa tangu mwanzo hamjafuata utaratibu wa biashara ya samaki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom