LAKINI, hiyo shombo amletea nani?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Pilau ale yeye tena kwa kificho huku akjijua ni mwizi tu.............akiwa kwenye chumba alichokishindilia komeo tena la viro ili asije kubambwa na mwenye mlo wake.............baada ya uporaji wa pilau ya watu aja mtaani na huanza kutubehulia.........na kuacha mafuta ya pilau na vipunjepunje vyake mdomoni.......

Hivi, hiyo shombo amletea nani?

Mwingine ametoka kumtafuna kuku wa watu khalafu kwa kasi ya ajabu hurukia kitandani kwa mkewe na kumshulizia manukato yatokanayo na siagi ya samli aliyopikiwa kuku wa watu aliyemtafuna ............kwa kufanya hivyo ni mithali ya kumtambia mkewe ya kuwa amejinoma kuku wa watu..........lakini swali ni

Hivi, hiyo shombo amletea nani?

Kwa nini asiende bafuni akaoga na kutakata na abakie akichekwa na dhamira yake badala ya kuwaadhibu waliokuwamo na wasio kuwamo..........kama ile hadithi ya panya aliyekusudiwa kuuawa na mtego lakini mtego ukamnasa nyoka ambaye mwenye nyumba aliposikia umenasa akawahi kummalizia panya gizani na matokeo yake akaumwa na nyoka mwenye hasira na kufa hapohapo.........matangani ng'ombe na kuku walichinjwa kumsindikiza mwendazake............na hivyo kukamilisha maono ya panya ya kuwa mtego ulomlenga yeye wataingia waliomo na wasiokuwamo........

Hivi walakini...........hiyo shombo amletea nani?
 
Pilau ale yeye tena kwa kificho huku akjijua ni mwizi tu.............akiwa kwenye chumba alichokishindilia komeo tena la viro ili asije kubambwa na mwenye mlo wale.............baada ya uporaji wa pilau ya watu aja mtaani na huanza kutubehulia.........na kuacha mafuta ya pilau na vipunjepunje vyake mdomoni.......

Lugha uliyotumia inahitaji utulivu sana ili mtu aweze kuchangia, any way nikipata breakfast nitaangalia uwezekano wa kuchangia:coffee:
 
Eti mwingine kalishwa mijichips kuku huko na kidume cha jirani...anakuja kitandani na kuanza kuachia hewa zisizovutika sawia puani kwa mwenzie..hilo shombo amleteee nani??

Ana lambwa lambwa mdomo kama paka akiwa na kijike au kidume pori, anarudi nyumbani hataki hata kunawa mdomo anataka akugushishe mdomo wake..hilo shombo amletee nani??

Kaachia, kanyonywa nyonyo weeeee hata kuliko anavyoweza kuwamchia mwanae, eti baadae anarejea nyumbani anataka kumnyonyesha mtoto wake mchanga pasipo hata kujishwafi uzuri....eti hilo shombo anamletea nani??

Karuhusu kidume shume kimguse sehemu ambazo hata wewe mumewe/boy friend hujawahi kugusa, kanogewa huko, anarejea nyumbani, anakugezia nawe uguse huko asijue wewe sie yule aliyezoea mambo hayo..sasa hilo shombo la mtandao huo wenye wateja kidogo amleteee nani??
 
Ngonjera nzuri sana hii, umefundishwa na nani? Mk'were mzee wa misemo?

ni kiitafsiri kwa kimombo cha level yangu.............hapakaliki hata chembe......pambana na hiki kiswahili.......
 
Ruta
Aksante kwa mada hii hivi ni kweli mla nje hujisahau na kuja na shombo kweli??Haogopi kubambwa?

ajivunia kufuli la viro..........lakini basi hata aoge lol.........
 
Eti mwingine kalishwa mijichips kuku huko na kidume cha jirani...anakuja kitandani na kuanza kuachia hewa zisizovutika sawia puani kwa mwenzie..hilo shombo amleteee nani??

Ana lambwa lambwa mdomo kama paka akiwa na kijike au kidume pori, anarudi nyumbani hataki hata kunawa mdomo anataka akugushishe mdomo wake..hilo shombo amletee nani??

Kaachia, kanyonywa nyonyo weeeee hata kuliko anavyoweza kuwamchia mwanae, eti baadae anarejea nyumbani anataka kumnyonyesha mtoto wake mchanga pasipo hata kujishwafi uzuri....eti hilo shombo anamletea nani??

Karuhusu kidume shume kimguse sehemu ambazo hata wewe mumewe/boy friend hujawahi kugusa, kanogewa huko, anarejea nyumbani, anakugezia nawe uguse huko asijue wewe sie yule aliyezoea mambo hayo..sasa hilo shombo la mtandao huo wenye wateja kidogo amleteee nani??

zihurumie mbavu zangu zaniuma kupita kiasi.................
 
Bwana Ruta naona leo umetumia Tafisida kubwa sana hapa
Ngoja na mie nitafute namna ya kutumia Tafisida ili twende sambamba

tafisida nd'o nini?.......................Umeniacha kwenye mataa........
 
kajisaidia kwa jirani na kuchamba hajachamba eti anarud nyumbani huyoo mpaka kitandani,hilo shombo amletea ani?kapigwa mabusu,midenda kedekede hata mswaki hajapiga,eti hilo shombo amletea nani?kapiga magoli sita huko uanjani eti vuvuzela la ushindi aja kupigia ndani jaman
hilo shombo la mijasho amletea nani?hahahah ruta umewaza nini?
 
mh, haya bana. ila kwa mwenye utambuzi na busara hawezi cheka, bali atatafakari, atathmin pia ajitathmini kisha asikitike.
 
Ruta,

Haya mambo ya kuja kusemana humu ndani ya JF, si mazuri. Tuheshimiane kabisa bana.

Sasa wewe umejuaje haya yote na mie sikukuambia?

(Hapa wengi tu wamewaza hayo maneno hapo juu, hihihiiiii...... Hata Ruta mwenyewe ni Mbovu.)
 
Ruta we mzaramo? mbona maneno mengi mtego weye?

Ngoja nijitafsirie kiiraqw niielewe vizuri
 
Ruta,
Rejea kisa cha baba kutanguliza salam kabla hajafika home ulikitoa paleee...ndo utakubakuli kuwa binadamu hana asili wala fasili.
 
Rutashubanyuma
umenikumbusha zamani kidogo (1989) Mara tu baada ya shairi langu kutoka kwenye gazeti la "Uhuru" nilipata barua nyingi sana nyingine za kutaka... Ushairi ni jambo jema sana na watu wengi ambao ni wajuvi wa kutumia Lugha wao pia huwa ni werevu na weledi kwenye mambo mengi sana. Aakh! Bahati mbaya sana siku hizi matumizi ya lugha si jambo la kutiliwa maanani sana!!
 
Last edited by a moderator:
Ruta,

Mtu anayefanya hayo yote ni wa hovyo na huna sababu ya kumuuliza swali lako...

Babu DC!!
 
Hili somo sio la kucheka wala kufurahi
Mwenye uelewa atatafakari na kujiuliza maswali mengi na kujihukumu mwenyewe kuhusu hilo shombo analokuja nalo kwa mkewe au mumewe au kwa mpenziwe
Tena ajipangusa mdomo kama mbwa mwitu asionekane kabisa kuwa amekula chochote
Huku dhamiri ikimsuta kwa alilolifanya huko alikokuwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom