Laki tano tu unaweza badilisha historia

Laki tano tu unaweza badilisha historia

sumbua kichwa japo kidogo acha kuonyesha upumbavu wako hapa, bank tellers wametumika hapo kama mfano flani hivi na sio kwamba kawadharau!!!!na kusema laki tano sio kwamba uchukue mshahara wa mwezi mmoja na kusepa bush kwenda kulima BUT ni kuonyesha kwamba unaweza kuwa unafanya kazi katika taasisi yoyote ile iwe ya umma au binafsi na kile unachopata unawekeza kwenye project nyingine ambayo itakuingizia kipato cha ziada...na sio lazima iwe kilimo!!!!Jifunzeni kufikiri nje ya boksi, kuweni na plan B katika maisha inkesi chochote kikitokea kwa plan A yako uwe na pakujishiza japo kwa muda wakati unaangalia unatokaje.
Naona povu linakutoka sana punguza kula omo. Kisha rudi usome upya hiyo mada utaona jinsi alivyoeleza matumizi ya laki tano na pia heading imetaja bank tellers moja kwa moja usijifanye unaelewa sana kuliko uelewa wenyewe
 
kijijini watu hawalimi wanachimba chimba aridhi.....unakuta mzee ana watoto kumi amelima robo heka ya mahindi....mtu huyo atawezaje kujikwamua.....vijana tufanye mabadiliko.....bank tellers wabaki vijana wa form 4 na darasa la saba 7.....form six na kuendelea tuhamishie uwezo wetu wa kufikili kwenye kutumia rasili mali zetu.....ni ujinga mzungu anakuja pensi(kaptula)tz anaondoka na na mabilion ya pesa....wazungu wote waliokuja kutafuta hela wako maporini na wanapiga hela sana
hehehe[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji14]
 
  • Thanks
Reactions: 365
View attachment 328257

SHULE BILA ADA:

Laki tano, Mshahara wa Ma-Teller wa Benki hapa mjini Laki Tano, Bei ya TECNO PHANTOM mpya kabisa kwa kujishau Snapchat na Istagram Laki Tano, Bajeti ya Mafuta ya SUBARU mwezi Mzima.... Laki Tano , Bajeti ya HEINEKEN 100 KWA wanywaji wa Pombe... HELA FLANI MBUZI TU ambayo wengi wanaona HAINA ISHU .

Lakini , Laki Tano hii ina uwezo wa kukodi shamba Ekari 13 pale Kiteto au Mpwapwa na ikakutengenezea Million 15 baada ya Miezi MITATU kwa kulima Matikiti maji.

Laki Tano hii hii ina uwezo wa kununua SIMTANK la lita 5000 ( ndoo 250 za lita 20) ambal inaweza kutumika kusolve shida ya maji mtaani kwako kwa kuuza ndoo 1 Sh 500 na ukaingiza 125,000 kwa kila SIMTANK unalouza.

Laki tano hii hii inaweza kulima Ekari 2 za Maharage pale Simanjiro na baada ya Miezi Minne ukavuna si chini ya Million 3 ambazo zitaexpand kilimo chako MARA 6 zaidi ya Mwanzo na Kuexpand Kipato chako mara 6 zaidi ya Mkupuo wa kwanza!

Laki Tano hii ina uwezo wa kulima Matikiti Maji Ekari 2 na zikakupa si chini ya Milion 2 na nusu baada ya SIKU 90!

SHIDA NI: Kila mtu anataka akae mjini AONEKANE SAMAKI SAMAKI, aonekane Muvi Mlimani City, Apost akiwa Escape 1, Apige Snapchat akiwa 777 ... Kila mtu anataka aonekane MDARISALAMA... Yuko mjini

MDADA yupo radhi aishi mjini kwa kuuza mwili wake kuliko kwenda Ruaha Mbuyuni Kuinvest kulima Vitunguu... Ataonyesha saa ngapi CROP TOP yake Mpya kutoka YAHYA BOUTIQUE? Sistaduu alime vitunguu?? Hapana, bora atafute Danga la Laki 2 akalale nalo!!

Big Up kwa wadada wote wajanja WALIOINVEST KWENYE KILIMO., kila Jumamosi wakati wewe unaona sifa kwenda HIGH SPIRIT LOUNGE Wadada wenzako wako RUVU wamekodi mashamba wanalima mpunga, unashangaa Huyu mdada anafanya nini kumbe mwenzio analima.

KUDOS kwa wanaume wenzangu ambao wamegundua siri kwamba kuuza Sura hakulipi ma wameinvest Shamba, kila weekend wanapotea kwenda kusimamia nyanya na pilipili Bagamoyo.

Utaendelea kuwashangaa wenzio wanatajirika na kudhani kila mtu anauza UNGA hapa mjini, Kilimo ndio unga mpya... nnadhani mkandamizaji amenuunua ile BMW X6 kwa episode za ORIJINO COMEDY? Thubutu, nenda MBARARI umkute amejaa Matope akipalilia Mpunga wake ndo utajua na wewe kwa nini unapanda Bajaji mpaka leo na kubaki kulalamika tu.

Je laki 5 yako, unafanyia nini?

#letitshine

Huu ni uwongo. Hata milioni 2 haziwezi kufanya mambo haya aliyotaja. Nam challenge atoe ushuhuda kamilifu wa matumizi shilingi kwa shilingi wa mtaji wa hizo laki 5 kwenye kilimo hadi upate faida anayodai.
 
Hiyo laki tano inahusisha na huyo muekezaji na fedha ya kujikimu mpaka avune hayo matikiti maji yake Masanja hapo kuwa mkweli Mimi ni mjasiriamali Laki tano kwa hizo siku tisini mpaka uvune hazitoshi hata kidogo.....toa ushauri ulio komaa usilete maigizo kwenye maisha . Kilimo ni kazi na inahitaji kujitoa hasa na si kwa hiyo 500lk
 
Huu ni uwongo. Hata milioni 2 haziwezi kufanya mambo haya aliyotaja. Nam challenge atoe ushuhuda kamilifu wa matumizi shilingi kwa shilingi wa mtaji wa hizo laki 5 kwenye kilimo hadi upate faida anayodai.
Teller vipi???
 
ni uongo mtakatifu huu...huwezi fanya kilimo anachosema kwa 500,000/=, aweke mchanganuo hapa wa ZANA ZA KILIMO, PEMBEJEO , MBENGU , VIUWADUDU NA VIUWATILIFU..... HAJAONGELEA SUALA LA MAJI ANAFANYA KILIMO CHA ASILI AU CHA UMWAGILIAJI!!!
 
Nami pia nataka nikalime Karanga. Je nimkoa gani unafaa?
 
ni uongo mtakatifu huu...huwezi fanya kilimo anachosema kwa 500,000/=, aweke mchanganuo hapa wa ZANA ZA KILIMO, PEMBEJEO , MBENGU , VIUWADUDU NA VIUWATILIFU..... HAJAONGELEA SUALA LA MAJI ANAFANYA KILIMO CHA ASILI AU CHA UMWAGILIAJI!!!

Wengi wanao ongea hivo hawalimi na hawajawahi lima
Mkulima halisi anajua hiyo hela haitoshi labda analima mchicha
Afu ukitaka angalia washauri wengi kuanzia wa kilimo, biashara, wengi wao hawalimi na hawana biashara
 
ujira wangu upo hii idara ya KILIMO ,UMWAGILIAJI NA USHIRIKA, kwa hiyo pesa hata kilimo cha pilipili hufanyi.... labda mboga mboga .... tena uwe na eneo lako na uhakika wa maji ni muhmu zaidi
 
View attachment 328257

SHULE BILA ADA:

Laki tano, Mshahara wa Ma-Teller wa Benki hapa mjini Laki Tano, Bei ya TECNO PHANTOM mpya kabisa kwa kujishau Snapchat na Istagram Laki Tano, Bajeti ya Mafuta ya SUBARU mwezi Mzima.... Laki Tano , Bajeti ya HEINEKEN 100 KWA wanywaji wa Pombe... HELA FLANI MBUZI TU ambayo wengi wanaona HAINA ISHU .

Lakini , Laki Tano hii ina uwezo wa kukodi shamba Ekari 13 pale Kiteto au Mpwapwa na ikakutengenezea Million 15 baada ya Miezi MITATU kwa kulima Matikiti maji.

Laki Tano hii hii ina uwezo wa kununua SIMTANK la lita 5000 ( ndoo 250 za lita 20) ambal inaweza kutumika kusolve shida ya maji mtaani kwako kwa kuuza ndoo 1 Sh 500 na ukaingiza 125,000 kwa kila SIMTANK unalouza.

Laki tano hii hii inaweza kulima Ekari 2 za Maharage pale Simanjiro na baada ya Miezi Minne ukavuna si chini ya Million 3 ambazo zitaexpand kilimo chako MARA 6 zaidi ya Mwanzo na Kuexpand Kipato chako mara 6 zaidi ya Mkupuo wa kwanza!

Laki Tano hii ina uwezo wa kulima Matikiti Maji Ekari 2 na zikakupa si chini ya Milion 2 na nusu baada ya SIKU 90!

SHIDA NI: Kila mtu anataka akae mjini AONEKANE SAMAKI SAMAKI, aonekane Muvi Mlimani City, Apost akiwa Escape 1, Apige Snapchat akiwa 777 ... Kila mtu anataka aonekane MDARISALAMA... Yuko mjini

MDADA yupo radhi aishi mjini kwa kuuza mwili wake kuliko kwenda Ruaha Mbuyuni Kuinvest kulima Vitunguu... Ataonyesha saa ngapi CROP TOP yake Mpya kutoka YAHYA BOUTIQUE? Sistaduu alime vitunguu?? Hapana, bora atafute Danga la Laki 2 akalale nalo!!

Big Up kwa wadada wote wajanja WALIOINVEST KWENYE KILIMO., kila Jumamosi wakati wewe unaona sifa kwenda HIGH SPIRIT LOUNGE Wadada wenzako wako RUVU wamekodi mashamba wanalima mpunga, unashangaa Huyu mdada anafanya nini kumbe mwenzio analima.

KUDOS kwa wanaume wenzangu ambao wamegundua siri kwamba kuuza Sura hakulipi ma wameinvest Shamba, kila weekend wanapotea kwenda kusimamia nyanya na pilipili Bagamoyo.

Utaendelea kuwashangaa wenzio wanatajirika na kudhani kila mtu anauza UNGA hapa mjini, Kilimo ndio unga mpya... nnadhani mkandamizaji amenuunua ile BMW X6 kwa episode za ORIJINO COMEDY? Thubutu, nenda MBARARI umkute amejaa Matope akipalilia Mpunga wake ndo utajua na wewe kwa nini unapanda Bajaji mpaka leo na kubaki kulalamika tu.

Je laki 5 yako, unafanyia nini?

#letitshine
Aende atoe shukrani kanisani kwa anayempa mibaraka, afya na uhai
 
Mimi niliwahi kulima mihogo ya KAEMP ina soko sana huko UGANDA, nililima miche elfu tatu, nlipo vuna, nikapata karo nikaja hapa Dar nikajiunga na chuo cha ualimu STMARYS nimemaliza nasubiri post, kazi ya kilimo hiyo. Big up Massanja
Safi sana mkuu kwa kutoa ushuhuda.
Dar kwa vijana ni bom linalolipuka kila siku,ila kila mtu na maumivu yake.
Maana ukiangalia nyumba ya masanja,kwa haraka gharama alizotumia kuijenga haifiki hata 100m.
Sasa je ni kweli ananshindwa kumiliki pesa ndogo hiyo?au tuseme nyumba na magari vyote ni 300m,je ni kweli pesa hiyo anashindwa kuiingiza kwa kazi zake na kilimo na biashara zake nyingine?
Kuna watu wanakata Elfu 50 kwenye Bia kila weekend,ukiwauliza wanakuambia mtu hafiisiki kwa Bia.Hizi ndio akili zetu

Ukimuona mtu anapesa halafu anafanya starehe usimuige,ujue yule alisota saaana,na wengine huwa wanamiradi nje ya jiji wanakuja Dar kutumia,ukiiga umepotezwa.
 
Masikini akishapata lazima ... ilie mbwata. Hivi Masanja wakati unazunguka na bidhaa jijini ukiwa mmachinga hayo mashamba yalikuwa yamekwisha huko kwenu Ludewa. Leo hii unabeza kazi za wateja wako waliokuweka mjini kitambo.

Kila kazi ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi na mzunguko wa life kiujumla, ni mpuuzi pekee awezaye kufikiri wote tunaweza kulima nyanya au auze maji na wote tuwe na maisha mazuri. Hao wanaolipwa laki 5 wote wakitoka ofisini wakauze maji au kulima vitunguu atanunua nani?

Kilimo kingekuwa simple kama unavyobwatuka unadhani nani angekuja mjini kufanya kazi ya laki 5 unayoibeza, mbona Masanja ulikuja ukakomaa hapa hadi ukatoka baada ya kuungua sana na jua. Ulishakuwa hadi HOUSEBOY wewe, leo hii teller wamuona kama hana akili au hana malengo na maisha haya.

Mmekaa tu mnaongelea kilimo kana kwamba ni rahisi saaana. Mngejua watu wanaozewa na mazao mashambani huku kwa kukosa masoko. True vipo vinavyolimwa vinalipa haraka lakini havistawi nchi nzima na kwingineko gharama za kuvilima si ndogo.

Masanja hukutoka kwa sababu una akili kuliko vijana wanaosota,huo ni mzunguko wa maisha tu na bahati iliyochagizwa na kipawa. Ulijituma ndio lakini haimaanishi wasiotoka hawajitumi. Chunga kauli zako bro.
Anafanya nini cha maana si uhuni, ulofa wa kuchekesha. Ni kukosa akili kichwani ndio unaenda kwenye upuuzi wa kuchekesha. Hiyo kila mtu anaweza kufanya mradi ujitoe utu uwe hayawani, basi. Sioni tofauti ya Masaja na malaya anayejiuza utu wake kufanya uchekeshaji. Na malaya anafanya kuwafurahisha watu kama yeye anavyofanya, wote ni uhuni
 
Bahati mbaya sana, ukisoma unajifanya mzuri kufanya risk analysis. Opportunities zote waziogopa. Wasiosoma hawana sana hayo, ndio maana wanafanikiwa zaidi.
Ni kweli Mkuu,wasomi waoga saana.
Mie ninayo mifano kwenye biashara yangu ya Bodaboda,na ukifungua uzi humu utakuta wasomi kibao waogaaa.
Kuna siku nilienda kusajili Bodaboda yangu mpya nikamkuta mdada mmoja anazo 19 anaenda kurenew na kuongeza ya 20.Nikasema hili jembe kweli,anaongoza kwa kuibiwa bodaboda ila anakomaaa hivyo hivyo.
Hivi karibuni nilimpigia anasema anaingia kwenye biashara ya Gari za mizigo.
Sasa chuku mfano kwa yeye alieanza biashara hii miaka mingi sana,hemb piga hesabu ya Hesaba anayoingiza kwa mwezi anayoingiza
Tsh:50,000 x 20 bodabodas x 4 weeks = 4m kwa mwezi

Sasa mtu kama huyu tangu ameanza kufanya biashara unafikiri hawezi kufanya makubwa,na mtaani unamuona wa kawaida,then unaweza kuona anauza unga kumbe alisota muda mrefu saaana,tena ali risk miaka ya mwanzo kwa kuuza kiwanja ili anunue bodaboda,na alianza na tatu tu,leo hii zimezaa 20 na anaingia kwenye biashara ya gari za mizigo.

Maisha kujipanga tu,la sivyo kila mtu utamuona anauza unga,wakati mtu anasota,wewe upo na Smart phones za bei mbaya,pombe,madem telee,ukifika muda wa mafanikio ya mwenzio unaona kama amepata juzi tu wakati mwenzio amesota muda mrefu saana.

Leo hii watu mnauziwa viwanja chanika mpaka 1m,unasikia mtu anakuambia ahhh,kiwanja gani,nani akae chanika.dharau kibaooooo,siku chanika ikiwa mji mkubwa ndio wa kwanza kulalamika.

Na watu wa Jiji wanatabia ya kuigana hadi lugha,yaani ukumuuliza kijana mmoja kati ya 10,basi 8 of them wanamajibu yanayofanana,kuonyesha kwamba wamekariri maisha
 
Tumieni akili wadau. Aliandika anayoyahisi yapo sahihi.

We ukiona tofauti unapita kuleee..

KILA MTU KWA NAFASI YAKE AKIKOMAA IPASAVYO ANATOKA.(anatusua maisha) LABDA TU MUNGU APENDE VINGINEVYO....
 
ni uongo mtakatifu huu...huwezi fanya kilimo anachosema kwa 500,000/=, aweke mchanganuo hapa wa ZANA ZA KILIMO, PEMBEJEO , MBENGU , VIUWADUDU NA VIUWATILIFU..... HAJAONGELEA SUALA LA MAJI ANAFANYA KILIMO CHA ASILI AU CHA UMWAGILIAJI!!!
Elimu, elimu, elimu, hapo katoa mfano WA laki tano akimaanisha kuwa hata kwa hela kidogo Tu unaweza tajirika na si lazima uanze na kidogo
 
Back
Top Bottom